13/10/2022
MAKALA YA LEO
Uko kundi gani kati ya haya mawili?
A. Watu Walio Busy (Wana Mambo Mengi Bila Mwelekeo)
1. Huwa wanakimbizana na mambo mengi kila siku...
..ila siku ikiisha hawafanyanyi tathmini ya walichofanikiwa katika siku hiyo.
2. Huwa wanataka wahusike kwenye kila kitu kunachoendelea, mtandaoni, ofisini n.k...
Hawa huwa hawataki kupitwa na chochote.
3. Wanapenda kujisifia kuwa hawana muda kabisa...
..ila sababu kubwa ni kwamba wanataka kuonekana kila kitu wanajua.
4. Siku yao haina mpangilio, huwa wanaendesha siku kutegemea kinachowajia mbele yao.
Hawana vipaumbele kabisa.
5. Wanataka kujionesha kuwa wamefanikiwa sana lakini ukichunguza kwa undani wanaigiza.
B. Watu Wanaoishi Kwa Ufanisi.
1. Siku yao inaongozwa na vipaumbele muhimu...
..hawakubali kuendeshwa na matukio.
Kila siku wana vitu maalumu wanavyolenga kuvikamisha.
2. Wanaamini kuwa hawana muda wa kufanya kila kitu.
Wana ujasiri wa kusema hapana kwa mambo ambayo wanaona sio ya muhimu kwao.
3. Focus yao ipo kwenye malengo yao.
Hawaishi ili kushindana wala kujionesha kwa wengine.
NIA yao kubwa ni kutimiza malengo yao.
4. Kila siku huwa wanajiuliza...
..Hivi leo nitafanya nini kitakachonisogeza karibu zaidi na malengo niliyonayo?
Hawakubali siku ipite bila hata kufanya kitu kidogo kinachochangia kwenye mafanikio yao.
Wewe uko kundi gani?
Kuna jambo linakutatiza?
Jiunge
https://t.me/Esotech_biashara
kujipatia kitabu (SOFTCOPY) Kinachohusu namna ya kutatua jambo hilo.
K**a unahitaji kuwa mtu mwenye mafanikio, nilazima ukubali kubadili mtazamo, kubali kjifunza kila siku na kubali kubadilika katika kila kitu... Siri ya mafanikio ni Ufahamu