Soko la Mchikichini

Soko la Mchikichini Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Soko la Mchikichini, Business service, Dodoma.

26/05/2022
TEUZI MBALI MBALI ZA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA MACHINGA NGAZI ZA TAIFA NA MKOA ZIMEENDELEA KUFANYIKAMwenyekiti wa Shirik...
19/05/2022

TEUZI MBALI MBALI ZA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA MACHINGA NGAZI ZA TAIFA NA MKOA ZIMEENDELEA KUFANYIKA

Mwenyekiti wa Shirikisho la Machinga Tanzania (Shiuma)
Bw: Ernest Matondo Masanja

Amezungumzia juu ya Changamoto ya baadhi wa viongozi wa Mikoa kutokuwa na ushirikiano mzuri ka viongozi wa Machinga Taifa.

Mwenyekiti wa Shiuma Taifa amefanya mabadiliko ya Uongozi wote wa Mkoa wa Dar Es Salaam kuanzia nafasi ya Mwenyekiti, Katibu, mweka hazina Pamoja na Nafasi Ya makamu mwenyekiti wa Shiuma Taifa.

UTEUZI MPYA WA DAR ES SALAAM - KUTOKA KWENYE KILA WILAYA
—————————————————
💡Mshauri wa Mkoa - Geofrey Millonge

💡Mweka Hazina Mkoa - Mohamed Asumani Ally

💡Naibu katibu Mkoa - Kelvin Josephat

💡Katibu mkoa - Marcelina misingo

💡Mwenyekiti Mkoa - Christopher Kisiga

💡Makamu mwenyekiti Mkoa - John Packsence Mbagwile

💡Afisa Habari Mkoa - Ismail Sal Feisal

Dodoma mambo yanaenda kuwa mazuri
18/05/2022

Dodoma mambo yanaenda kuwa mazuri

MAFUNZO KWA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA UMOJA WA MACHINGA TANZANIA (SHIUMA)Ikiwa Leo ni Siku ya Pili tangu kuanza kwa Semi...
17/05/2022

MAFUNZO KWA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA UMOJA WA MACHINGA TANZANIA (SHIUMA)

Ikiwa Leo ni Siku ya Pili tangu kuanza kwa Semina ya Uongozi wa Machinga Tanzania.

Wamachinga wafurahia Wimbo wa Hamasa juu ya Anuwani ya Makazi.

Mafunzo yanaendelea na sasa Wamachinga wanapata Elimu kuhusu Anuani ya Makazi.

NI FURSA SAHIHI YA KUKUZA UCHUMI WA NCHI YETU.

Imetolewa na Afisa Habari wa Soko la Mchikichini- Ismail Sal Feisal.

Follow us on Instagram
Soko_la_Mchikichini




Wawakilishi wa wafanya Biashara wadogo wadogo wa Wilaya Ilala (Machinga) ambao ni Viongozi wa Machinga Wilaya ya Ilala (...
15/05/2022

Wawakilishi wa wafanya Biashara wadogo wadogo wa Wilaya Ilala (Machinga) ambao ni Viongozi wa Machinga Wilaya ya Ilala (Shiuma)

Wakiwa kwenye picha ya Pamoja wakati wa Safari ya kuelekea Dodoma kwaajili ya Semina ya Uongozi kuanzia ngazi ya masoko,Wilaya na Mkoa.

Semina hiyo inataraji kuanza siku ya Jumatatu May 16. 2022 Hadi May 19 .2022.

Wawakilishi wa wafanya biashara Wilaya ya ILALA ambao ni viongozi wa wafanya Biashara wadogo wadogo (Shiuma) Leo wametem...
14/05/2022

Wawakilishi wa wafanya biashara Wilaya ya ILALA ambao ni viongozi wa wafanya Biashara wadogo wadogo (Shiuma)

Leo wametembelea Soko la Mchikichini wakiongozwa na Katibu wa Wilaya ya ilala Bi: Catherine Bundala.

ikiwa ni muendelezo wa Mazungumzo ya kuona namna gani ya kusaidia wafanya Biashara na Changamoto Zao.

Imetolewa na Afisa Habari wa Soko la Mchikichini: Ismail Sal Feisal.

By: Afisa Habari wa Soko
Ismail Sal Feisal

Follow us on Instagram
Soko_la_Mchikichini




Mapema Leo 12 May 2022 Viongozi wa Shiuma Wilaya ya Ilala, wamekutana kwaajili ya Kujadili mambo ya kimaendeleo. Viongoz...
12/05/2022

Mapema Leo 12 May 2022 Viongozi wa Shiuma Wilaya ya Ilala, wamekutana kwaajili ya Kujadili mambo ya kimaendeleo.

Viongozi wa Shiuma wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wilaya ya ILALA
Bw: Christopher Kidiga wamekutana kwaajili ya kutazama changamoto za wafanya Biashara wadogo wadogo katika Wilaya ya Ilala na kuona namna gani wanaweza kutatua Changamoto hizo ikiwa ni Pamoja na kutembelea Masoko yote ya Wilaya na kukusanya maoni kutoka kwa Viongozi na wafanya Biashara.

By:Afisa Habari wa Soko la Mchikichini.

💪🏻Nguvu moja 💥

MCHIKICHINI YAPATA MIKOPO. Wafanya Biashara wa Soko la Mchikichini, ILALA, Dar Es Salaam, wapata mikopo yenye Riba na Ma...
10/05/2022

MCHIKICHINI YAPATA MIKOPO.

Wafanya Biashara wa Soko la Mchikichini, ILALA, Dar Es Salaam, wapata mikopo yenye Riba na Masharti nafuu kutoka MAENDELEO BANK, kwaajili ya kujiendeleza Kibiashara.

Hatua Hii imefanikiwa baada ya Uwongozi wa Machinga Mkoa wa Dar wakiongozwa na Mwenyekiti Bw: Yusuph Namoto Walipokutana na Uongozi wa Soko la Mchikichini Na kufanya majadiliano na Mwenyekiti wa Soko Bw: Geofrey Millonge,
Nakukubaliana kuwasaidia wafanya Biashara kwa kuwawezesha kupata Mikopo kutoka Maendeleo Bank.

Hatua Hii imechukuliwa kwa Lengo la kusaidia wafanya Biashara baada ya wengi kupoteza mitaji Yao wakati Soko lilipoteketa kwa Moto Tarehe 16/01/2022.

Aidha Uongozi wa Soko la Mchikichini wana Shukuru sana Maendeleo Bank kwa kujitolea kuwasaidia wafanya Biashara wote.

By: Afisa Habari wa Soko
Ismail Sal Feisal

Follow us on Instagram
Soko_la_Mchikichini






Mkurugenzi wa Idara ya Sera, Mipango na Uratibu wa Machinga SHIUMA (T) Tanzania, Leo Alipata wasaa wa kutembelea Ofisi z...
28/04/2022

Mkurugenzi wa Idara ya Sera, Mipango na Uratibu wa Machinga SHIUMA (T) Tanzania, Leo Alipata wasaa wa kutembelea Ofisi za Soko la mchikichini na kukutana na Uongozi wa Soko kwaajili ya kujadili mambo ya kimaendeleo na kubadilisha na wazo juu ya utendaji.

Aidha Mwenyekiti wa Soko la Mchikichini Bw: Geofrey Millonge amesisitiza viongozo wa Masoko nchini kujenga utamaduni wa kutembeleana ili kusaidia kuimarisha Umoja wa Machinga.

By: Afisa Habari na Mahusiano wa Soko
Ismail Sal Feisal

Follow us on Instagram
Soko_la_Mchikichini




Uongozi wa DCC Business Park “Machinga Complex”, Ilala, Dar Es Salaam. Leo wamepata nafasi ya kutembelea Ofisi za Uongoz...
23/04/2022

Uongozi wa DCC Business Park “Machinga Complex”, Ilala, Dar Es Salaam.
Leo wamepata nafasi ya kutembelea Ofisi za Uongozi wa Soko la Mchikichini.

Lengo ni kualika Uongozi wa Mchikichini na Wafanya Biashara wote kwenye Wiki ya Maonyesho ya Biashara ya Soko la Machinga Complex.

Itakayofanyika kuanzia Tarehe 25-30 Mwezi wa 4 Mwaka 2022.

Ikiwa ni Ishara nzuri ya kutengeneza ushirikiano wa Masoko na kuunganisha Wamachinga wote nchini.

Uongozi wa Soko la Mchikichini Umefurahia kupata mualiko huu wa Kipekee.

By: Afisa Habari wa Soko
Ismail Sal Feisal

Follow us on Instagram
Soko_la_Mchikichini




NMB wakutana na baadhi ya Viongozi wa Wafanya Biashara ndogo ndogo (Wamachinga) kwaajili ya Kujadili namna gani wanaweza...
22/04/2022

NMB wakutana na baadhi ya Viongozi wa Wafanya Biashara ndogo ndogo (Wamachinga) kwaajili ya Kujadili namna gani wanaweza kusaidia kundi la Wafanya Biashara ikiwa ni Pamoja na kuanzisha Account mpya kwaajili ya Machinga.

Bank ya Nmb Imeamua kutengeneza Account maalum kwaajili ya Machinga.

Masharti ya Account
—————————————————-
Kianzio cha Account - 10,000/=
Kitambulisho cha nida

Baada ya kufungua Account ya Machinga inaweza kukuingiza moja kwa moja kwenye Fulsa Ya kupata Mkopo.

By: Afisa Habari na Mahusiano wa Soko
Ismail Sal Feisal

Follow us on Instagram
Soko_la_Mchikichini




Uongozi wa Soko la Mchikichini wakiongozwa na Bw:Geofrey Millonge mapema Leo wametembelea Ofisi za Almashauri ya Manispa...
22/04/2022

Uongozi wa Soko la Mchikichini wakiongozwa na Bw:Geofrey Millonge mapema Leo wametembelea Ofisi za Almashauri ya Manispaa ya Ilala na kukutana na Mkurugenzi wa Manispaa Bw: Jumanne K Shauri, Kwaajili ya Kujadili mipango na maendeleo ya Soko la Mchikichini.

Lengo kubwa ni kuona namna gani ya Kuboresha utendaji ndani ya Soko.
Pia Mkurugenzi wa Almashauri ya Ilala amepongeza jitihada zinazofanywa na Viongozi Hawa Wapya kwenye kuimarisha ulinzi wa Soko na Kuratibu miradi ya Maendeleo.

By: Afisa Habari na Mahusiano wa Soko
Ismail Sal Feisal

Follow us on Instagram
Soko_la_Mchikichini




Address

Dodoma

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Soko la Mchikichini posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share