11/05/2026
JE, UNAJUA UMUHIMU WA KUYAONGEZEA THAMANI MADINI YA VITO KABLA YA KUYAUZA ?
Madini ya Vito ni miongoni mwa Madini yenye thamani kubwa maradufu zaidi pindi baada ya kuongezewa thamani, kitu ambacho ni rahisi kukuza uchumi wa mfanya biashara husika pale endapo ataujua umuhimu wa kuyaongezea thamani Madini ya Vito kabla ya kuyaingiza sokoni.
MFANO HAI KWENYE MADINI YA VITO AINA YA RED SPINAL.
Kwa kuanza ni vyema tukafahamu zaidi kuhusu mpangilio wa vipimo vya uzito kwenye Madini ya Vito ambapo Gram 1 ni sawa na Carats 5, na Carat 1 ni sawa na Gam 0.2.
Sasa katika majukumu yangu ya kikazi nilikutana na Mteja mwenye Gram 0.52 za Madini ya Vito aina ya Red Spinal na kuniomba ushauri baada ya kumpatia huduma ya valuation ambapo swali lake lilikuwa ni hili; "NIFANYAJE ILI KUJIONGEZEA FAIDA KUPITIA JIWE HILI", na Mimi k**a mtaalamu wa Jimolojia (Gemologist) nilimshauri akaliongezee thamani jiwe hilo ili kuongezea kiwango cha thamani yake na mfanya biashara huyo alikubali kisha kwenda kuliongezea thamani jiwe lake.
Baada ya mchakato wa uongezeaji thamani kukamilika ilipatikana sample yenye uzito wa Carats 3.19 ambayo ni sawa na Gram 0.313 na majibu ya tathimini ya thamani yake yalikuwa ni k**a ifuatavyo:
KABLA YA KUONGEZEWA THAMANI (BEFORE FACETED).
• Aina (Species): Red Spinal.
• Daraja (Grade): A
• Grams: 0.313
• Thamani (Price): 81,511.67284 Tsh ($31.3 USD)
BAADA YA KUONGEZEWA THAMANI (AFTER FACETED).
• Aina (Species): Red Spinal.
• Daraja (Grade): A
• Carats: 3.19
• Thamani (Price): 23,294,004.816368 Tsh ($8,944.76 USD)
UHIYANO (DIMENSIONS).
• Urefu (Height): 10 Millimeters
• Upana (Width): 8 Millimeters
• Kina (Depth): 5 Millimeters
HITIMISHO.
Biashara ya Madini ya Vito ni miongoni mwa biashara zenye faida zaidi pale endapo itafanyika kwa kufuata Sheria na kanuni zote za kitaalamu bila kutegemea ufanyaji wa biashara kwa kutumia mazoea au blaa blaa za vijiweni. Asante
Unaweza kunitafuta k**a utahitaji huduma za kitaalamu ikiwemo kutathiminisha thamani za Madini ya Vito ili kujua bei yake, na gharama zangu ni nafuu mno ya shillingi Elfu 15 tu ambapo popote pale ulipo huduma inakufikia kikubwa unitumie video yenye kuonyesha vyema upande wa ndani na nje mwa jiwe lake kisha kusubiri report ya majibu yako baada ya masaa mawili ya kazi kutimia.
Piga Number zifuatazo kwa maelezo zaidi:
+255688882893
+255627438433
AU
WhatApp:
https://wa.me/255694444391
Na k**a huhitaji kufanyiwa valuation na mtaalamu wa jimolojia unaweza kutumia software ya T-TanzaniteGram itakayo kusaidia kufanya valuation kwa gharama nafuu zaidi kwa mwaka mzima.