20/05/2026
KUNA BUNDI DHIDI YA UPEPO NA TAARIFA ZISIZOTHIBITISHWA KUHUSU AFYA YA 'Tundu Lissu';
Askofu wa Chadema Tanzania, Tarehe 18 May 2026 saa 07:30hrs akiwa Itunge Dar Es Salaam kwenye account ya Facebook Emmaus Bandekile Mwamakula, Alichapisha taarifa yenye kichwa 'ASKOFU ATOA KAULI JUU YA AFYA YA LISSU!').
Nipo tofauti na Askofu, kwani Katika nyakati ambazo jamii inahitaji utulivu, busara na ukweli, baadhi ya watu k**a Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula, John Heche nk! wameendelea kutumia majukwaa yao kueneza simulizi za hofu, taharuki na mashaka bila ushahidi wa moja kwa moja na kufanya sisi jamii tujielekeze kwenye Maswali. Kauli ya Emmaus Bandekile Mwamakula kuhusu afya ya Tundu Lissu imeibua maswali mengi kuliko majibu.
Swali kubwa ambalo jamii inapaswa kujiuliza ni hili:
Ni kwa nini taarifa nyeti k**a hizi zitolewe kwa hisia kali, tuhuma nzito na lugha ya kuashiria njama kabla ya kuthibitishwa rasmi na madaktari au mamlaka husika?
Kwa mujibu wa simulizi hiyo, John Heche anadai mbele ya jukwaa kupigiwa simu na ndugu wa Lissu aitwaye Vicent Lissu kuhusu maumivu ya tumbo 'Hakutaja alipiwa tarehe ngapi! mwezi gani! Mwaka gani! Saa ngapi?. Lakini ghafla, bila ripoti ya kitabibu, bila uchunguzi wa daktari, bila ushahidi wa maabara simulizi linaanza kugeuzwa kuwa “Sumu”, “Njama”, na mazingira ya kisiasa. (Hawa wanataka kuaminisha nini na kwa maslahi gani?.
Hapa ndipo jamii inapaswa kuwa makini.
Maumivu ya tumbo si ushahidi wa sumu. Binadamu anaweza kuumwa kwa sababu nyingi za kawaida kabisa. Lakini unapochukua taarifa ambayo haijathibitishwa kisha ukaijenga kwa lugha ya hofu, machozi, taharuki na lawama za kisiasa, unakuwa hutafuti ukweli tena unatengeneza huruma ya kuchochea hisia kwa jamii.
Kinachoshangaza zaidi ni namna kauli hiyo ilivyojaa, lawama za mapema na hukumu kabla ya uthibitisho. Mdomo huponza kichwa; Hii ndiyo mbinu inayotumika mara nyingi kwenye propaganda za kisiasa; kuanzisha hisia kwanza, ushahidi baadaye. 'Kwanza watu waogope' Kwanza jamii ichukie. 'Kwanza wananchi waamini kuna “mkono wa siri”. Halafu baadaye ukweli uje ukiwa umechelewa.
Hata hivyo jamii tunao ushahidi wa Post za askofu huyuhuyu 'Kushadadia asiyo yajua' aliyoongea baada ya tukio la mwanafunzi wa IFM Kukatwa kichwa! lakini baada ya watuhumiwa kuk**atwa aibu anajisikia yeye mbele ya jamii. Mzee 'mdomo huponza kichwa' wapo watu wanayakusema lakini kwa busara zao hunyamaza! kwakuwa wewe umeumbwa kusema sema mambo yenye mantiki,udhibitisho wakimamlaka.
Watanzania wanapaswa kuelewa kuwa taasisi k**a Jeshi la Magereza Tanzania zina wajibu wa kisheria wa kuhakikisha usalama wa mahabusu na wafungwa. Tuhuma nzito k**a “kupewa sumu” haziwezi kutolewa kwa hisia, kwa presha za kisiasa au kwa maneno ya kusisimua mitandao bila ushahidi wa kitaalamu. Emmaus Bandekile Mwamakula