16/03/2026
CONTENT CREATOR:
Duh, saa 1:30 asubuhi! Alooo dah, nimechelewa kuamka kabisa leo. Wakati nahangaika kukurupuka kuamka, mara simu inaita...
"Naam, hallow!! Dah, niko njiani, dakika 10 nitakuwa hapo."
Nanawa uso chapu, nachukua nguo navaa huku naangalia k**a baiskeli yangu ina upepo. Duh, chapu nafunga mlango, nakimbizana na muda kuwahi kazini.
Haya ndio maisha yangu mara nyingi kila asubuhi, na hali hii ya kuchelewa kazini huwa inanikumba sana hata nikiwa nimeweka alama (alarm) ya kuniamsha. Hii yote inatokana na kuchelewa kulala. Mimi mbali na kazi yangu hii, pia ni content creator. Hivyo, mara nyingi huwa nalala saa sita usiku hadi saa saba, na natakiwa kuamka saa 12 asubuhi. Ilishakuwa k**a maisha yangu japo huwa napambana sana kuhakikisha nabadilika.
Mimi jina langu naitwa Erick, na haya ndio maisha yangu ya kila siku; yaani nashinda juani nasambaza maji kwa kutumia baiskeli kwa wateja, na pia nasambaza vyakula. Japo nikipata upenyo, lazima niingie TikTok kuangalia kunaendeleaje, maana nina matumaini sana kuwa ipo siku moja content yangu moja itabadili shilingi moja yangu kuwa bilioni moja, japo sijui ni lini.
Kwenye kazi hii ya kusambaza maji na vyakula nina k**a miaka miwili sasa kuelekea wa tatu, ila kuhusu mambo ya u-content creator nina k**a mwaka na miezi mitatu au minne. Kazi yangu ni ngumu sana kwani ina hekaheka nyingi sana. Kuna muda wateja wanakuudhi hadi unatamani uache kazi yenyewe, ila ukikumbuka ndio kazi mama, mmmhhh unapiga moyo konde unakuwa k**a hujakereka.
Haya ndio maisha yangu ya muda wote; kuzunguka na baiskeli yangu kwa wateja, kuunda content tofauti tofauti, na kushare live za wadau TikTok. Kuhusu kuweka akiba, dah, nilishafeli kabisa na huwa ni k**a naishi kwa imani tu, maana mara nyingi nikipata hela huwa nanunua vitu vya kutengeneza contents tu mitandaoni. Kazi zangu zote huwa nazipost sana TikTok kuliko mitandao mingine. Hivyo kuhusu akiba, dah, labda laki moja au 80,000 ndio unaweza kukuta ninayo ndani. Hekaheka zangu ni nyingi sana kiasi kwamba hata mahusiano yanayumbayumba sana. Wanawake wananikataa sana; k**a unavyojua wao ukishakuwa baby tu, aaaahhh unakuwa M-PESA kwao! Sasa duh, wananikataa sana.
Sema hawawezi kukukataa wote. Hivyo kuna pisi yangu moja hivi, kwao sio mambo mbaya sana, wako vizuri tu. Sijui ndio maana vizinga hainipigi sana. Ile ndio msasa wangu na inanikubali sana. Kuhusu wivu na upendo, dah, ile pisi inanijali sana na ishapigana sana na mademu wangu, na kuna sehemu zingine ilikuwa ni k**a inaniokoa. Maana duh, si unajua sisi vijana, yaani mambo magumu mfukoni ila kuomba namba za mademu mmhhhh, ni k**a kawa. Sema ndio hivyo, sasa hivi nimetulia nayo sana ile pisi bwana, inaitwa Sara.
Siku moja nilikuwa nahitaji kutengeneza video kwa kutumia AI. Sasa kumbe kifurushi nilicholipia kimeisha. Dah, nikanyoosha waya kwa Sara nikamkopa bwana; mtoto akatuma na ya kutolea! Nikamuahidi wiki mbili namrudishia mzigo wake. Nikatengeneza content yangu safi, nikatupia TikTok k**a tatu hivi. Ila nilikuwa bored sana, hivyo nikavuta waya tena kwa Sara nikamwambia, "Sielewi, kichupa kiko full!" Aaahhh mtoto kazungukaaa, ila mwisho akaja kwa Mkapa... tukakiwasha sana!
Yaani nakuja kukurupuka ni saa 1 na nusu tena! Duh, hivyo nikamuacha mtoto anajiandaa kwenda kwao, mimi nikadandia baiskeli yangu hadi job. Nikipata nafasi nachungulia tena TikTok wanasemaje.
Basi jioni nikarudi zangu home. Mmhh, nashangaa mlango wazi wakati Sara nilimwambia akitoka afunge. Sasa wakati natahamaki, mara nashikwa mkono nyuma.
"Mmhh vipi tena, kumbe hukwenda?" nilimuuliza Sara kwa mshangao mno.
Mtoto akacheka tu kisha akasema, "Baba kaniambia nirudi nilikolala jana. Maana wewe nilikwambia mzee hajalala ukalazimisha tu, sasa ndio matokeo haya. Kasema nikitaka kwenda niende na niliyelala naye akaseme kwanini nililala kwake."
Unajua niliganda k**a sekunde hivi hahahaaaa, hadi akanibumburusha na kibao begani! Ndio kukurupuka sasa nikasema mbona msala tena. Ila nikajisemea moyoni, "Aaaahhh, ngoja tuone mwisho wa hii movie nayo." Basi bwana, nikawa mume wa mtu bila ndoa wala mshenga! Sema mtoto alikuwa ananipenda sana hivyo ni k**a nilipata real assistance sasa.
Maisha yakaenda hivyo k**a miezi minne huku nikiwa naendelea na kazi zangu k**a kawaida. Mtoto kutokana na mazingira yao, yeye alikuwa ndani na season na single movie tu. Japo nilikuwa na-enjoy sana maana nilisahau kufua na kupika kabisa, na ugonjwa wa kuosha vyombo sasa hahahaa nilipona kabisa.
Sasa siku moja nikiwa zangu nazurura TikTok, kuna meseji mpya zikaingia k**a nne kwa wakati mmoja kutoka kwa watu tofauti. Si unajua k**a kawaida unajua hawa ni wana tu wanagawa hii. Sasa nikajibu tu k**a kawaida, ila mmoja k**a akawa serious na chatting, hivyo nikawa naye inbox. Akasema kapenda sana kazi zangu hivyo anataka tuonane kwa ajili ya mazungumzo. Mmhh nikasema hili mbona zali! Ila dah, nisipaniki. Nikamwambia, "Sawa, ila naomba tuonane tarehe 17," na siku hiyo ilikuwa tarehe 12. Jamaa akasema fresh, akachukua namba zangu pale profile yangu na akanipigia k**a sekunde 42 kunitambulisha kisha akakata.
Basi kwa kuwa sasa hivi nilikuwa na wa kuniamsha, nilikuwa sichelewi sana. Nikaingia zangu mzigoni k**a kawaida. Ila siku k**a ya nne hivi nikamshirikisha Sara hili jambo la kuhusu jamaa aliyetaka tuonane. Sara akaangalia chatting mara akawa mkali, "Yaani mtu anakuomba muonane we unajiwekea siku nyingi hivyo? Kweli badala upambanie labda inaweza kuwa ndio bahati yenyewe!"
Nikamwangalia Sara na nikamwambia (kwa upole), "My wangu, hata k**a una maisha ya chini au ya kati hutakiwi kabisa kuwa available sana kwa watu. Hata k**a una shida kweli watakuchukulia wa kawaida, kwamba kila wakikuita ni chapu tu k**a cha kwanza unatokea."
Hahahaaa, Sara alicheka sana kisha akasema, "Haya bwana mwanafalsafa, sawa wewe nenda kamsikilize jamani maana huwezi jua."
Basi tarehe 16 nikamcheki jamaa nikamwambia kesho nakuja k**a tulivyoongea. Jamaa kasema sawa, akanipa maelekezo na mengine kusema atanielekeza nikiwa njiani. K**a unavyojua usiku wa deni haukawii, basi kukacha; na si unajua nina mke! Hivyo nikaandaa nguo za kwenda kuonana na mtu ambaye wote hatumjui. Na siku hiyo bwana nilioga maji ya vuguvugu bwana (hahahaaa mapenzi bwana). Nikashika zangu barabara nikawa nampigia jamaa hadi nikafika aliponielekeza.
Mmmhhh nilishtuka! Mbona k**a kampuni hii, na ni kampuni kubwa sana? Ila nikapiga moyo konde maana jamaa alinitumia kikadi hivi WhatsApp akasema nikifika tu mapokezi niwaonyeshe hicho kikadi wao wanajua cha kufanya. Nikafika bwana mapokezi... duuh!!! Si nikakutanisha macho na pisi moja kali hivi! Mmmhh ikabidi tu nimeze mate bwana. Nikasalimia na kumuonyesha ile karatasi. Nilishangaa baada ya kumuona k**a kashtuka kidogo, ila nikawa k**a sijamwangalia na akanielekeza kwa upole sana mahali ambapo kadi ilielekeza.
Nikawa najiuliza, mmhh mbona k**a silielewi hili movie, nisije nikawa naenda kuchinjwa (hahabaaa mawazo ya kifukara bwana, matatizo tu). Sasa nikawa nimepanda kwenye lifti. Shida ikaanzia kwenye lifti sasa, maana sijawahi hata kubonyeza kitufe chochote! Ila Mungu sio Athuman, akaja mtu akaniongoza hadi mahali kadi inaelekeza. Sasa nashangaa mlango ninaoelekezwa kuingia ni mlango umewekwa kibango cha CEO. Nikasema mmmhh, au hili neno lina maana zaidi ya ninayoijua???
MWISHO WA PAONE ONE
K**a umeipenda story like comments na share kwa wengine na nambie k**a unahitaji mwendelezo