Sauti ya Flora

Sauti ya Flora Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Sauti ya Flora, Nyankumbu, Morogoro.

ukiwa kazini jichague wewe kwanza sababu kazi itaisha wewe utabaki,ukiwa katika mahusiano jichague wewe kwanza sababu up...
24/02/2026

ukiwa kazini jichague wewe kwanza sababu kazi itaisha wewe utabaki,
ukiwa katika mahusiano jichague wewe kwanza sababu upendo huisha wewe utabaki,
ukiwa na rafiki jichague wewe kwanza sababu urafiki unaweza geuka uadui wewe utabaki,
katika familia jichague wewe kwanza sababu ndugu waweza tawanyika na kugawanyika,ndugu yako wa damu anaweza kukutoa hata uhai ili kutetea maslahi yake,
ukiwa unatafuta maisha pia usisahau kuishi sababu maisha Yana mwisho na hujui wakwako utakuwa lini

31/01/2026

Wasiliana na mwalimu mkuu kupata maelekezo 0685640382

10/12/2024
09/12/2024
08/06/2022
08/04/2022

MY STORY; MKE WANGU SITAKI UPUMZIKE KWA AMANI!

Ni miezi miwili tangu nimzike mke wangu, nyumba imekua kimya sana, pamoja na kukaa naye kwenye ndoa kwa miaka 7 leo ndiyo k**a nimegundua kuwa nilikua na mke.

Wakati wote wa ndoa nilikua namuona k**a lidubwasha flani tu lipo kunijazia choo. Nilishamfukuza mara nyingi, nilishampiga mara nyingi nikimuambia kuwa hana akili, mjinga kaja kunijazia choo tu hana faida.

Kusema kweli sikuwahi kuwaza k**a itakuja kutokea siku k**a hii ya leo nikatamani kuwa na mke wangu. Ndugu zangu walikua ndiyo kila kitu kwangu, hasa dada yangu mkubwa, kaolewa lakini kila siku alikua anakuja kwangu.

Anakagua nyumba na kuniambia ni chafu, naishia kumpiga mke wangu kumuambia kazi yake ni kula na kunya tu hata kufanya usafi hawezi.

Niulishamnyang’anya watoto na kuwapeleka kwa dada yangu, wanakaa muda nawarudisha, nilishamlaza nnje mara nyingi, nikampiga mbele ya watoto.

Niliwakataza mpaka wanangu kumuita Mama, ni kawaambia mtu mwenye hadhi ya kuitwa Mama ni mama yangu tu yeye ni mjinga hapaswi kuitwa Mama. Nikataka wamuite kwa jina lake. Lakini miezi miwili iliyopita kila kitu kilibadilika, niliamka asubuhi k**a kawaida yangu nikiwaza kwenda kazini.

Mke wangu hakua kitandani, sikushangaa yeye kutokua kitandani ila nilishangaa kwanini hajaniamsha wakati jua lilishaanza kuwaka.

Nilintanyuka huku nikitukana, nikaenda sebuleni nakuta watoto bado hawajaandaliwa, jikoni simuoni, nikarudi chumbani huku nikitukana.

Naingia bafuni namkuta kalala, nahisi labda kachoka kajilaza, naanza kumpiga huku nikimtukana ili anyanyuke ila hakunyanyuka.

Alikua ameshakauka muda mrefu, hata hakuonekana kudondoka bali kukaa. Naita watu, mwili unachukuliwa, Baada ya vipimo kumbe presha ilipanda, mishipa ya kichwa ikapasuka.

Naumia zaidi kwakua usiku wake nilikua namtishia aondoke kwani aliedna hospitalini kupima ana ujauzito ambao ingawa nilijua kuwa ni wangu ila nilimuambia si wangu atafute mwanaume wakumpa. Sikumgusa usiku huo, si kwakua sikutaka ila nilikua niemchoka sana, kumtukana tu nilimtukana.

Mke alizikwa, nilijikaza silii, nilikua sioni umuhimu wake. Lakini miezi miwili tu, mke wangu kafariki, kila siku nilikua namuambia aondoke anichie watoto leo kaondoka, kaniachia, baada ya mazishi niliwapaleka kwa Dada ila leo kawarudisha anasema kazi zimemzidia nitafute mfanyakazi.

Dada yuleyule aliyekua akiniambia “Aondoke kwani alikuja na na watoto, wanao ni damu yetu tutalkea!” Leo miezi miwili tu mke wangu kaondoka hakuna hata ndugu anayekuja kunisalimia.

Nimekaa mwenyewe na wanangu, kila dakika wanamuulizia Mama yao na sijui cha kuwajibu. Mke wangu nionyeshe ishara nifanye nini na hawa watoto, Mama kaniambia niwapeleke Kijijini lakini naona ugumu kwani umri wake mkubwa na kule maisha ni magumu.

Nataka kumleta kwangu akae na wajukuu zake lakini hataki kuondoka kijijini. Mke wangu ni k**a umeondoka na kila kitu, umeondoka na furaha yangu, kila mtu kanigeuka mke wangu. Natamani hata ningekuonyesha upendo.

Vile vitu vyote nilivyokua nakunyanyasia mke wangu, nyumba, gari ambayo hukuwahi kuipanda, miaka minne mimi mume wako nilikua na gari lakini ulipanda Bajaji, hukuwahi kuipanda hata siku moja ila ndugu na marafiki nilikua nawaazima waitumie.

Mke wangu leo ndiyo nimejua nakupenda, sioni hata sababu ya kuamka tena. Natamani sana hata ungejua nijinsi gani nilikua nakupenda, nilishindwa kukuonyesha upendo, najua unaweza usiamini ila naumia na sijui maisha yangu bila wewe yatakuaje.

Ningesema upumzike kwa amani ila sitaki upumzike mke wangu. Naomba hata unisaidie kuela hawa watoto, waambie kitu wanyamaze. Nilijitahidi Sana wakuchukie kila dakika wanakuita wewe, nisaidie mke wangu usipumzike kwanza.

MWISHO

03/04/2022

Nina miaka 52, najua kila mtu atanishangaa lakini natamani ungekuepo kipndi hicho naachana na baba wa mtoto wangu.

Aliniacha kwa dharau, akaniambia nina mikosi, siwezi kupata mwanaume wa kunioa kwani hata yeye kuwa na mimi sio k**a alinipenda bali alielekezwa na mganga ila ameona n**idi kumletea mikosi.

Nilikua sijipendi, nina hasira, nikikutana na mwanaume mwili unawake moto, mwanaume akinisalimia naona k**a vile ananidhihaki.

Nakua nawaza k**a nanuka kwanini wananisalimia, nilikataa wanaume wazuri, kila mmoja alikua ananishangaa kwani ni mzuri ila nilikua najiona k**a takataka.

Maneno yake mpaka leo hayaondoki kichwani kwangu. Nimekua nikikusoma muda mrefu, nafarijika lakini sasa hivi ndiyo umenigusa kabisa. Yule mwanaume alinifanya nisijiamini, nijichukie.

Nina kazi nzuri mtu mkubwa sana lakini nikitoka kazini naishia kujifungia ndani, hujui tu ulichonifanyia ila nakushukuru sana. Nilikua najichukia sana kutoka na mwanaume, nimesoma kitabu chako nimejua ni kwanini aliniambia vile.

Kwanza nilimzidi elimu, cheo na kila kitu nilimzidi, alikua anajaribu kunishusha na kweli aliweza, nilizaa naye mtoto mmoja lakini mpaka leo hataki hata kumuona mtoto, nina miaka 52, mwanangu niliozaa naye ana miaka 27, tangu kuachana naye mwenetu akiwa na miaka 2 sijawahi kukutana kimwili na mwanaume yoyote yule.

Kikubwa nikuwa naogopa, najichukia. Nashukuru na natamani uongee na mwanangu kwani naona k**a naye anakua k**a mimi, nimemlea kuchukia wanaume, kuogopa wanaume na kutokujipenda, nitakulipe chochote ili tu umfanye mwanangu asiwe k**a mimi maana naona naye ni mtu wa kujifungia ndani k**a mimi.

NB: Ukiona mwanaume anakuacha kwa daharu, kukutukana kuwa wewe si wa hadhi yake, unanuka, hutakuja uolewe, una mikosi basi juakua hajiamini na anataka usijiamini.

Cheka na akikuambia “Hutakuja kupata mwanauume k**a Mimi!” Muambie “Nishakua na wewe sihitaji tena mwanume k**a wewe, nahitaji Bora zaidi na nilivyo mtamu nitampata!”

Ondoka kifua mbele ukijua kuwa huyo mwanaume hjakua wa hadhi yako! Mwanaume kamili akiachana na mwanamke hana haja ya kumtukana, anaenda na mambo yake anajua ndiyo maisha, ila wale wa hovyo atakutukana mpaka ukoo wako mzima!

07/01/2022

NAFANYA BIASHARA YA CHAKULA SIPATI FAIDA YOYOTE!

Nilinunua Kitabu chako cha Biashara 50, kutokana na mazingira yangu basi nikaamua kufungua Biashara ya chakula. Sina mtaji mkubwa hivyo napikia nyumbani kisha napeleka kukisambaza.

Shida nikuwa, naona k**a sipati faida yoyote, chakula kinaisha kweli lakini nikipiga mahesabu najikuta narudisha pesa ya kununulia vitu, nishauri Kaka nifanye nini wakati mwingine nakosa hata nauli.

Napika wali, sahani moja wali maharage nauza Buku na wali nyama nauza 1500/-

JIBU LANGU, NINI CHA KUFANYA?

Kwanza hongera kwa kuamua kuanza, najua kuna changamoto nyingi ila naamini utatobboa, hata k**a unachokipata ni kidogo lakini angalau umetoka na akili imefunguka.

Katika Biashara ya chakula hasara inatokana katika sehemu kuu tatu Upishi, kwenye kupakua na bei ya chakula.

(1) Upishi; Mtu anayenunua chakula cha 1,000-1,500 mara nyingi haangalii ubora bali kushiba. Hivyo, ili kupunguza gharama angalia vituunavyotumia, kwa mfano nyanya, n**i, kiwangoc ha nyama na viungo vyake.

Najua kuna baadhi ya wateja wanataka ubora, ila kwa kuanza, pika kutokana na uwezo wa sasa wa wateja wako, ukipanuka utapandisha bei.

Kwenye mboga hakikisha unaweka vile vitu vya lazima tu, kiwe Kitabu lakini kisikugharimu sana. K**a ni Mchele unaotumia usiwe wa bei ghali sana, chukua wa kawaida ila upike vizuri.

(2) Kupakua; Wateja kila siku watataka kingi lakini hawatakua tayari kuongeza pesa. Weka kipimo maalum na hakikisha unakisimamia. Kwa mfano, kwa kilo moja ya mchele mara nyingi inatoa kuanzia sahani 5 mpaka 6 za wali.

Chini ya hapo utakuta ni hasara. Kwa upande wa nyama, weka finyango mbili mpaka tatu kulingana na ukubwa. Pia zisiwe kubwa sana, ukikata vifinyango vitatu mtu anaona vingi kuliko moja kubwa!

(3) Bei; Hapa kwasasa soko ndiyo linakuamulia bei, uwezi kupandisha bei wakati kila mtu anauza tofauti. Lakini sasa ni ngumu kidogo kutoka kwa bei hiyohiyo.

Hivyo, unatakiwa kuwa na malengo ya muda mrefu. Anza kutafuta wateja wa kununua chakula cha bei ghali.

Zunguka maofisini kupokea oda, na sehemu ambazo utakuta watu wanye uwezo wa kununua chakulacha hata 2,000 mpaka 3,000.

07/11/2021

UNAANZA BIASHARA? USIOGOPE UKIKUTANA NA HALI HII!

K**a unafanya Biashara unatakiwa kujua kitu kimoja, wakati wa kuanza idadi kubwa ya watu wanaokuja kununua kwako si wateja bali ni watu ambao huja kujaribu huduma zako kuona k**a ni nzuri, wengine huja kinafiki kukuchira katika kutafuta mapungufu ili wapate cha kusema na wengine huja kwakua tu walikua wanapita umbea wakaona vitu vizuri au wanataka kukaa sana ili kupiga umbea mwingi na kuona aibu wakaamua kununua.

Kwa maana hiyo basi mara nyingi unakuta mwanzo wa Biashara kunakua na wateja wengi lakini baada ya muda unakuta hakuna mtu na kuanza kuwaza labda ni gundu au jirani kakuona unauza sana kakuloga. Kabla ya kukata tamaa hembu jiulize, ni mara ngapi wewe mwenyewe ushapita mjini na kuona duka jipya la nguo.

Lakini baada ya siku hiyo hukurudi tena na hata siku ukapita na rafiki yako nayeye akawa na hamu ya kuingia ili tu kujua na kupiga umbea k**a wewe ila ukamuambia “Wala hawana kitu pale nilishakulaga chakula chao si kizuri kihivyo?” Sio kwamba una roho mbaya bali ndiyo maisha yalivyo na ndiyo Biashara nyingi huanza hivyo. Hiyo ni hatua ya pili ya Biashara, k**a ni mfanyabiashara basi hatua ya kwanza utauza sana, yapili watu watakukimbia na ya tatu ni kutengeneza wateja wa kudumu.

Usikatishwe tamaa na hatua ya pili ya Biashara yako, ukaona k**a vile una gundu na kutaka kufunga Biashara. Watu wengi na hata wateja wangu ambao hawaelewi, hunipigia simu na kuniambia Kaka nimekua nikiuza labda chakula sahani 50 lakini sasa hivi nauza sahani kumi tu au ishirini sijui kuna nini? Mimi nawaambia hapo upo katika hatua ya pili ya Biashara yako, hao wanaonunua sasa ndiyo wateja wako wale wengine thelathini walikua wapiti njia wanajaribu huduma.

K**a uko katika hali hii badala ya kukata tamaa na kuwaza kufunga Biashara au kubadilisha Biashara nyingine hembu waza namna ya kukuza Biashara yako, hao ulionao kwa sasa ndiyo wateja wako, ndiyo wastani wa wateja wako hivyo unachotakiwa kufanya ni kwanza kuwafanya kuwa wateja wa kudumu na pili ni kujifunza namna ya kutengeneza wateja wapya. Hao wateja ulionao wakiridhika basi jua inatosha kufungua milango mingine ya wateja.

Kuna muda utashinda,Kuna muda utashindwa,Kikubwa upo hai, upo hai ili upambanie kesho yako
23/07/2021

Kuna muda utashinda,
Kuna muda utashindwa,
Kikubwa upo hai, upo hai ili upambanie kesho yako

Matatizo ni k**a makalio,,Kuna wenye makubwa wengine madogo lakini hakuna asiyekuwa nayo
03/12/2020

Matatizo ni k**a makalio,,
Kuna wenye makubwa wengine madogo lakini hakuna asiyekuwa nayo

Address

Nyankumbu
Morogoro
2015

Telephone

+255746304577

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sauti ya Flora posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Sauti ya Flora:

Share