21/10/2025
Shaloom Mwana Mwa Mungu.
Nakusalimu kwa jina la Yesu Kristo Bwana wetu alie hai.
Ni wakati wako Mtu wa Mungu wetu Jehova wa mbinguni kusimama na Mungu wetu iki kuikomboa nchi yetu ya Tanzania na Kanisa Lake.
Omba k**a vile haukuwahi kuomba ukimwomba Roho mtakatifu akusaidie namna ya kuiombea nchi yetu ya Tanzania.
Wakati Waisraeli walipoandikiwa walaka wa kuuawa, Ester hakutilia maanani kwa kuwa alijiona yuko salama kwani alikuwa ndani ya himaya ya mfalme akaona jambo hili halimhusu(Soma Esta1 hadi Ester 10) . Nawe pia waweza kudhani kuwa uko salama na jambo hili halikuhusu kumbe hauko salama pia.
Siku ya kutoweka kwa amani yanchi na kukionja kikombe cha mateso cha haitachagua.
Mateso yakianza hautapata Muda wa Kuomba, hautapata muda wa kukesha. Nyumba na kitanda chako utavisahau, biashara yako na shamba lako vitabaki kuwa histori.
Tafakari ni kiti kipi cha enzi ninachoitawala nchi kisha chukua hatua ya Maombi ili Mungu akatawale kiti cha Enzi cha Nchi yetu.
Chukua hatua ya Kuiombea Tanzania na Utawala wa Tanzania uwe chini ya Mungu wetu Muumba mbingu na nchi kambla wakati haujapita Mungu asitupite.
Osiombe kutimiza matakwa ya Moyo wako. Omba kwa Msaada wa Uongozi wa Roho mtakatifu katika jina la Yesu.
Ukiweza kufunga na Kuomba Funga kwa kadri utakavyoongozwa na Roho bila hila wala Uadui na Mtu.
Sambaza ujumbe huu ukamfikie kila mtanzania ili k**a itampendeza Mtanzania huyo Kuombe nchi, Na aiombee nchi yetu yaliyo Mema kwani Tanzania ni Yetu sote na ikiharibika itatuharibikia sote kwani wengi wetu hatuna uwezo wa kukimbia. Ikiwa ni Mabaya yatatukuta humu humu na ikiwa ni maziri yatatukuta humu humu na tegemeo la Wokovu wetu ni Mungu wetu wa Mbinguni.
Mungu atubariki Watanzania na kuilinda amani yetu na Furaha yeu katika Jina la Yesu
Amina.
Ewe Mtanzania Simama na Msitari huu katika Maombi.
2 Mambo ya Nyakati 7:14
[14]ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
If my people, which are called by my name, shall humble themselves, and pray, and seek my face, and turn from their wicked ways; then will I hear from heaven, and will forgive their sin, and will heal their land