Gotgo times habari motomoto

Gotgo times habari motomoto the page is all about providing news to public , eventually raise awareness among community

Canada hawaamin
01/12/2022

Canada hawaamin

Muda wa 7:00 PMMbungi linapigwa. Mjini.
21/11/2022

Muda wa 7:00 PM
Mbungi linapigwa. Mjini.

Tuzungumze world cup.Leo muda wa saa kumi za alasiri Kuna tukio.Tukio lenyewe ni kati ya England na Iran Kuna vitu vingi...
21/11/2022

Tuzungumze world cup.
Leo muda wa saa kumi za alasiri Kuna tukio.
Tukio lenyewe ni kati ya England na Iran Kuna vitu vingi watu mnaweza kuwa hamvifahamu.
1 kitu Cha kwanza masaa ya afrika mashariki na Qatar kimasaa tuko sawa mpaka sekunde Kwa hiyo tukisema mpira utakuwa saa kumi basi Kila doti tuko sawa

2 kombe lenyewe ni balaa unaposema pombe haitakiwi kabisa hii Ina maana na k**a wewe ni mpenda mademu basi hili kombe haliwezi kukufaa kabisa maana ukitongoza tu mtu mule ndani ya uwanja jua kabisa miaka Saba gerezani ni yako.

3 mechi yenyewe sasa England na Iran ni mechi Yao ya kwanza kukutana kwenye mashindano makubwa hawajawahi kukutana kabisa.

4 Iran Si underdog k**a mnavyodhani walimpiga Uruguay k**a kasimama na k**a ukitaka kujua ni kwamba Uruguay yupo huyu jamaa mng'ataji na mkeraji yaan Suarez utakiii......hacha mbungi lipigwe.

5 kumbukizi ya malkia Elizabeth itafanyika Kwa vijana wa malkia kupiga goti.

6 one love armband zimekataliwa kabisa na FIFA hivyo haziruhusiwi uwanjani.

7 uingereza hawajashinda mechi hata Moja walizocheza hivi karibuni huku wapinzani wao ni balaa. Tutegemee changamoto.

8 Jana katika mechi ya ufunguzi we bwanaaa we Qatar wamewekeza mizawadi ya mipira na fire work lanterns ziliwekwa..
Hii ndio world cup....ebwanaaaa eeh pilau kunukia Kwa jirani Si ulaji wako.

Goli la Ecuador dhidi ya Qatar Enner Valencia mchezaji wa fernabache anawapatia Raha mashabiki wa Ecuador Kwa goli mbili...
20/11/2022

Goli la Ecuador dhidi ya Qatar Enner Valencia mchezaji wa fernabache anawapatia Raha mashabiki wa Ecuador Kwa goli mbili ambapo goli lake la awali lilikataliwa na VAR.

Mpaka sasa equador wanaongoza mbili huku mchezaji kinara Enner Valencia akiwafunga Qatar goli mbili zote.
20/11/2022

Mpaka sasa equador wanaongoza mbili huku mchezaji kinara Enner Valencia akiwafunga Qatar goli mbili zote.

20/11/2022

Valencia anawapatia Ecuador goli la kwanza Kwa mkwaju wa penalty.
Ecuador 1 na Qatar 0

Vijana wa Ecuador wanafanya jambo hapa ndani ya dakika tatu lakini goli linakataliwa hapa albayt. Baada ya VAR kukataa g...
20/11/2022

Vijana wa Ecuador wanafanya jambo hapa ndani ya dakika tatu lakini goli linakataliwa hapa albayt. Baada ya VAR kukataa goli.
Vijana hawa wamesafiri Kwa masaa ishirini na tatu kufika Qatar. Wanaonekana ni vijana wazoefu sana mbele ya vijana wa Qatar na bao hili kidogo limewatingisha wanaonekana Qatar kulinda sana.

Ukitaka kujua fujo za mshabiki ndio hapa.Eeeh bwanaaa Qatar ni k**a wamechokoza Wana kwambia hawataki watu kushikana shi...
20/11/2022

Ukitaka kujua fujo za mshabiki ndio hapa.
Eeeh bwanaaa Qatar ni k**a wamechokoza Wana kwambia hawataki watu kushikana shikana mikono yaani wanaume Kwa wanaume au mabinti Kwa mabinti hivi vitisho bwana haviwanyimi Raha mashabiki tena hata kidogo.
Mashabiki wanakwambia pombe utatunyima ila kombe tunachukua.

Hapo hao ni mashabiki wa Croatia wametinga makanzu na wanatamba uarabuni na wanakwambia tutekenye tucheke au utaki...kombe la dunia hili mzee baba. Sisi ndo tunatamba...unahitaji lingine Ile pilipili imeanguka kwenye supu mchuzi mtamu.

Wewe.
20/11/2022

Wewe.

Kombe la dunia nchini Qatar kuanza Leo.
Huku ikiambatana na burudani kutoka Kwa mwanamuziki mahiri Shakira na mechi ya kwanza inatarajia kuwepo kati ya mwenyeji na Ecuador utakaoanza saa Moja ikumbukwe masaa ya Qatar na east Africa yako sawa hii inaamaanisha miji mingi ya south America watakuwa wanacheki mpira usiku...eeh bwanaaa ee imagine baba watoto anakwambia mama watoto naomba nikacheki mpira kibanda umiza muda wa saa nane usiku.
Si hivyo ni picha ya pamoja ya Luis Vuitton kati ya mess na Ronaldo kuelekea mchuano mkubwa huu. Na ikizingatiwa kuwepo Kwa sintofahamu aliyoitoa Cris this week na sakata dhima kati yake na Manchester united we bwanaaa we pilipili limemwagikia mchuzi utamu wake Si unaujua tukutane Qatar baadae....

Kombe la dunia nchini Qatar kuanza Leo.Huku ikiambatana na burudani kutoka Kwa mwanamuziki mahiri Shakira na mechi ya kw...
20/11/2022

Kombe la dunia nchini Qatar kuanza Leo.
Huku ikiambatana na burudani kutoka Kwa mwanamuziki mahiri Shakira na mechi ya kwanza inatarajia kuwepo kati ya mwenyeji na Ecuador utakaoanza saa Moja ikumbukwe masaa ya Qatar na east Africa yako sawa hii inaamaanisha miji mingi ya south America watakuwa wanacheki mpira usiku...eeh bwanaaa ee imagine baba watoto anakwambia mama watoto naomba nikacheki mpira kibanda umiza muda wa saa nane usiku.
Si hivyo ni picha ya pamoja ya Luis Vuitton kati ya mess na Ronaldo kuelekea mchuano mkubwa huu. Na ikizingatiwa kuwepo Kwa sintofahamu aliyoitoa Cris this week na sakata dhima kati yake na Manchester united we bwanaaa we pilipili limemwagikia mchuzi utamu wake Si unaujua tukutane Qatar baadae....

15/11/2022
Simba wanashinda dhidi ya de agosto wanaupiga mwingi Kuna mengi ya kuzungumza hapa.Cha kwanza mgunda Huyu mgunda anajua ...
10/10/2022

Simba wanashinda dhidi ya de agosto wanaupiga mwingi Kuna mengi ya kuzungumza hapa.

Cha kwanza mgunda
Huyu mgunda anajua football anajua kuchanganya kachumbali vizuri tokea ameachiwa mikoba na kocha zolan jamaa ameweza tengeneza game plan nzuri ambayo inashinda popote.

Ukiangalia Jana ni k**a waliwaheshimu de agosto ambao walikuwa na Hali ya juu katika utafutaji wa goli katika uwanja wao japo Simba walitulia sana na kuweza kuwamark vizuri hii ilikuwa ni game plan nzuri sana upande wao. Na inaonyesha ukak**avu wa mgunda.

Mbili performance ya baka yaan mcheza majukwaa ilitulia hii inaonyesha jinsi Gani mgunda kampika baka (enock hinonga) na kufanya arudi kwenye ubora wake wa juu sana. Katika kukontrol na kucheza mipira Kwa muda muafaka.

Tatu ni huyu mwenda lile goli la pili ni la aina yake unapiga movement Kali lakini mwisho wa siku unapambana na mpira unakuwa huna mambo mengi scoring ni muhimu sana k**a una mambo mengi bigup Kwa mwenda.

Address

Mbeya City
Kariakoo

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Gotgo times habari motomoto posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share