Uzazi Bora Clinic

Uzazi Bora Clinic Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Uzazi Bora Clinic, Business Center, Mbeya.

29/06/2026

🇨🇦

28/06/2026

Mwanaume tumekuletea tumaini jipya la kumaliza tatizo la tezi dume bila upasauji wala dawa zenye chemical.
Uzazibora clinic tumaini lako.
Wasiliana nasi:+255754638695.

28/06/2026

Wewe ni mwanamke wa miaka30 na zaidi
Umekuwa ukitafuta mimba kwa zaidi ya miezi 6 bila mafanikio?
Uzazibora clinic tunakuwezesha uweze kushika mimba ndani ya siku30 tu.

21/04/2026

Matatizo ya Korodani (Testicular Problems)
Korodani ni viungo muhimu kwa mwanaume vinavyohusika na uzalishaji wa mbegu za uzazi (sperms) na homoni ya testosterone.

Matatizo yake yakipuuzwa yanaweza kuathiri uzazi na afya kwa ujumla.
1.Hydrocele
Maana.
Maji kujaa kwenye mfuko wa korodani.
Dalili.
Uvimbe usio na maumivu makali, uzito kwenye korodani.

Madhara.
Huongeza ukubwa wa korodani na kuleta usumbufu wa muda mrefu.

2.Varicocele
Maana,Mishipa ya damu kuvimba ndani ya korodani.

Dalili.
Maumivu ya kuvuta, korodani kushuka au kuhisi nzito.

Madhara.
Inaweza kusababisha ugumba (infertility).

3.Testicular torsion
Maana.
Korodani kuzunguka na kukata mzunguko wa damu.

Dalili.
Maumivu makali ya ghafla, uvimbe, kichefuchefu.

Hatari.
Ni dharura ya kitabibu – kuchelewa kunaweza kusababisha kupoteza korodani.

4.Orchitis
Maana.
Maambukizi au uvimbe wa korodani.
Dalili.
Maumivu, homa, uvimbe.

Madhara.
Inaweza kuathiri uzalishaji wa mbegu za uzazi.

5.Testicular cancer
Dalili za tahadhari.
Uvimbe usio na maumivu
Kubadilika kwa ukubwa wa korodani
Maumivu ya mgongo au tumbo la chini

Faida ya kugundua mapema.
Saratani ya korodani ikigunduliwa mapema hutibika kwa kiwango kikubwa sana.

Dalili Hatarishi Zinazohitaji Uchunguzi Haraka
Maumivu makali ya ghafla
Uvimbe unaoongezeka
Korodani kuwa ndogo au kunywea
Maumivu yanayoendelea zaidi ya siku chache

Ushauri wa Kitaalamu
✔️Jifanyie uchunguzi wa korodani mara moja kwa mwezi
✔️Epuka maambukizi ya zinaa kwa kujikinga
✔️Fika hospitali mapema ukiona dalili zisizo za kawaida
✔️Epuka kujitibu bila ushauri wa daktari.

Wasiliana nasi kwa ushauri zaidi na uhakika wa matibabu+255754638695

15/04/2026

Wanaume wengi hukaa kimya wanapopata dalili za matatizo ya korodani—wakidhani yataisha yenyewe, au wakihofia kusema.

Lakini ukweli ni kwamba kuchelewa kutafuta matibabu sahihi kunaweza kuleta madhara makubwa, si tu kimwili bali pia kihisia.

Fikiria maumivu yanayoanza kidogo, kisha yanaongezeka taratibu hadi kuwa makali kiasi cha kukunyima usingizi na amani ya moyo.

Kuvimba kunapoanza, huja na hofu—hofu ya kutojua kinachoendelea ndani ya mwili wako.

Unajiuliza:
Je, nitakuwa sawa tena?
Kadri muda unavyopita bila matibabu sahihi, hali inaweza kuwa mbaya zaidi.

Mbegu za kiume zinaweza kuharibika, na ndoto ya kupata mtoto inaweza kufifia polepole.

Hili linaweza kuleta huzuni kubwa, msongo wa mawazo, na hata kupoteza kujiamini k**a mwanaume.

Wakati mwingine, matatizo haya yakipuuzwa kwa muda mrefu yanaweza kugeuka kuwa magonjwa hatari zaidi k**a saratani ya korodani.

Hapo ndipo majuto huanza—ukitamani ungechukua hatua mapema.
Usikubali ukimya au hofu vikunyime afya yako.

Kuchukua hatua mapema ni kujali maisha yako, ndoto zako, na familia yako.

Afya yako ni muhimu. Usichelewe. Tafuta matibabu sahihi mapema.
Dr. Ibrahim
📞 +255754638695

21/03/2026
21/03/2026

Matatizo ya Korodani (Testicular Problems)
Korodani ni viungo muhimu kwa mwanaume vinavyohusika na uzalishaji wa mbegu za uzazi (sperms) na homoni ya testosterone.

Matatizo yake yakipuuzwa yanaweza kuathiri uzazi na afya kwa ujumla.
1.Hydrocele
Maana.
Maji kujaa kwenye mfuko wa korodani.
Dalili.
Uvimbe usio na maumivu makali, uzito kwenye korodani.

Madhara.
Huongeza ukubwa wa korodani na kuleta usumbufu wa muda mrefu.

2.Varicocele
Maana,Mishipa ya damu kuvimba ndani ya korodani.

Dalili.
Maumivu ya kuvuta, korodani kushuka au kuhisi nzito.

Madhara.
Inaweza kusababisha ugumba (infertility).

3.Testicular torsion
Maana.
Korodani kuzunguka na kukata mzunguko wa damu.

Dalili.
Maumivu makali ya ghafla, uvimbe, kichefuchefu.

Hatari.
Ni dharura ya kitabibu – kuchelewa kunaweza kusababisha kupoteza korodani.

4.Orchitis
Maana.
Maambukizi au uvimbe wa korodani.
Dalili.
Maumivu, homa, uvimbe.

Madhara.
Inaweza kuathiri uzalishaji wa mbegu za uzazi.

5.Testicular cancer
Dalili za tahadhari.
Uvimbe usio na maumivu
Kubadilika kwa ukubwa wa korodani
Maumivu ya mgongo au tumbo la chini

Faida ya kugundua mapema.
Saratani ya korodani ikigunduliwa mapema hutibika kwa kiwango kikubwa sana.

Dalili Hatarishi Zinazohitaji Uchunguzi Haraka
Maumivu makali ya ghafla
Uvimbe unaoongezeka
Korodani kuwa ndogo au kunywea
Maumivu yanayoendelea zaidi ya siku chache

Ushauri wa Kitaalamu
✔️Jifanyie uchunguzi wa korodani mara moja kwa mwezi
✔️Epuka maambukizi ya zinaa kwa kujikinga
✔️Fika hospitali mapema ukiona dalili zisizo za kawaida
✔️Epuka kujitibu bila ushauri wa daktari.

Wasiliana nasi kwa ushauri zaidi na uhakika wa matibabu+255754638695

15/03/2026

JE, KAZI YAKO INAKULAZIMISHA KUKAA MUDA MREFU? CHUNGA HATARI YA BAWASIRI (HEMORRHOIDS)
​Watu wengi wanaofanya kazi za ofisini, madereva wa masafa marefu, na wale wanaokaa sehemu moja kwa zaidi ya saa 5-8 kila siku, wako kwenye hatari kubwa ya kupata tatizo la Bawasiri.

​Kwa nini kukaa sana ni tatizo?

​Unapokaa kwa muda mrefu, unazidisha mgandamizo (pressure) kwenye mishipa ya damu ya sehemu ya haja kubwa.

Mgandamizo huu husababisha mishipa hiyo kuvimba na kulegea, jambo linalopelekea.

​Maumivu makali wakati wa haja kubwa.
​Kujitokeza kwa kinyama sehemu ya siri au haja kubwa
​Kuwashwa na kutoa damu.

​Hatua 3 za Kuchukua Leo Ili Kujikinga.

​Kanuni ya Dakika 50.
Usikae zaidi ya saa moja bila kusimama.

Kila baada ya dakika 50, simama na tembea kwa dakika 5-10 ili kuruhusu mzunguko wa damu ukae sawa.

​Maji na Nyuzinyuzi (Fiber).
Hakikisha unakunywa maji ya kutosha (lita 2-3 kwa siku) na kula mboga za majani na matunda (k**a papai au kucha za okra) ili kulainisha choo na kuepuka kukamua.

​Tumia Mto Laini (Cushion).
Ikiwa ni lazima ukae, hakikisha kiti chako kina mto laini ili kupunguza mgandamizo wa moja kwa moja kwenye misuli ya nyonga.

​Afya Yako Ni Uwekezaji Wako!
​Usisubiri mpaka maumivu yawe makali.

Anza leo kubadili mfumo wako wa maisha na kulinda mwili wako.

​Afyataasisi
Elimu ya Afya kwa Maendeleo Yako.

K**a ungependa kupata ushauri zaidi wa kimatibabu kwa tatizo la bawasiri ili kuepuka matibabu ya upasuaji
Piga simu hii+255754638695.

15/03/2026

Kukaa sana sehemu moja kwa muda mrefu, hasa kwa wale wanaofanya kazi za ofisini, udereva, au ufundi wa mitambo, kunaweza kuwa na athari za moja kwa moja kwenye afya ya mfumo wa uzazi wa mwanaume, hususan korodani.

​Hizi hapa ni athari kuu na namna zinavyotokea.

​1.Kuongezeka kwa Joto (Scrotal Hyperthermia)
​Hii ndiyo athari kubwa zaidi.
Korodani zimeumbwa kukaa nje ya mwili ili ziwe na joto ambalo ni pungufu kwa nyuzi joto ka 2 hadi 3 kulinganishwa na joto la ndani ya mwili.Hali hii ni muhimu kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu (spermatogenesis).

​Athari.
Unapokaa sana, mapaja yanabanana na mzunguko wa hewa unakata, jambo linalofanya joto kuongezeka.

Joto likizidi, uzalishaji na ubora wa mbegu hupungua kwa kiasi kikubwa na kuathiri afya ya uzazi kwa mwanaume.

​2.Hatari ya Kutanuka kwa Mishipa (Varicocele)
​Kukaa kwa muda mrefu kunaweza kuongeza shinikizo kwenye mishipa ya damu ya eneo la nyonga (pelvic region).

​Athari.
Hali hii inaweza kuchochea au kuzidisha tatizo la varicocele (mishipa ya damu kutanuka ndani ya mfuko wa korodani), jambo linaloweza kusababisha maumivu butu na kuathiri urutubishaji.

​3.Msongo wa Mishipa ya Fahamu (Nerve Compression)
​Kukaa kwenye kiti kigumu au katika pozi moja kwa saa nyingi kunaweza kukandamiza mishipa ya fahamu inayopita eneo la katikati ya njia ya haja kubwa na sehemu za siri (perineum).

​Athari.
Hii inaweza kusababisha hali ya ganzi, muwasho, au maumivu yanayoweza kusambaa hadi kwenye korodani.

​Hatua za Kuchukua (Kinga)
​Ili kulinda afya yako ukiwa kazini, unaweza kuzingatia mambo yafuatayo.

​Sheria ya Dakika 50/10.
Kwa kila dakika 50 unazokaa, simama na utembee kwa angalau dakika 10 ili kuruhusu mzunguko wa hewa na kupunguza joto.

​Uchaguzi wa Mavazi.
Vaa nguo za ndani za pamba (cotton) ambazo hazibani sana ili kuruhusu hewa kupita vizuri.

​Aina ya Kiti.
Tumia kiti kinachoweza kurekebishwa na chenye mfumo mzuri wa hewa (mesh chairs).

​Maji ya Baridi.
Unapokoga, hakikisha unatumia maji ya kawaida (baridi kiasi) eneo la siri ili kusaidia kupoza joto lililokusanywa mchana kutwa.

K**a unashida yoyote ya korodani ama mfumo wa uzazi kwa mwanaume,wasiliana nasi kupata msaada wa haraka ili kudumisha na kuimarisha afya bora ya korodani.
Piga simu+255754638695.
​

Address

Mbeya

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Uzazi Bora Clinic posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share