16/06/2026
1. MAANA YA PID
PID (Pelvic Inflammatory Disease) ni maambukizi makali ya bakteria yanayotokea katika mfumo wa uzazi wa mwanamke. Maambukizi haya yanahusisha maeneo ya shingo ya uzazi (cervix), mfuko wa uzazi (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes), na mayai ya uzazi (ovaries).
2. CHANZO CHA PID
Chanzo kikuu cha PID ni bakteria wabaya wanaopanda kutoka ukeni kwenda juu kwenye mfumo wa uzazi.
Bakteria wa Magonjwa ya Zinaa (STIs): Hasa bakteria wa Kisonono (Gonorrhea) na Kaswende au Kifungatiba (Chlamydia).
Bakteria wa Kawaida wa Ukeni: Mabadiliko ya mazingira ya uke (k**a matumizi ya sabuni kali au douching) yanayosababisha bakteria wa kawaida kupanda juu.
Sababu Zingine: Maambukizi baada ya kujifungua, kutoa mimba, au wakati wa kuwekewa vifaa vya kuzuia mimba (k**a lupu/IUD) katika mazingira yasiyo safi.
3. DALILI ZA PID
Wanawake wengi wanaweza kuwa na PID bila kujua kwa sababu dalili zinaweza kuwa hafifu, lakini dalili kuu ni pamoja na:
Maumivu chini ya kitovu (kwenye nyonga) yanayoweza kuwa makali au ya muda mrefu.
Uchafu wa uke unaotoa harufu mbaya na wenye rangi ya njano au kijani.
Maumivu makali wakati wa kukutana kimwili na mwenza.
Kuhisi maumivu au kuungua wakati wa kukojoa.
Kutokwa na damu nje ya siku za hedhi au baada ya tendo la ndoa.
Homa, kichefuchefu, na mwili kuchoka.
4. MADHARA YA PID (Yasipotibiwa)
PID isipotibiwa mapema au isipotibiwa vizuri, inaweza kusababisha madhara makubwa ya kudumu:
Ugumba (Infertility): Bakteria wanapoharibu au kuziba mirija ya uzazi (Fallopian Tubes), yai linashindwa kupita, jambo linalomfanya mwanamke ashindwe kushika mimba.
Mimba Nje ya Mfuko wa Uzazi (Ectopic Pregnancy): Mirija ikilemaa kutokana na makovu ya PID, mimba inaweza kutungwa na kuanza kukulia kwenye mrija, jambo ambalo ni hatari kwa maisha ya mama.
Maumivu Sugu ya Nyonga (Chronic Pelvic Pain): Maumivu yanayodumu kwa miezi au miaka kutokana na makovu kwenye viungo vya uzazi.
Kutokea kwa Majipu (Abscess): Kukusanyika kwa usaha kwenye mfumo wa uzazi.
5. TIBA NA USHAURI
PID inatibika kabisa ikigundulika mapema kwa kutumia mchanganyiko sahihi wa dawa za kuua bakteria (Antibiotics) na virutubisho maalum vya kuongeza kinga ya mwili na kusafisha mfumo wa uzazi. Ni muhimu pia mwenza (mwanaume) na yeye apate tiba ili kuzuia maambukizi kujirudia.
Kwa tiba na ushauei piga ☎️📞+255756403981