17/10/2025
Miongoni mwa matukio ya kushangaza sana ni tukio hili la bahari mbili maji yake kukutana lakini hayachanganyikani.Hili tukio kwa mara ya kwanza lilielezwa vizuri na mwenyezi Mungu katika Quran zaizi ya miaka 1,000 iliyopita.
Ukisoma katika quran tukufu,
Surah _Al-Fur'qan Ayah Ile ya 53, mwenyezi Mungu mwenyewe anasema :
وَهُوَ ٱلَّذِي مَرَجَ ٱلۡبَحۡرَيۡنِ هَٰذَا عَذۡبٞ فُرَاتٞ وَهَٰذَا مِلۡحٌ أُجَاجٞ وَجَعَلَ بَيۡنَهُمَا بَرۡزَخٗا وَحِجۡرٗا مَّحۡجُورٗا
"Naye ndiye aliye zipeleka bahari mbili, hii tamu mno, na hii ya chumvi chungu. Na akaweka baina yao kinga na kizuizi kizuiacho"
MFANO WA HIZO BAHARI KWA SASA NI HIZI ZIFUATAZO :
1️⃣Bahari ya Mediterranean (Bahari ya Kati) na Atlantiki. Bahari hizi hukutana kwenye Mlango-Bahari wa Gibraltar (kati ya Uhispania na Morocco).
2️⃣Wengi pia wanataja eneo la Gulf of Alaska, ambako maji baridi ya glacial hukutana na maji ya bahari lakini hayaungani haraka.
3️⃣Pia hutajwa kukutana kwa maji ya Bahari ya Shamu (Red Sea) na Bahari ya Hindi kupitia Bab al-Mandab.
Sayansi ya sasa inasema kuwa tukio hili husababishwa na tofauti kubwa ya msongamano (density) ya maji ambapo bahari moja ina chumvi nyingi kuliko nyingine.sababu nyingine ni joto tofauti kati ya bahari mbili na sababu ya mwisho ni mtiririko wa nguvu wa mikondo ya bahari yaani Ocean currents.
Qur'an ilisema Kwanza miaka zaidi ya elfu moja iliyopita harafu wanasayansi wakaja kufahamu baadaye karne ya 20 ambapo ni kuanzia miaka ya 1990's kwa kutumia satelite na submarine imaging kuwa maeneo haya yana tabaka za maji zinazoigawanya bahari, na unapopita katikati yake unaona mstari halisi k**a ukuta laini.
Sina ufahamu mwingi kuhusiana na Biblia kwahiyo wakristo mnaweza mkanukuu vifungu tuone na nyie wapi hili tukio limetajwa waziwazi k**a katika quran.Hii ipo kwa lengo la kujifunza na wala sio marumbano ya dini.
Mwisho naweza kusema,
Allahu Ya'lam(mwenyezi Mungu ndie mjuzi zaidi)
NIWATAKIE SIKU NJEMA