18/06/2026
Watu wengi huona model akitembea kwa kujiamini kwenye runway, lakini hawazioni saa za mazoezi, marekebisho na kujifunza zinazowekwa nyuma ya mafanikio hayo.
Huyu ni mmoja wa wanafunzi wetu wa Muda Kids Club akiwa siku yake ya pili tu ya mafunzo ya catwalk. Ingawa safari ndiyo inaanza, tayari anaonyesha jambo muhimu sana ambalo haliwezi kufundishwa kirahisi, ujasiri wa kusimama mbele ya watu na kuthubutu kujifunza.
Kila hatua anayopiga leo ni uwekezaji wa kesho yake. Kila maelekezo anayopokea yanamjenga kuwa na nidhamu, kujiamini, kujitambua na kuwa na uwezo wa kujieleza kupitia mwendo wake. Haya ndiyo mambo yanayowatofautisha wale wanaoota mafanikio na wale wanaochukua hatua kuelekea kuyafikia.
Tunajivunia kuona watoto wakikua katika mazingira yanayowapa nafasi ya kugundua vipaji vyao, kujenga tabia bora na kuamini kuwa wanaweza kufikia ndoto zao bila kujali umri wao.
Hongera kwa mwanafuni wetu Buya kwa jitihada na moyo wa kujifunza. Hongera pia kwa wazazi wanaoendelea kuwaunga mkono watoto wao katika safari hii ya ukuaji na maendeleo. Kila dakika wanayoitumia kujifunza leo ni sehemu ya msingi imara wa mafanikio yao ya baadaye.
Safari bado ni ndefu, lakini mwanzo mzuri ni dalili ya mwisho mzuri. Tunaamini kuwa kwa mazoezi, nidhamu na kujituma, hakuna kinachoshindikana.
Train up a child in the way he should go, and when he is old he will not depart from it.
Karibu ushuhudie safari ya ukuaji wa nyota wa kesho, hatua moja baada ya nyingine.