Abari zetu Informations de contact, plan et itinéraire, formulaire de contact, heures d'ouverture, services, évaluations, photos, vidéos et annonces de Abari zetu, Centre d’affaires, Mulongwe, Uvira.

14/05/2022

🇨🇩
Rais Felix Tshisekedi yupo njiani kapunguza idadi ya Wafanyakazi Ikulu ili kapunguza gharama kufatana na kwamba gharama za maisha kwa wananchi zinaendelea kupanda.

14/05/2022

USALAMA MDOGO MASHARIKI MWA DRCONGO 🇨🇩

“...Hatuwezi kuendelea na kuhesabu vifo k**a vile watu ambao hatuna uwezo wa kuwatetea wananchi wenzetu wanaoendelea kuuawa hovyo, kutokana na uzembe fulani.
Kwa matukio haya, imeonekana kwamba wenda jeshi letu ndilo likawa halina nguvu au labda hao waasi wananufaika na njama zao na baadhi ya viongozi wa jeshi letu.
Hilo halikubaliki...”, Rais Felix Tshisekedi amesema.

14/05/2022

🇨🇩🌏
DRCongo miongoni mwa mataifa yenye miundombinu mibovu zaidi duniani.

14/05/2022

MAUAJI YA RAIA MASHARIKI MWA DRCONGO 🇨🇩

Spika wa bunge la taifa Mh Christophe Mboso Nkodia awataka Wabunge kuchanga pesa kila mmoja dola 100 kwenda kuomboleza pamoja na wananchi wa majimbo ya Ituri na Kivu-kaskazini mashariki mwa nchi, haswa watoto ambao ndio wahanga wakubwa.

14/05/2022

USALAMA MDOGO MASHARIKI MWA DRCONGO 🇨🇩
Ubalozi wa Marekani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo waonya kwamba wenda kukatokea shambulio la kigaidi mjini Goma jimboni Kivu-kaskazini katika siku za hivi karibuni.
Lakini licha ya onyo hilo, viongozi wa serikali mjini humo wamewaambia wananchi kwamba wasihofu kutokana na taarifa hizo, na kuwahakikishia kwamba mji upo salama na kila kitu kipo chini ya ulinzi wa serikali, hivyo kila mtu aendelee na shughuli zake za kila siku.

14/05/2022

USALAMA MDOGO MASHARIKI MWA DRCONGO

Burundi yasema ipo tayari kuanza matayarisho ya kuzungumuza na makundi ya waasi wa nchi hiyo wanaoendesha mapigano mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ili kuwaondoa ugenini na kuwarejesha nchini.

11/03/2022

Jemadari wa FARDC John Numbi ambaye alikimbia nchi kuepuka mashtaka yanayomkabili kuhusiana na kifo cha mwanaharakati wa kutetea Haki za binadamu, Floribert Chebeya na dereva wake Fidel Bazana, taarifa zimesema kwamba askari huyo ameonekana nchini Russia kwa Vladmir Putin.

11/03/2022

“.. Malipo ya kupata Paspoti hayajapandishwa, bado ni zilezile dola 99 za kimarekani.
Watu wamekuwa wakilalamikia kupandishiwa bei ya malipo katika Ofisi mbalimbali ndani na nje ya nchi, bila kutambuwa kwamba na wenyewe ndio wanaosababisha hali hiyo...
Wengi wao wanapohitaji kuhudumiwa, hutaka mambo yote wafanyiwe kwa wakati mmoja bila kusubiri kufuata utaratibu uliopangwa na serikali...
Hiyo nayo inaweza kuwa moja ya sababu za kupandishiwa bei...”, Christophe Lutundula, Waziri wa mambo ya nje.

18/02/2022

🔴🇨🇩" Quelques Rwandais copieusement frappés par la diaspora congolaise en France !

Les congolais en colère contre la réclamation de Paul Kagame d'une partie de la RDC se sont farouchement attaqué aux rwandais en France...
quelques-uns ont été copieusement frappés " la police française est finalement intervenue".

Adresse

Mulongwe
Uvira
DRC

Téléphone

+243858970198

Site Web

Notifications

Soyez le premier à savoir et laissez-nous vous envoyer un courriel lorsque Abari zetu publie des nouvelles et des promotions. Votre adresse e-mail ne sera pas utilisée à d'autres fins, et vous pouvez vous désabonner à tout moment.

Contacter L'entreprise

Envoyer un message à Abari zetu:

Partager