Elias M Tryphone

Elias M Tryphone Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Elias M Tryphone, Business consultant, Dar es Salaam.

Scene:- 2022 | Shot:- Eagle Eye | Lens: Grateful (To God, You and Me)
31/12/2022

Scene:- 2022 | Shot:- Eagle Eye | Lens: Grateful (To God, You and Me)

To all blessings and lessons🥂, Happy Birthday to you, Elias!
29/10/2022

To all blessings and lessons🥂, Happy Birthday to you, Elias!

NZI AU NYUKI 🐝Niaje  Najua haya sio mazungumzo tuliyokuwa tunazungumza hapa, lakini si haba nikashare na hili.—————————-...
05/10/2022

NZI AU NYUKI 🐝

Niaje

Najua haya sio mazungumzo tuliyokuwa tunazungumza hapa, lakini si haba nikashare na hili.

—————————-

Nzi na Nyuki, kila mmoja anachukiwa na mwanadamu, na sababu kubwa ni wanadamu wanawaogopa.

Nzi hang’ati, lakini analeta maradhi. Yupo yupo tu anazunguka, anatua hapa mara anaenda pale (hachagui penye taka au pasipo taka)… asijue anabeba hatari na kuipeleka kusiko hatari… na ndio maana mwanadamu akimfikiri Nzi; UOGA wa maradhi unaamsha CHUKI.

Kwa upande mwingine Nyuki,… Nyuki ni anauma… nafikiri karibu kila mtu (sio wa kishua ofcourse), ashaionja ya nyuki. Nyuki anapenda vitu vitamu/vizuri (maua) na kwenye hili hayumbishwi; nyuki mchavushaji. Licha ya UOGA na CHUKI aliyonayo mwanadamu kwa Nyuki; BILA nyuki; mimea anayoichavusha isingekuwepo na wanayama wanayoila mimea hio pia wasingukuwa na maisha.

Kuna wanadamu Nzi, na kunawanadamu Nyuki. Nzi wanasemwa sana 😂 (Pale mzee, mi siendi kuna kuna Nzi wengi)… Nyuki hawasemwi semwi lakini wanachukiwa sana (utashangaa ndani ndani wanaheshimiwa kinoma).

Nzi au Nyuki, sio bahati mbaya; au destiny… ni maamuzi… na unaweza kuhamia upande wowote unaotaka.

Najua hamuwezi kuwatag Nzi haba 😂😂😂, basi muwatag Nyuki 🐝


MTOTO Au UTOTOUnajua wewe ni mkubwa kabisa, acha kujifanya mtoto (wakati mwingine wakimaanisha ‘acha utoto’)? Lakini je ...
23/08/2022

MTOTO Au UTOTO

Unajua wewe ni mkubwa kabisa, acha kujifanya mtoto (wakati mwingine wakimaanisha ‘acha utoto’)? Lakini je ni kweli mtoto na utoto ni vitu sawa? Na ni sawa kuwa kimoja wapo?

Nilipokuwa mdogo mdogo nilikuwa nachezaga football bhana…. Na mara kadhaa niliota kuwa mchezaji pro k**a kina Edgar Davis (aliyekuwa anacheza mpira na miwani)… mara kadhaa nilifunga goli pekee/la ushindi… mara kadhaa niliitwa kwenye kikosi cha Shule ya Msingi Nyamalango B…. ilikuwa tamu sana… hata mara kadhaa niliporudi nyumbani nimechelewa, mama Mwalimu akaniwasha njiti, bado siku iliyofuata nilirudi uwanjani. Mpaka pale nilipoanza kuwa mkubwa na kuwa busy zaidi na madaftari.

Kadri tunavyokua; tunajifunza au tunafundishwa kuwa wakubwa (kwa maana nyingine kuukataa/kuuchukia utoto…); japo hio haimaanishi kuzikataa furaha, fahari na ndoto tulizoota tukiwa watoto. Vitu hivyo ndio vilivyotupa msukumo wa kuwa sisi leo, na kwa sehemu kubwa vinaendelea kuwa na maana kubwa na kuwa sehemu kubwa ya furaha kwenye maisha yetu.

K**a wengi wasemavyo, furaha sio gharama; gharama ni kuendelea kumkumbuka mtoto aliyeko ndani yako, na vitu alivyovipenda na kuvifurahia. Hio ndio namna bora ya kujipenda wenyewe na kuwapenda tuwapendao!

Ilikuwa wakati mzuri kucheza mpira tena…. K**a ilivyo kwa wengine kukumbatiwa, kula ice cream, kulishwa, kusafiri, kuchora, kuimba na kucheza….. listi ni ndefu kidogo 😂… Wewe unanijua vyema zaidi

Unaweza kuendelea kumlea mtoto ndani yako bila kuukumbatia utoto!


Aisee imekuwa muda hatujaongea (no, I admit, imekuwa muda sijachukua muda kukuandikia)….Uko? Mambo yanaenda?Salamu hii i...
27/07/2022

Aisee imekuwa muda hatujaongea (no, I admit, imekuwa muda sijachukua muda kukuandikia)….

Uko? Mambo yanaenda?

Salamu hii inanikumbusha my old legal consultant friend ; kila aliponisalimia kujua naendeleaje na startup yangu, alipenda kuniuliza “Mambo yanaenda?”… “Mambo yanaendeshwa” nilipenda namjibu.

Mambo yanaenda?

Kila mtu ana kauelekeo na viKPIs vyake anakokapigania; na deep down ni tamanio la kila mtu kuona mambo yanaenda…. Lakini mambo yanaenda endaje? Au yanaenda endeshwaje?

Unapoamka na kauluvivu ka kila kitu, lakini ukajisukuma na kukamilisha ya siku hiyo.. mambo yameenda, umeyaendesha! Ukimkosea mteja, baada ya muda mrefu wa kufikiri (ambao hautatui chochote ‘inter’, labda ‘intra’) kisha ukaamua kumuomba msamaha na nafasi ya kufuta makosa, ukadeliver extra; mambo yameenda, umeyaendesha! Ukiwa na wazo, ukaamua kulifanyia kazi na kulikuza kuwa bishara/platform/opportubnity (anyways kuna milioni ya ideas zinafia vichwani kwa watu); mambo yameenda, umeyaendesha! And the stories goes on!

Mambo yanaenda yakiendeshwa, mambo yanaendesha ukisubiri yaende! Somewhat jitahidi kubaki kuwa on control! Unaweza kujipa muda wa kupumzika, lakini rudi, yaendesha, jifunze kuwayaongoza twende mbele!

Tunasherehekea zawadi ya maisha yako....Mbegu ilipandwa, kupanda mbegu zaidi!  Cc
01/05/2022

Tunasherehekea zawadi ya maisha yako....Mbegu ilipandwa, kupanda mbegu zaidi!

Cc

Hata sasa, Mungu ni mwema! Happy birthday to me!
29/10/2021

Hata sasa, Mungu ni mwema! Happy birthday to me!

WAZO AU UWEZOSikuwa kichwani kwake yule muuza Ice cream za ukwaju pale Morroco, lakini naamini hili ndo lilikuwa WAZO ki...
12/10/2021

WAZO AU UWEZO

Sikuwa kichwani kwake yule muuza Ice cream za ukwaju pale Morroco, lakini naamini hili ndo lilikuwa WAZO kichwani kwake "Hii pesa siwezi kuiachia, hata k**a taa za barabarani zimeruhusu. Nitamuwahi huyu mteja chap na kuipata hii pesa kwa ajili ya kibubu changu!!" Na alipopiga hatua ya kwaza, pili, tatu, nne kutoka kwenye hifadhi ya barabara... Akajikuta amegongwa na kitu kizito, akaanguka chini. Yote haya yalitokea ndani ya sekunde thelathini or so.

Akajaribu kuinuka, mkono wala mguu haukuwa unatembea. Kutoka mtu aliyekuwa anaikimbilia riziki iliyoliongoza na kukitawala WAZO lake, UWEZO ulimuondoka. Akabebwa na kwenye hifadhi ya barabara alikotomea na mteja huyoo kwenye gari yake akaondoka. Mimi nikijiona mwenye ahueni kidogo, japo niliweza kuinuka, sikuweza kukanyaga chini.

Nilipofika hospital niliambiwa nmevunjika mguu kwenye mfupa wa unyayo. Nikafungwa muhogo (POP Cast) kwa mwezi na sasa nmeanza mazoezi. Sijui hali ya mwenzangu l aliyegongwa, angalau dereva aliyekuwa kanibeba kwenye boda boda yeye hakuumia sana (andiko la Dereva Au Abiria ntalisimulia siku nyingine...)

WAZO linahatiji UWEZO. Unaruhusiwa kuwaza kuuzidi UWEZO lakini si kuwaza kiasi cha kuhatarisha kuupoteza UWEZO.

Tuendelee kuchukua tahadhali na kuwa salama katika mihangaiko yetu.

26/05/2021

MAX


MAGUFULI ANGEFANYA NINI?Juzi Jumatano usiku, Mama  alipotutangazia taifa kuhusu msiba wa Raisi wetu mpendwa  wa Awamu ya...
19/03/2021

MAGUFULI ANGEFANYA NINI?

Juzi Jumatano usiku, Mama alipotutangazia taifa kuhusu msiba wa Raisi wetu mpendwa wa Awamu ya Tano, Mh. Dr. John Joseph Pombe Magufuli….. ni k**a taifa tulipatwa na chafya, na tulikuwa tunajilazimisha kuipiga bila kufumba macho (inawezekanaje kupiga chafya bila kufumba macho?).

Hatimaye chafya tuliipiga, macho tukafumba, kwa muda kukatanda giza totoro lakini, tumefumbua macho tena. Leo saa 4 asubuhi, tutampata Raisi mwingine, Raisi wa kwanza Mwanamke, atakeyeliongoza taifa hili kwa miaka minne, ya ndoto ya miaka mitano ya awamu ya tano. Tuendeleaje mbele?

Raisi Magufuli, kwa kadri ya uwezo wake kibinadamu na k**a kiongozi alionesha nia ya dhati ya kuipeleka Tanzania kwenye uchumi bora, kutatua matatizo yetu na kugusa maisha ya kila Tanzania (hata yule mwenye uwezo wa chini). Hapo ndipo nafikiri tunapoirudia filosofia ya …. Sio kwa utani wa twitter, bali userious wa kitaifa ili ituongoze kwenye Tanzania bora zaidi, kwa njia/mifumo bora zaidi na zenye mafanikio zaidi.

Hongera Mama, Raisi wetu Mpya. Sisi ndo Tanzania, Sisi ndo Future.

28/02/2021

NGOMA YA RUGE MUTAHABA

Siku moja tulikuwa tunaandika makala na nakumbuka kabisa mstari wa kwanza “Maisha ni k**a utunzi wa Ngoma ya ndoto zetu”.... hatua zako ndio tempo ya ngoma yako, mishe mishe zako ndo snares, hit hat na percussions... na mawazo na plan zako ndo arrangement ya ngoma yako (part ipi ni chorus ijirudie, ipi ni loop na verse zako ni zipi).

Note rahisi, Uandishi wa K**awaida, chords zisizo na muafaka na Hisia butu hazijawahi kutengeza muziki na waimbaji wakubwa na mahiri.

Ngoma yako uliiandika kwa uhodari mkubwa, hisia nzito na uandishi ya kipekee uliokufanya uwe RUGE wa pekee.

Kwa pamoja, tunaamka kuzikusanya karatasi ulizitumia kutunga ngoma yako na kuanza kuiimba kwa harmony uliyoipendA na kuiarrange k**a ulivyotamani iwe. So help us God!

Address

Dar Es Salaam
11000

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Elias M Tryphone posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Elias M Tryphone:

Share