Auction & Minada & Viwanja& Nyumba

Auction & Minada & Viwanja& Nyumba 🔨 Licensed Auctioneers & Property Agents
🏠 Auctions | Real Estate
📍 Tanzania
📲 WhatsApp for enquiries

26/01/2026
02/10/2021

Kusanya hela kwa maarifa yaani muonekano wa kadi yenyewe tu umeshapata hela. Kadi za mialiko, vikao, semina au shughuli za makampuni taasisi n.k tuone kwa maelfu hadi kadi 100K unapata😊😊😊

14/08/2021

Badala ya 300,000 k**ata Logo k**a hii kwa 70,000 usilipe hata 100 k**a hautapenda kazi tutakayokufanyia. Ofa inaisha tarehe 16/08/2021 J3. WhatsApp: 0686 129 032. Pia Tembelea www.zatra.co kuona kazi zetu na huduma zitakazokuoambanua sokoni. Wahi sasa

14/08/2021
16/03/2021

Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo. Mit 22:29 SUV

13/03/2021

MOYO WA UBUNIFU
Kisa cha Msomi mwenye degree ya banking anayeuza nyanya na apples mtaani, Benin Afrika ya Magharibi.

Baada ya kuhitimu masomo yake ya elimu ya juu katika fani ya banking msomi huyu akakaa nyumbani bila ajira k**a wengi wetu tulivyo. Mara likamjia wazo, "kwanini nisifungue biashara nikaipa hadhi k**a vile ambavyo nimeajiriwa bank?"

Baada ya kutafakari akachukua hatua, akatengeneza kitolori kisha akaweka nyanya na apples, akavalia suti iliyonyooshwa vizuri nadhifu na maridadi, kapiga na tai akaanza kuzunguka mitaani anasambaza nyanya na apples. Watu wengi walipoona usafi ule na unadhifu wakavutiwa sana kununua, kwa ufupi akateka hisia za watu. Wakati wao wanashangaa mtu wa viwango vile kuuza nyanya na apples yeye anatengeneza hela.

Kufanya hadithi iwe fupi, akahojiwa na shirika la habari la BBC: Kwanini umeamua kuuza nyanya kwenye tolori na huku umevalia suti na tai? Akawajibu k**a ifuatavyo: "Nimemaliza chuo kikuu katika fani ya banking na sikupata kazi inayohusiana na bank, hivyo nimeamua kutumia hadhi na muonekano ule ule ambao ningekuwa nao bank katika biashara hii"

Unadhani shida ni mtaji au ubunifu unaoweza kukupa matokeo chanya? Pamoja na bidii ambayo mtu anaweza kuwa nayo endapo utakosa ubunifu utafanya kazi nyingi za kuchosha ambazo hazina manufaa kidogo

Watu awaangamii kwa kukosa maombi, kufunga au kutoa sadaka; bali kwa kukosa maarifa. Wakati wote Mungu hajawahi kuwa na tatizo kanuni zinabaki pale pale. Unaamua mwenyewe uchukue hatua ufanikiwe au uendelee kukaa nyumbani mpaka muujiza utokee.

Unaweza ukapitia www.zanobay.com kuna huduma unaweza ukazipenda karibu

Pia unaweza kumsaidia mtu mmoja ukawa baraka kwake kwa Like | Share | Comment zitakazofanya iwafikie na wengine

NB: Picha haina uhusiano na muhusika wa kisa hiki, imewekwa kuakisi habari yenyewe

Imeandaliwa na Joseph Magwega Marwa kwa msaada wa mtandao

12/03/2021

NIUZE NYANYA?
Ni miongoni mwa maswali wanayojiuliza watu wengi wakitaka kuonyesha wazi kwamba wanachoangalia siyo fursa zilizopo kwenye nyanya bali udhaifu na dharau utakazozipata kwa kuuza nyanya hizo.

Hebu twende taratibu. Chukulia mfano maembe, yana hatua za ukuuaji hadi kufikia mahali pa kutumika. Utaona wakati sahihi wa kuliwa ni pale yanapokomaa. Kuna usemi maarufu unaosema "Fursa ni k**a maembe, wakati unasubiri yaive wengine wanayala kwa chumvi" kadhalika na kila wazo la kuzalisha faida.

Mara nyingi siyo chache, watu wengi wangependa kupata kazi mahali ambapo kuna kila kitu; yaani kwa ufupi ukute viti vya kuzunguka, meza nzuri za heshima na viyoyozi. Mazingira k**a hayo yenye ushawishi kwa jamii utaona ni rahisi mtu kufurahia kazi ya namna hiyo yenye hadhi ambayo ataweza kupiga picha na kuwavutia wanaomfahamu na jamii kwa ujumla.

Jambo moja dhahiri ni kwamba uzuri wa kazi au biashara haupimwi kwa uzuri wa jengo la ofisi au samani (furniture). Linapokuja swala la kutengeneza biashara yenye manufaa basi bidhaa yoyote inaweza kufaa kulingana na uhitaji na faida inayoacha.

Ndiyo, siyo suala la nyanya tu, hata k**a ni manyoya ya kuku, samadi (vinyesi vya wanyama), mchanga, kokoto, nyasi hata k**a ni pumba. Kinacho angaliwa siyo uzuri wa bidhaa bali uwezo wa bidhaa hiyo kuhitajika sana sokoni.

Wakati wewe unashangaa juu ya nyanya kuna watu wao wanauza mkojo wa sungura na wanazalisha mpaka 200,000 kwa dumu la lita 20. Mkojo huu hutumika k**a mbolea maalum mashambani

Mambo ya muhimu ya kuzingatia ni kwamba:
1. Mfumo wa biashara (business system) ndiyo kitu pekee kitakacho kutofautisha na mkulima kule shambani. Bill Gate kwa mfano hakuanzisha Microsoft bali alinunua wazo kutoka kwa kikundi cha watu mtaani akajenga biashara na kuanza kuliuza wazo hilo. Miongoni mwa wateja waliomletea matokeo makubwa alikuwa IBM na yaliyofuata mpaka leo ni historia. Angalia namna bora ya usambazaji, jinsi ya kuwafikia wateja wengi na jinsi ya kutengeneza mfumo utakaowahudumia watu wengi zaidi (Hii ndiyo sehemu muhimu zaidi kuliko hata bidhaa au huduma unayotoa)

2. Anza taratibu (Humble beginning). Epuka kuanza kwa nguvu kubwa na kuokoa gharama za uendeshaji. Biashara nyingi kubwa hazikuanzia maghorofani bali kwenye karakana majumbani au nje ya miji. Fuatilia historia ya Google, Apple, Disney na Alibaba

3. Lenga kutatua changamoto zaidi na siyo kupata faida za haraka haraka. K**a unataka faida za haraka haraka siyo wazo sahihi maana inaweza ikakuchukua miaka mpaka kupata uelekeo sahahi. Hivyo unahitaji uvumilivu, na nguvu ya kuendelea kutoa huduma mfululizo bila kuacha ( | | | )

4. Badala ya kuona aibu kuwa utaonekanaje, ona aibu juu ya ugali na vitu vya bure unavyotumia hapo nyumbani. Ndiyo, pengine umri unaenda na wewe unasubiri kazi safi ambayo kila mtu atakusifu. Siyo wakati huu

5. Maarifa katika zama hizi yamejaa kila mahali na unaweza ukayapata bure au kwa gharama ndogo kabisa. Pia unaweza kujifunza moja kwa moja kwa watu wenye wazo sawa na la kwako. "Na k**a elimu ni ghari basi jaribu ujinga"

Ndiyo unaweza kuuza siyo nyanya tu bali huduma na bidhaa yoyote na ukafanikiwa. Unahitaji wazo sahihi, mahali sahihi na muda sahihi. Siyo kila wazo ni fursa mahali ulipo. Tafuta wapi linahitajika fanya majaribio kisha wekeza.

Kila la heri
Unaweza kutembelea www.zanobay.com
Ukipenda Like | share | Comment. Asante

Imeandaliwa na: Joseph Magweiga Marwa

11/03/2021

Bahari iliyotulia haitengenezi baharia mwenye ujuzi. Magumu na mawimbi ya maisha katika kila eneo la maisha yana lengo moja kuu "KUKUIMARISHA" ili ufike unapostahili kufika. Kuna maisha unapitia mpaka yanakukatisha tamaa? Unatengenezwa usiogope! Like, share, comment iwafikie na wengine , , , , ,

10/03/2021

Mambo yote ni magumu kabla hayajaanza kuwa mepesi. Inachukua kati ya siku 18 hadi 254 unachokifanyia mazoezi kuwa tabia au sehemu ya maisha yako. Kadili kinavyokuwa kigumu zaidi na ndivyo idadi ya siku huongezeka zaidi. According to a 2009 study published in the European Journal of Social Psychology, it takes 18 to 254 days for a person to form a new habit. Visit www.zanobay.com

Address

Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00
Saturday 08:00 - 17:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Auction & Minada & Viwanja& Nyumba posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category