Augus nyakwar mother.

Augus nyakwar mother. The page is about small scale farming

15/07/2023

Kennedy Ouma (Boy)Baba Jera third born to Tino and atoti nyakadero, three years now since he missed,was brother to wakina B,kiddos,R,lelo,T,nya many,etc😧

06/07/2023
29/08/2022

𝗙𝗔𝗛𝗔𝗠𝗨 π——π—›π—”π— π—•π—œ π—žπ—¨π— π—œ 𝗭𝗔 NDIMI ZETU (matamshi) PINDI TUNENAPO

TONE LA UPENDO β€οΈπŸ‘‡

Mpendwa! Kuna njia nyingi unaweza ukazitumia ili kupata utakatifu, lakini kubwa kuliko yote ni kuweza kuuzuia mdomo wako usinene mabaya. Maana Mtume Yakobo anasema hivi: Ulimi ni kitu kidogo sana kinachofanana na njiti moja ya kibiriti, ambacho ukikiwasha ndani ya msitu, inaweza kuunguza miti yote. (Yakobo 2:5)

Vivyo hivyo hata katika ndimi zetu, japo zinaonekana ni ndogo mno, lakini ukweli zinaweza kuleta madhara makubwa sana k**a tukizitumia vibaya tofauti na vile inavyohitajika.

Daima ulimi ndio kiungo pekee cha mwanadamu, ambacho kimepewa uwezo na Mwenyezi Mungu wa kubeba laana na baraka tele maishani mwetu. Na ndio maana hata Yesu mwenyewe anatutahadharisha, tuwe makini nacho. Kwani baada ya maisha ya hapa duniani kupita, kila mmoja atatoa hesabu ya maneno yake mbele ya kiti cha hukumu. (Mathayo 12:36)

Mfano wa maswali utakayoulizwa kutokana na namna ulivyotumia ulimi wako ni haya: Je ulimi wako umeutumia kumsifu Mungu na kulitangaza Neno lake, au kutwa nzima ni kupiga stori za mipira na kuwasifu wengine? Je ulimi wako ulikuwa baraka ya kuwaombea wengine, au kuwalaani kila siku pale wanapokuudhi? Je ulimi wako ulikuwa taa ya kuwaongoza wengine kwenye njia ya mafanikio yao, au yalikuwa sumu ya kuwakatisha tamaa pale walipoomba ushauri wako? N.k

Hakika ukiyatafakari haya kwa kina, ndipo utagundua kuwa, kinachomchafua mtu na kumtia unajisi, sio chakula anachokula wala kitu chochote kichafu anachokigusa, bali ni maneno ya mtu mwenyewe yanayotoka kinywani mwake. (Mathayo 15:10-11, 17-20)

𝗦π—ͺπ—”π—Ÿπ—œ: π——π—›π—”π— π—•π—œ π—§π—œπ—¦π—” 𝗭𝗔 π—¨π—Ÿπ—œπ— π—œ 𝗦𝗔𝗦𝗔 π—‘π—œ π—­π—œπ—£π—œ 𝗛𝗔𝗣𝗒?

π—π—œπ—•π—¨: πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

1. π—žπ—¨π—¦π—˜π— π—” π—¨π—’π—‘π—šπ—’

Uongo ni mojawapo ya vitu ambavyo hata Mungu mwenyewe anavichukia sana, kwa sababu ukichunguza vizuri utagundua, asili yake haikutoka kwa Mungu bali kwa shetani aliye baba wa uongo (Mithali 16:17) Na adhabu yake ni kubwa sana ya kutupwa motoni, kwa wale wote wanaosema uongo (Ufunuo 21:8).

2. π— π—”π—π—œπ—©π—¨π—‘π—’

Kiburi ni dhambi kubwa iliyomfanya shetani afukuzwe pale Paradisini, mara nyingi watu wenye kiburi hujiona wao ni bora kuliko wengine, hawataki kushaurika wala kufundishika. Hakika mtu wa namna hiyo, ni chukizo mbele za Mungu. (Zaburi 12:3-4)

3. π—Ÿπ—”π—”π—‘π—”

Laana ni maneno mabaya sana yanayoleta mikosi kwa yule anayetaamkiwa, maana mwanadamu alipewa uwezo huo na Mungu kupitia kinywa chake, lakini Mungu bado anaonya vikali kwa wale ambao wanawalaani wenzao. Haijalishi mtu amekukasirisha vipi, ila Biblia inatuambia tusiwe wepesi wa kulaani, bali tushukuru na tuondoke mahali pale kwa amani, kwani kazi ya kulaani sio yako, bali ni ya Mungu mwenyewe hata k**a uwezo huo uko ndani mwako. (Warumi 12:17-18)

4. π—¨π— π—•π—˜π—”

Dhambi hii ya umbea kwenye Biblia, imekatazwa katika vitabu vya (Zaburi 15:3 na Mithali 8:8). Maana watu wanaozungumza umbea mara nyingi, maneno yao huwa sumu kwa wale wanaowasikiliza, na wakati mwingine huweza kuleta malumbano na chuki kubwa ndani ya jamii, kwa sababu maneno yao umbea, mara zote huwa hayana ukweli zaidi ya kujaa uchonganishi tu, ili wengine wapigane. Mtu mmbea, haifai kuwepo katika jamii.

5. π— π—”π—§π—¨π—¦π—œ

Inashangaza sana kwa mtu ambaye anaonekane anampenda Mungu na kushika dini, lakini bado anazungumza matusi kinywani mwake. Ukweli matusi ni dhambi kubwa, maana anayetukana huwa hathaminiwi katika jamii, na muda mwingine matusi yake yanaweza kuleta vita na migogoro kwa yule anayetukanwa hasa ambaye hana moyo wa ustahimilivu. Kwahiyo matusi hayafai hata kidogo, kwa kuwa yanahatarisha maadili ya watoto, hivyo ni vema kuepukana nayo. (Wakolasai 3:8)

6. π—¨π—‘π—”π—™π—žπ—œ

Unafki kamwe haijawahi kumuacha mtu salama, maana utakuta mtu anakuambia mazuri yako yote pale anapokuwa nawe, lakini ukimpa kisogo, anakung'ong'a na kukusambazia maneno mabaya mbele za watu. Hivi unafikiri yule unayemsengenya akipata habari zako itakuwaje, k**a sio mwanzo wa kuvunjiana heshima na kununiana bila sababu za msingi? Hivyo tujihadhari na unafki, wala haipendezi kwa Mkristo kuwa msengenyaji, maana adhabu yake ni ya mauti. (Mithali 25:23 na Warumi 1:30)

7. π——π—›π—œπ—›π—”π—žπ—”

Siku zote hata uwe tajiri mkubwa vipi, lakini tambua kuna kitu kimoja tu ambacho utakikosa ila unaweza kukipata kwa maskini unayemdharau. Hivyo kuwadhihaki wengine kwa maneno ya kejeli sio jambo jema na ni chukizo mbele za Mungu. Maana sote tumeumbwa ili tupendane na kusaidiana, kwahiyo unapomdharau mwengine kwa sababu yeye ni fukara, hana elimu au umbo zuri k**a lako, jua unamdharau hata Mungu aliyemuumba kwa sura na mfano wake. (Yakobo 3:9)

8. π—žπ—”π—₯π—œπ—£π—œπ—”

Ukaripiaji ni ishara ya kuongea na mwenzako kwa sauti ya juu, k**a alama ya kumuonya, kumkemea au kumdhihaki mbele ya wengine. Lakini kumkaripia mtu kwa lengo la kumuonya sio vibaya, ila ubaya unakuja unamkaripia mtu kwa mazingira yapi? Maana ni vema umuite mtu peke yake na kumuelezea makosa aliyoyafanya mkiwa wawili, na sio kumchamba mbele za watu ili umuaibishe. Kwani unapofanya hivyo, unamuongezea hali ya kutokujiamini kwa mtu huyo, na muda mwingine kukuchukia kabisa kwa kitendo cha udhalilishaji ulichomfanyia. (2Timotheo 4:2)

9. π—žπ—¨π—π—œπ—£π—˜π—‘π——π—˜π—žπ—˜π—­π—”

Daima Mungu anachukia kiherehere, hasa pale mtu anapoamua kujipendekeza mwenyewe kwa watu kupitia matendo na maneno yake mazuri ili asifiwe (Luka 14:8) au utakuta mtu anamsifia mwenzake, ili apate kitu kutoka kwake. Hiyo nayo ni chukizo mbele za Mungu. Maana ni vema kuwa mnyenyekevu, na hayo yote yatakujia, kwa sababu anayejikweza hushushwa ila aliye mnyenyekevu hupandishwa kiwango cha juu zaidi. (Luka 1:52)

10. π—žπ—¨π—’π—‘π—šπ—˜π—” 𝗦𝗔𝗑𝗔

Siku zote mtu anayeongea sana, basi maneno yake mengi huwa ni ya uongo, kejeli na majivuno au matusi wakati mwingine, jambo ambalo Biblia inatutahadharisha tuwe makini nacho (Muhubiri 5:2 na Mithali 10:9) Na ndio maana hata Yesu mwenyewe anatuasa kuwa, maneno yetu mara zote yawe machache, yaani ndiyo au hapana, mengine zaidi ya hayo hutoka kwa shetani. (Mathayo 5:37)

Kwaahiyo ndugu zangu, tujihadhari sana ulimi, kwani ndiyo kitu pekee tulichotegwa nacho, na siku ya mwisho ndicho tutakachohukumiwa nacho. (Mithali 6:2)

Kwa Maombezi ya Mtakatifu Anthony wa Padua, Mungu atufanye tuwe watu wa kuzungumza maneno mema k**a alivyofanya Mtakatifu huyu, ambaye baada ya kifo chake, ulimi wake haukuweza kuoza pale kaburini, k**a ishara ya kutuonyesha kuwa, mtu huyu nyakati zote aliongea maneno matakatifu ya kumpendeza Mungu na watu wote waliomzunguka.

Credit: Mpendwa Theofilo
π—§π—¨π— π—¦π—œπ—™π—¨ π—¬π—˜π—¦π—¨ π—žπ—₯π—œπ—¦π—§π—’...

NAKUTAKIA DOMINIKA NJEMA NA SIKUKUU NJEMA KWA HESHIMA YA MTAKATIFU AUGUSTINOπŸ™πŸ™

15/07/2022

Address

Siaya

Telephone

+254758169161

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Augus nyakwar mother. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share