Marry Malaki

Marry Malaki Yohana 3:16

MPENDE MUNGU 100%WAPENDE WAZAZI 80%MPENDE MUME /MKE/WATOTO 75%WAPENDE WATU 70%MPE MUNGU ASILIMIA ZOTE MPENDE KWA ROHO YA...
26/07/2026

MPENDE MUNGU 100%
WAPENDE WAZAZI 80%
MPENDE MUME /MKE/WATOTO 75%
WAPENDE WATU 70%
MPE MUNGU ASILIMIA ZOTE
MPENDE KWA ROHO YAKO YOTE
KWA MOYO WAKO WOTE
NAFSI YAKO IMPENDE MUNGU
NDIYE ATAKAEKUPA NAMNA YA KUISHI NA WATU

20/07/2026

Wakati mwingine ,Mungu huondoa kila aina ya msaada wa kibinadamu, ili ujue kuwa yeye pekee anatosha!

(MWANZO 17:1---)➡️Nguvu ya Jina Bwana Yesu asifiwe Ipo nguvu katika jina lako ,ambayo imesimamia kwako na ndo inaleta ma...
20/07/2026

(MWANZO 17:1---)

➡️Nguvu ya Jina
Bwana Yesu asifiwe
Ipo nguvu katika jina lako ,ambayo imesimamia kwako na ndo inaleta matokeo ya maisha yako unayoishi sasa
Kuna watu wanaishi maisha ambayo yamebarikiwa na Bwana baada ya majina yako kubarikiwa na kuwekewa wingo wa Mungu
Neema hiyo ikupate na wewe
Unaweza kubadili jina likakupa matokeo hasi ama chanya kutengemeana na njia uliyotumia
Pia kuna watu walizaliwa wakapewa majina ambayo kiukweli hayakuwa mpango sahihi yamefanya matokeo ya maisha yao kuwa mbaya
Bwana atusaidie
Tuziona Baraka za Mungu juu ya Ibrahimu kupewa Jina jipya likiwa na maana ya kubeba uzak ambao atskuwa baba wa mataifa
(MIMI NA WEWE NI WATOTO WA IBRAHIMU KWA IMANI)

➡️Mungu hachelewi wala hawahi
Wakati wa Mungu ni wakati sahihi sana pale anapotaka kufanya jambo lake
Kikubwa ni kuwa na subira katika kila jambo
Jaribh lolote lile lipe muda ,vumilia unapohisi kujata tamaa ndipo Mungu huinuka na kukuinua juu zaidi

Ameni

TAFAKARI YA NENO*MWANZO 1:1-31*Hallelujuh!Bwana wetu Yesu Kirsto Asifiwe🖐️🖐️🖐️🖐️1️⃣.Weka ratiba katika safari yako ya Wo...
07/07/2026

TAFAKARI YA NENO
*MWANZO 1:1-31*

Hallelujuh!
Bwana wetu Yesu Kirsto Asifiwe🖐️🖐️🖐️🖐️

1️⃣.Weka ratiba katika safari yako ya Wokovu
Nimejifunza kuwa ratiba kwenye kila jambo langu ambalo natamani kulifanya ,Mungu wetu ni Mungu wa utaratibu sana
Tangu siku ya kwanza ya uumbaji wake amekuwa na siku tano ambazo siku hizo kila mmoja na ratiba yake
Uwezo alionao BABA YETU ni mkubwa sana kiasi kwamba hayo yote aliyoyafanya ndani ya siku 5 alikuwa anauwezo wa kuyafanya siku moja,lakini anatufundisha namna ambavyo tunapaswa kuweka ratiba zetu vizuri ili kila tulifanyalo tulifanye kwa ufasaha na utaratibu maalumu ,hii itakusaidia kukuza kiakiri na kuweka utulivu

2️⃣.Ufahamu wa binadamu (Akiri)
Alimuumba binadamu kwa mfano wake ,jambo la kwanza baada ya kuumba binadamu alimpa ufahamu ambao ulimsaidia mtu huyo kutambua kila aliloambiwa na BABA YETU
isingekuwa ufahamu asingekabidhiwa miliki hiyo ,alimkabidhi ikiwa tayari alikuwa ameweka ufahamu ndani yake,jambo ambalo adui analitumia sana ni kuharibu ufahamu wa mtu
Maana palipo na akiri ndipo kila jambo huzalishwa
Ko anajua njia ya kumk**ata binadamu ni ufahamu
Watu wengi wamek**atwa fahamu zao na kuachiliwa fahamu za mizimu
Ndio maana huoni Nuru
Huoni miliki ile Mungu alikukabidhi
Huoni tena mafanikio
Kazi unafanya lakink huoni mwanga
Adui kashika eneo la ifahamu
Adui Akishika ufahamu (akiri)
Anaachilia tabia za kuzimu
Ufahamu wa ngiza

Mungu awabariki sana

11/04/2026

KIBALI KAZINI
NA
Marry Malack
0759984391

Wakati wa Mungu ndio sahihi kwako kukuwezesha
Maombi ya kibali kazini
Inawezekana upo kazini lakini hauna kibali

Yaani huna Amani na waajiri wako
Wamekuchoka
Hawakuelewi
Kila kukicha afadhali ya jana
Kila ufanyalo haoni wema wako hata kidogo

Adui ameiba kibali chako ndo maana unapata changamoto hizo

Muombe Mungu aachilie kibali kazini kwako

Yusuph aliwekwe kila aina ya vikwazo lakini Mungu bado alimpa kibali na kumpandisha juu

Tunajifunza hali ya kumtumaini Mungu pekee

Neno hilo likawa jema machoni pa Farao, na machoni pa watumwa wake wote.
Mwanzo 41:37

38 Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu k**a huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?
Mwanzo 41:38

39 Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima k**a wewe.
Mwanzo 41:39

40 Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe.
Mwanzo 41:40

41 Farao akamwambia Yusufu, Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri.
Mwanzo 41:41

42 Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
Mwanzo 41:42

43 Akampandisha katika gari lake la pili alilokuwa nalo. Na watu wakapiga kelele mbele yake, Pigeni magoti. Hivyo akamweka juu ya nchi yote ya Misri.
Mwanzo 41:43

44 Farao akamwambia Yusufu, Mimi ni Farao, na bila amri yako, mtu asiinue mkono wala mguu katika nchi yote ya Misri.
Mwanzo 41:44

KIBALI MBELE ZA MUNGU   NaMarry Malack  +255759984391Kibali ,ni hatua ya kukubalika kwa Mungu ,mtu ,kazini,family na jam...
11/04/2026

KIBALI MBELE ZA MUNGU
Na
Marry Malack
+255759984391

Kibali ,ni hatua ya kukubalika kwa Mungu ,mtu ,kazini,family na jamii kwa ujumla

Unapokuwa na kibali ndipo huwa unakuwa na ruhusa ya kufanya jambo ,ama kuomba jambo sehemu uliyojipatia kibali

Unapaswa kujua hali uliyo nayo sasa inakuruhusu kuomba kibali ?

Ni hatua ya kuingia ndani zaidi na kukaa ,kusikiliza na kujifunza zaidi
Napo ni baada ya Mungu kukupa kibali

Unapopata kibali kwa Mungu hutuketisha mazungumzoni na kuanza kutupa maelekezo zaidi nini twapaswa kufanya na ni kwa wakati ngani

Ili upate kibali na mazungumzo na Mungu yakupasa uwe msafi yaani kujitakasa

1 Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu.
Kutoka 3:1

2 Malaika wa Bwana akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea.
Kutoka 3:2

3 Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei.
Kutoka 3:3

4 Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa.
Kutoka 3:4

5 Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu.
Kutoka 3:5

6 Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu.
Kutoka 3:6

Address

Tanzania �
Misungwi
1999

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Marry Malaki posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share