22/06/2026
π NENO LA JIONI β UCHUMI NA KANISA ACADEMY TANZANIA
"Kila mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, k**a kwa Bwana wala si kwa wanadamu."β Wakolosai 3:23 (BHN)
Jioni hii jitathmini: Je, umefanya kazi zako kwa uaminifu, ubora na kumtukuza Mungu? Uchumi imara haujengwi kwa maombi pekee, bali pia kwa kazi yenye bidii, uadilifu na usimamizi mzuri wa rasilimali ambazo Mungu ametukabidhi. Biblia inafundisha kwamba kazi ni sehemu ya mpango wa Mungu kwa mwanadamu na tunapaswa kuitenda kwa moyo wote.
Maombi:
Baba wa mbinguni, asante kwa kunipa nguvu za kufanya kazi leo. Nisamehe pale nilipokosea, unipe hekima ya kusimamia vizuri rasilimali ulizonipa, na unibariki ili niwe baraka kwa wengine. Katika jina la Yesu, Amina.
π± UCHUMI NA KANISA ACADEMY TANZANIA*
"Maarifa yanajenga uchumi, na hekima hudumisha mafanikio."