Mwita AgroWealth

Mwita AgroWealth AgriEconomist ||Entrepreneur||Business news ||Writter ||Consultancy service.

Biashara ya viatu na faida zake.Mwanadamu anaweza kushinda bila kula vyakula vya gharama lakini hawezi kutembea peku bil...
23/07/2026

Biashara ya viatu na faida zake.

Mwanadamu anaweza kushinda bila kula vyakula vya gharama lakini hawezi kutembea peku bila viatu mtaani.

Leo hii, kila mtu anahitaji viatu kuanzia mtoto anayezaliwa leo hadi mtu mzima. Hii inaifsnya hii biashara ya viatu kuwa moja ya biashara isiyokufabmsimu mzima. Sio masika, wala kiangazi.

Unafuu wa biashara hii ni kwamba inaweza kukupa faida kuanzia 50% hadi 100% ya bei ya jumla, hasa ukijua machimbo ya kupata mzigo kwa bei nafuu na mzigo wenye ubora. Iwe ni viatu vya mpira, maofisini, kushindia soko lipo la kutosha kinachoshindika ni wewe tu hujaamua kuamka na kuanza kulifanyia.

Hebu waza ukiwa na duka lako sehemu uliko au mtandaoni kila siku unafunga na faida ya 20k kwa mwezi mzima utakuwa umetengeneza zaidi ya 600k kwa maeneo ambayo hayajachangamka, kwa eneo lililo vizuri kutengeneza zaidi ya 100k faida kwa siku ni kawaida.

Biashara hii inakupa nafasi ya kufanya na mambo yako, pia ni biashara inayokuwa kwa kasi sana ukizingatia nidhamu kwenye kazi yako. Nasema kutoakana na uzoefu wangu kwenye hii kazi kwa zaidi ya miaka miwili sasa.

Kumbuka sio lazima uanze na mamilioni, unaweza kuanza kwa kuchukua order chache mtandaoni na kuwazuia jamaa zako au watu unakaa nao. Unaongeza mzigo kadri mtaji unavyokuwa.

Je, unataka kujua ni wapi utapata viatu kwa bei ya jumla yenye punguzo kubwa?, Comment chini "VIATU " nikutumie muongozo mzima.

Biashara yoyote ile haikui kwa bahati bali kufanya mambo sahihi kwa mwendelezo na kwa uhakika1. MJUE MTEJA WAKO. Huyu nd...
22/07/2026

Biashara yoyote ile haikui kwa bahati bali kufanya mambo sahihi kwa mwendelezo na kwa uhakika
1. MJUE MTEJA WAKO.
Huyu ndiye msingi wa biashara, jiulize
✅️Anataka nini?
✅️Ana changamoto gani?
✅️kwa nini anunue kwako na sio kwa mtu mwingine.

2. TOA HUDUMA BORA
Fanya haya ili usimpoteze mteja wako;-
✅️Mkaribishe kwa heshima.
✅️Jibu maswali yake kwa wakati.(online and physical )
✅️Mfatilie baada ya mauzo.
✅️Timiza ahadi yako

3. KUWA HAI MITANDAONI
Dunia imehamia kwenye ulimwengu wa teknolojia, ukiendelea kubaki kuuza dukani tu unasubiri wateja utapata shida sana. Fanya haya.
✅️Pata elimu kuhusu huduma au bidhaa zako.
✅️Weka shuhuda za wateja kwa mtandao.
✅️Picha na video za bidhaa zako.
Usisubiri kuuza tu, chapisha mara kwa mara

4. ENDELEA KUJIFUNZA
Watu woote waliofanikiwa hawaachi kujifunza, kila kukicha wanasoma vitu vipya kwa ajili ya kuongeza maarifa ya kuendeleza biashara zao
✅️Soma vitabu vya biashara na mafanikio.
✅️Hudhuria mafunzo ya ujasiriamali, biashara na uwekezaji.
✅️Jifunze mbinu mpya za mauzo na masoko.
✅️Fatilia watu woote waliofanikiwa walifanya nini.
Kumbuka: Maarifa mazuri huleta maamuzi bora
Umejifunza nini kwa siku ya leo?. Tuachie ujumbe kwenye comment, usisahau kutofollow kwa tips k**a hizi kila siku
Facebook: Mwita AgroWealth
Instagram : .co

16/07/2026

Tengeneza faida kupitia dhahabu hii ya miguu minne
🐐 💰🌱 📈

Siri ya Muda na Mafanikio (Sehemu ya 1)​Je, unajua kuwa masikini na tajiri wote wana masaa 24 sawa kwa siku? Tofauti pek...
16/07/2026

Siri ya Muda na Mafanikio (Sehemu ya 1)

​Je, unajua kuwa masikini na tajiri wote wana masaa 24 sawa kwa siku? Tofauti pekee iliyopo ni jinsi kila mmoja anavyotumia masaa hayo. Wakati mwingine unajikuta unafanya kazi kwa bidii, lakini siku inaisha ukiwa huna ulichofanya cha maana.

​Muda sio tu namba zinazosonga mbele; muda ni mtaji wako mkuu wa siri. Kila sekunde unayoipoteza ni sawa na fursa ya kutengeneza kipato au kujifunza kitu kipya inayopotea jumla. Watu waliofanikiwa hawana muda mwingi kuliko wewe, ila wana nidhamu ya juu ya kuutawala muda wao.

​Fikiria maisha ambayo kila dakika ya siku yako inaleta matokeo chanya kwenye malengo yako. Maisha ambayo huna presha ya kuwahi mambo yaliyochelewa, bali una amani ya kufanya mambo sahihi kwa wakati sahihi. Huo ndio mwanzo wa mafanikio ya kweli.

​Acha kulalamika kuwa huna muda! Anza leo kupanga ratiba ya siku yako usiku wa kuamkia kesho, na uandike mambo makuu matatu tu unayotakiwa kuyakamilisha.

​ Gonga Like na comment "Muda ni Mtaji" k**a uko tayari kuutawala muda wako kuanzia leo!

Viatu vyako ndio kitu cha kwanza watu huangalia wakikutana na wewe.Muonekano wako wa mtoko sokoni, kwenye shughuli, mtaa...
15/07/2026

Viatu vyako ndio kitu cha kwanza watu huangalia wakikutana na wewe.

Muonekano wako wa mtoko sokoni, kwenye shughuli, mtaani unakamilishwa na kiatu ulichovaaa. Huu ni muonekano mpya wa kiatu chenye soli nene, laini kinakupa muonekano Safi kila unakopita

Sendo hizi zina soli ya jeli laini isiyoumiza kisigino, na upande wa juu una nakshi za kung'aa zinazofanya mguu wako uonekane wa gharama. Hautapata maumivu ya miguu hata ukitembea siku nzima, na utapendeza kwenye mtoko wowote ule. ✨

Unajipatia muonekano huu wa kijanja kwa Tsh 25,000 tu. Zipo saizi tofauti. Tuma picha hii kwenda WhatsApp yangu sasa hivi kupitia namba 0763 908 825 tukuletee popote ulipo! 📦🚚

K**a unaweza kuanzisha biashara ndogo,K**a unaweza kuongeza ujuzi mpya,K**a unaweza kuongeza kipato,K**a unaweza kuchuku...
12/07/2026

K**a unaweza kuanzisha biashara ndogo,
K**a unaweza kuongeza ujuzi mpya,
K**a unaweza kuongeza kipato,
K**a unaweza kuchukua hatari kuongeza kipato,

Tumia ujuzi na akili yako yoote kuanza hata na kidogo ulichonacho.
Biashara ndogo inazaa Biashara kubwa. Anza na kidgo ulichonacho kisha unasonga mbele.

Acha kabisa akili ya kusema sina mtaji, anza hata na 10k,50k,100k. Muhimu fanya biashara, hakikisha kila siku unaingiza hata 5k.

Biashara zoote zilianza kwa kidgo, mwisho wa siku zikapata Usimamizi mzuri na zikakua.
usiogope, maisha yako, yako mikononi mwako.

Ukianza kufanya jambo au mradi wako huo unaoufikiria kichwani,  mwanzoni utaona k**a mateso na hakuna matumaini kabisa m...
08/07/2026

Ukianza kufanya jambo au mradi wako huo unaoufikiria kichwani, mwanzoni utaona k**a mateso na hakuna matumaini kabisa mbeleni.

Kadri utakavyokuwa unajitesa na kusimamia mikakati yako kutimiza lengo la kufanikisha wazo/mradi wako, ndivyo utakavyokuwa unaona matumaini mbeleni.

Mwandishi mmoja na mfanyabiashara mkubwa wa china Jack ma,aliwahi kusema kuwa "Leo ni ngumu, kesho ni ngumu zaidi ila siku baada ya kesho ni nzuri sana, ila watu wengu hufa/hukata tamaa kesho jioni".

Wazo lako liweke kwenye maandishi, liwekee mikakati ni vitu gani unahitaji ili uweze kufanikisha je ni watu, fedha, eneo au bidhaa. Anza kukusanya kimoja kimoja bila kukata tamaa.

Kwenye kitabu cha Atomic Habit anasema kuwa vitu vidogovidogo ndivyo hujenga vikubwa anza na kidgo weka nidhamu kuwa kadri muda unavyoenda.

07/07/2026

"Kupata hela ni sawa na kuchimba kwenye udongo mgumu kwa vidole, wakati kupoteza pesa ni rahisi k**a kumwaga maji kwenye mchanga"

07/07/2026

Kilimo cha kisasa na kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu.
K**a nchi ili kuifikia ajenda ya 10/30 kwenye sekta ya kilimo tunapaswa kuwekeza kwenye sekta ya kilimo hasa kwenye teknolojia ya umwagiliaji. Huu ni mfano wa shamba la kampuni moja huko Israel. Wizara ya Kilimo

Address

Kahama

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mwita AgroWealth posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share