30/08/2015
NYAKAME EDUCATION AND RESEARCH CENTER (NERC)
MAFUNZO KWA MAFUNDI NA WAKURUGENZI WA MAKAMPUNI KWA AJILI YA KUBORESHA UBORA WA KAZI ((QUALITY MANAGEMENT SYSTEM) (QMS))
Ubora wa kazi ndiyo mtaji kwa mafundi kwa ajili ya kujipatia wateja wa kutosha na kushikilia wateja utakao wapata katika soko, katika kingireza tunaita Quality Management System (QMS).
Misingi hii ya ubora wa kazi ndio njia sahihi ya kupata wateja katika soko, haijalishi unafanya kazi ndogo kiasi gani jambo la kwanza unalo takiwa kuwanalo katika ufahamu wako ni ubora wa kazi unayoenda kuifanya, kwa kujiuliza ni kwakiasi gani utamulizisha mteja wako katika kazi unayoifanya bila kujali pesa aliyokulipa ili mradi umeshakubali kuifanya.
Hii ndiyo njia wanayoitumia wenzetu mafundi waliobobea katika ufundi kwa maana kuwa mteja mmoja nyuma yake kuna wateja kumi.
Unapofanya kazi nilazima ujue misingi ya ufundi kwamba ninapofanya kazi hii anayefata baada yangu ni nani na yeye atafanyaje kazi yake pale nilipoishia mimi. Mawazo haya katika kingereza tunaita Total Quality Management (TQM).
Huu ni mfumo wa kufanya kazi kwa kuwaza nani anayefata kuendelea na kazi baada yangu . Hivyo kila mmoja anafanya kazi kwa kuzingatia ubora kwa kumulahisishia mwenzake atakayefata, na hapo ndipo umakini unapopatikani katika kazi.
Mfano k**a fundi anayejenga ukuta wa matofali atanyosha vizuri ukuta wake , fundi plasta naye atafanya kazi kwa urahisi huku akimsifia fundi aliyejenga ukuta ambayo itasababisha fundi aliyejenga ukuta kupata soko zaidi.
Vilevile k**a fundi plasta naye atapiga plasta yake vizuri kwa kunyosha vizuri atapo kuja fundi rangi atamsifia fundi plasta ambaye naye pia ataendelea kupata wateja kwa sifa za fundi rangi.
Mwisho kabisa atakapo kuja fundi rangi naye atapaka rangi yake vizuri na itakuwa na muonekano mzuri , ambayo italeta furaha kwa mteja hata watazamaje wakisema huyu fundi amepaka rangi vizuri. Naye hii itamusababishia aendelea kuwa na wateja wengi.
Mfumo huu ndio tunaita ujumla wa ubora wa kazi. Ambao ndiyo filosofi ya soko huria ya jinsi ya kupata wateja katika misingi ya ushindani.
Hivyo fundi kuwa makini unapo fanya kazi yako. Huu ni mfano mmoja tu katika kazi ya ukuta kati ya fundi kujenga ukuta, fundi plasta na fundi wa kupaka rangi.
Tunayo mambo mengi sana kuhusu kozi hii ambayo itabadilisha kabisa mtazamo wako na kukuwezesha kuwa na wateja wengi katika kazi yako , kozi hii itaanza hivi karibuni kwa mafundi, wakandalasi na watu wote waliojiajili bila kujali elimu zao katika kituo chetu cha NYAKAME EDUCATION AND RESEARCH CENTER (NERC).
Ukihitaji kozi hii tafadhali wasiliana nasi:
0713 56 58 74
0689 56 58 74
Tunapatikana Mwanjelwa, Kabwe , MBEYA.