Chozi la heri summary

Chozi la heri summary Get notes for chozi la heri mwongozo

15/01/2022

Which chapter summary do you need?
Note each chapter cost shs10
Kindly pay and forward the M-PESA message to 0706087083 and receive notes within 5 minutes through WhatsApp or Facebook messenger
☑️ Chapter 1
☑️ Chapter 2
☑️ Chapter 3
☑️ Chapter 4
☑️ Chapter 5
☑️ Chapter 6
☑️ Chapter 7
☑️ Chapter 8
☑️ Chapter 9
☑️ Chapter 10

 🌲_from_chozi_heri_summary
24/12/2021

🌲_from_chozi_heri_summary

https://www.facebook.com/106808101855157/posts/107120121823955/?app=fbl
12/12/2021

https://www.facebook.com/106808101855157/posts/107120121823955/?app=fbl

Hadithi inaanza kwa taharuki kuhusu uvumi uliogeuka mnong'ono ukaeneza wasiwasi-hofu. Wasiwasi ulikuwa vibanda vitabomolewa vote. Watu wakubwa walitaka kuchukua makao ya watu ili kuendeleza ujenzi wao. Kwa Mzee Mago ndiko kituo cha kuzungumzia juu ya haki zao. Yeye huwakusanya wenzake iii wajadili juu ya haki zao za kuishi pale wanapochagua. Wanahojiana mambo juu ya:

1. Kustahili kuishi kwa amani na furaha popote nchini mwao.

2. Namna ya kuruka vikwazo vya sheria vilivyowekwa ili watu wadogo wasiweze kupoteza mali zao.

3. Kushawishiana watafute wanasheria waaminifu iii kutatua (mazonge ya sheria). Wanadai kuwa wanasheria waaminifu wameadimika — Bhakuna haki siku hizi.

4. Kunasihiana na kuamshana juu ya kukubali maendeleo yanayopiga kasi nchini mwao.

5. Maendeleo yanahitaji mchango wa kila mtu — mdogo kwa mkubwa, wa k**e kwa wa kiume.



Mtu hawezi kukimbia ukweli, upya na usasa hutazamiwa kuleta mafanikio kwa watu wote. Mzee Mago huwaonya wauchunguze huo upya na usasa waujue jmst uhvyokaa —utaleta faida au hasara. Umaskini sio ujinga. Watu maskini wangeshauriwa wangeweza kuonyesha watakavyochangia maendeleo ya nchi yao. Watu wadogo hukasirika kwani wao hufanywa kuwa k**a takataka. Hasira yao ndiyo inayowapa motisha wa kusema na kujitetea. Wakubwa walidai kuwa jiji limejaa na halina nafasi tena, suluhisho ni kubomoa baadhi ya mitaa. Jiji limejaa hoteli, mikahawa, majumba ya Mall, maduka n k. Kwa hiyo, suluhisho la uhaba wa nafasi jijini ni kubomoa sehemu zingine.



Mzee Mago aliwaleta wenzake pamoja kupigania haki za hapo Madongoporomoka —pasibomolewe.

Baadhi ya wanyonge hawa wanataka wapewe visenti vyao vichache vaondoke. Wengine wanadai, hakuna kuondoka. Wanataka vvabaki pale pale na kupigania haki zao. Kabwe alisisitiza kwa nguvu kuwa wakubwa hawataweza, kwani wanaogopa umma wa Madongoporomoka. Bi. Suruta aliwatahadharisha kuwa wakubwa hawaogopi kitu chochote.



Wakati mjadala ukiendelea, chakula cha pale mga

Tazama filamu ya chozi la heri Sura  1 and 2. Bonyeza hii link utazame sahii.
04/10/2021

Tazama filamu ya chozi la heri Sura 1 and 2.
Bonyeza hii link utazame sahii.

01/08/2021

Do you need chozi la heri summary note of all chapter? Inbox the word chozi la heri and get all guide you want to the set book at low price 5shs per chapter or questions

01/06/2021

JAZANDA.



Hii ni mbinu ya kulinganisha vitu viwili moja kwa moja bila kutumia viunganishi. Katika ukurasa wa 4 tunasoma; "Mwangeka alisema Ridhaa kupitia kwa sauti ya mawazoni mwake, kumbe wewe ni sawa na yule Mwangeka wa kihistoria ambaye kivuli chake kikitembea siku zote mbele yake, ambaye mwili wake ulikuwa kaka tu, roho yenyewe iliishi nje ya kaka hillkwa kutotaka kudhibitiwa? Umewezaje kunusurika? Kumbe wadhifa waliokupa wa kwenda kudumisha Amani katika mashirika ya kati umetokea kuwa wongovu wako?"

Hapa, Ridhaa anamlinganisha Mwangeka wa kisasa na yule Mwangeka wa kihistoria.

Katika ukurasa wa 6 tunasoma; "Basi niambie, baba, unatumia mantiki gani kusema kuwa sisi si watoto wa miaka hamsini? Je, miaka hamsini ya uhuru imetukuza kiuchumi au tumebaki kuwa wategemezi wa hao hao ambao walitupa uhuru?"

Hapa kuna ulinganishi kati ya miaka hamsini ya uhuru wa taifa, na miaka hamsini ya kuzaliwa kwa hawa watu ambao bado hawajajikomboa kutokana na ule ukolonio mambo leo.



Katika ukurasa wa 8 tunasoma; "Ardhi ya mzee Mwimo Msumbili ikawa haitoshi kuyalea madume yake ishirini "

Vijana wake Mzee Mwimo wanalinganishwa na madume ishirini.

Katika ukurasa wa 29 tunasoma; "Nilihisi kwamba ingekuwa bora k**a tungefia katika mazingira tuliyoyazoea; huenda hata tungepata wa kutuomboleza, kuliko kufia ugenini "Sasa umeanza kufikiria k**a wafuasi wa nabii Musa ambao baada ya kukosa chakula huko jangwani, walimshutumu kwa kuwatoa kule Misri. Walidai kuwa huko Misri wangekula matikitimaji yao pamoja na kuwa watumwa!"

Hapa, msemewa anafananishwa na wale wana wa Israeli waliOtamani kuwa ni heri wangekufia huko misri badala ya kupelekwa jangwani na Musa kufia huko.



2. TASHIHISI/UHUISHAJI.



Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho uhai sifa za kiumbe mwenye uhai, au sifa za kibinadamu. Katika ukurasa wa 3 tunasoma; "Alijiona akiamka asubuhi ambayo ilizaa usiku wa jana, usiku ambao ulitandaza kiza katika maisha yake "



Usiku unapewa sifa za kuwa na uhai na ku

16/05/2021

SURA YA PILI



Ni siku kumi tangu kuondoka kwa Kaizari na wenzake na kujipata katika mazingira haya mageni. Si mageni kwani ni mumo humo kwao kwani si ughaibuni wala nchi jirani. Pahali hapa ni kambi au mabanda yaliyosongamana. Waliokuwa nacho na wachochole wote wako pamoja katika kambi hii.



Kuna kiasi fulani cha usawa. Japo wanasema kuwa wanadamu huwa sawa kifoni, kuna tofauti katika mandhari wanamofia. Kuna wanaofia zahanati za kijijini na wapo wanaolala maumivu yao yakiwa yamefishwa ganzi katika hospitali za kifahari huku wakiliwazwa na mashine. Kuna wengine ambao hufia kwenye vitanda vya mwakisu vitongojini baada ya kupiga maji haramu(pombe haramu) k**a nzi ambao kufia dondani si hasara. Kuna tofauti pia mitindo ya mazishi na hata mavazi ya mwenda zake na wafiwa. Hata majeneza yenyewe huhitilafiana.



Katika kambi la kina Kaizari mipaka ya kitabaka imebanwa. Kwani, hata waliokuwa navyo sasa hivi wanang'ang'ania chakula haswa uji. Hata aliyekuwa waziri wa Fedha miaka mitano iliyopita yumo katika kambi hii aking'ang'ania chakula na wenzake. Mvua kubwa inanyesha na matone mazito kuwaangukia wanawe wakembe wa Ndugu Kaizari-Lime na Mwanaheri. Hana hata tambara duni la kuwafunikia. Ubavuni amelala mke wake Subira. Anaonekana kuwa siye yule Subira wa awali kwani mwonekano wake niwa kukatisha tamaa amevimba sana baada ya kutendewa unyama na binadamu wengine.



Kwa mbali anaonekana Ridhaa, akitafuna kitu fulani kinachofanana na mzizi-mwitu. Ni kinaya Daktari mzima, Mkurugenzi mzima wa Wakfu wa Matibabu nchini kula mzizi!



Kaizari anaanza kusimulia yaliyojiri siku ile baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya. Anasema kuwa baada ya kutawazwa kwa kiongozi mwanamke(wengine waliamini hafai kuongoza) mambo yaliharibika. Watu wakashika silaha kupigania uhuru wao, uhuru ambao walidai hawakupewa wakaupigania. Wakatoa kauli kuwa wanaume watatumikishwa kwa walivyofanywa enzi hizo katika visakale vya jirani . Waliona kuwa kiongozi mwanamke atawarudisha pale walikotoka.

02/05/2021

Sura hii inapoanza, Ridhaa alikuwa amesimama kwa maumivu makali huku mikono kairudisha nyuma ya mgongo wake uliopinda kwa uchungu. Amelitazama wingu la moshi ambalo linamkumbusha ukiwa aliozaliwa nao na ambao anahofia kuwa angeishi na kuzikwa nao. Alipogeuka alitazamana ana kwa ana na moto ambao uliteketeza jumba lake la kifahari. Walioangamia mie ndani ni Terry (mkewe Ridhaa),bintiye Tila, Mkewe Mwangeka(Lily) na mjukuu wake Becky. Tukio hili linamkumbusha mambo kadha yaliyotokea hapo awali yakiwemo mlio wa kereng'ende na bundi usiku wa kuamkia siku hii ya kiyama. Milio hii ilimtia kiwewe zaidi kwani bundi hawakuwa wageni wa kawaida katika janibu hizi. Alikumbuka akimwambia Terry kuwa milio hii ni k**a mbiu ya mgambo ambayo ikilia huenda kukawa na jambo. Terry ambaye kawaida yake ni mcheshi hakunyamaza ball alimwambia Ridhaa kuwa kwake lazima kila jambo liwe na kiini. Terry alishangaa ni vipi daktari mzima alikuja kujishughulisha na mambo ya ushirikina. Terry anamkumbusha mmewe kuwa aliwahi kumwambia kuwa ni vizuri kuiacha mielekeo ya kijadi ambayo huyafifilisha maendeleo. Anazidi kumuuliza hata iwapo jambo likawa atafanya nini? Ndipo Terry anamjuza kuwa la muhimu ni kumlaani shetani kwani Iiandikwalo ndilo liwalo. Mazungumzo haya baina ya Terry na mmewe Ridhaa yalikuwa ya mwisho kabisa kutokea Terry akiwa hai. Ridhaa sasa anajutia kuwa angelijua angelitumia kila sekunde za uhai zilizokuwa zimesalia kumuuliza mkewe maswali ambayo sasa yameivamia akili yake. Machozi yalifulika machoni mwake na kuulemaza uwezo wake wa kuona na ndipo moyo wake ukamwonya dhidi ya tabia yake ya k**e ya kulia pindi tu akumbwapo na vizingiti ambavyo ni kawaida ya maisha. Aliyakumbuka maneno ya marehemu mamake kuwa machozi ya mwanamme hayapaswi kuonekana mbele ya majabali ya maisha. Siku hii Ridhaa hakujali la mama wala la baba; alijiskia k**a mpigana masumbwi aliyebwagwa na kufululiziwa makonde bila mwombezi. Alisalimu amri na kuyaacha machozi yamvamie yatakavyo.

02/05/2021

Sura hii inapoanza, Ridhaa alikuwa amesimama kwa maumivu makali huku mikono kairudisha nyuma ya mgongo wake uliopinda kwa uchungu. Amelitazama wingu la moshi ambalo linamkumbusha ukiwa aliozaliwa nao na ambao anahofia kuwa angeishi na kuzikwa nao. Alipogeuka alitazamana ana kwa ana na moto ambao uliteketeza jumba lake la kifahari. Walioangamia mie ndani ni Terry (mkewe Ridhaa),bintiye Tila, Mkewe Mwangeka(Lily) na mjukuu wake Becky. Tukio hili linamkumbusha mambo kadha yaliyotokea hapo awali yakiwemo mlio wa kereng'ende na bundi usiku wa kuamkia siku hii ya kiyama. Milio hii ilimtia kiwewe zaidi kwani bundi hawakuwa wageni wa kawaida katika janibu hizi. Alikumbuka akimwambia Terry kuwa milio hii ni k**a mbiu ya mgambo ambayo ikilia huenda kukawa na jambo. Terry ambaye kawaida yake ni mcheshi hakunyamaza ball alimwambia Ridhaa kuwa kwake lazima kila jambo liwe na kiini. Terry alishangaa ni vipi daktari mzima alikuja kujishughulisha na mambo ya ushirikina. Terry anamkumbusha mmewe kuwa aliwahi kumwambia kuwa ni vizuri kuiacha mielekeo ya kijadi ambayo huyafifilisha maendeleo. Anazidi kumuuliza hata iwapo jambo likawa atafanya nini? Ndipo Terry anamjuza kuwa la muhimu ni kumlaani shetani kwani Iiandikwalo ndilo liwalo. Mazungumzo haya baina ya Terry na mmewe Ridhaa yalikuwa ya mwisho kabisa kutokea Terry akiwa hai. Ridhaa sasa anajutia kuwa angelijua angelitumia kila sekunde za uhai zilizokuwa zimesalia kumuuliza mkewe maswali ambayo sasa yameivamia akili yake. Machozi yalifulika machoni mwake na kuulemaza uwezo wake wa kuona na ndipo moyo wake ukamwonya dhidi ya tabia yake ya k**e ya kulia pindi tu akumbwapo na vizingiti ambavyo ni kawaida ya maisha. Aliyakumbuka maneno ya marehemu mamake kuwa machozi ya mwanamme hayapaswi kuonekana mbele ya majabali ya maisha. Siku hii Ridhaa hakujali la mama wala la baba; alijiskia k**a mpigana masumbwi aliyebwagwa na kufululiziwa makonde bila mwombezi. Alisalimu amri na kuyaacha machozi yamvamie yatakavyo. Katika mito ya machozi n

Address

Nairobi

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Chozi la heri summary posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share