Donnie_collection

Donnie_collection Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Donnie_collection, Business consultant, Mwanza.

11/01/2024

Mara ngapi unafanya vitu kwa ajili ya watu wengine? Na kujisahau wewe?

Yaani kila kitu unachokifanya unafanya kwa ajili ya watu wengine kuna wakati unadiliki hata kujinyima ili kuwafurahisha wengine, unakopa, unadhalilika ili tu wengine wafurahi

Unashindwa kwenda sehemu unazozipenda au kufanya vitu unavyovipenda na kukupa furaha ukiogopa watu watasema nini, sijui nitaonekanaje?

Unajua uko kwenye utumwa wa kujitakia? Unawezaje kujikomboa?

1. Jifikilie kwanza wewe kabla ya mtu mwingine, yaani utagawaje upendo kwa watu wengine akati wewe mwenyewe hujipendi? Hujijali?

2. Mwanadamu anakupenda na kukuheshimu ikiwa unafaida kwake faida ikiisha atakukimbia asikusaidie hata kidogo ukitaka kuamini siku moja waambie yaani nimepokea barua ya kuachishwa kazi na sina hata pa kuanzia ndo najitafuta naomba unikopeshe hela nianzishe biashara harafu utakuja kutupa majibu hapa wangapi watakuwa tayari kukusaidia
Je wao wamefanys nini/ au wanafanya juhudi gani kukufurahisha?
3. Wanadamu hawana shukurani wala kumbu kumbu hivyo fanya unapokuwa na nafasi k**a huna nafasi acha.
4. Kila mtu anakosea hivyo usiogope kumkosea mwanadamu
5. Sisi wote tulikuja duniani kwa njia moja na tutaondoka hivyo hivyo so usimuogope mtu

Sisemi watu msifanye vitu kwa ajili ya watu wengine lakini namaanisha fanya kulingana na uwezo wako usijikamue

Fanya vith kwa ajili yako kwanza na vyenye manufaa kwako moja kwa moja

UKIFANYA HIVI UTAVUTA MAFANIKIO KARIBU YAKOSheria ya mvuto inasema kwambaUnaweza kupata chochote unachotaka katika maish...
10/01/2024

UKIFANYA HIVI UTAVUTA MAFANIKIO KARIBU YAKO

Sheria ya mvuto inasema kwamba

Unaweza kupata chochote unachotaka katika maisha yako kupitia sheria ya mvuto k**a utaamua kufikilia katika mtazamo chanya utapata vile vile unavyotamani na k**a utakuwa na mtazamo hasi kuhisiana na maisha vitakuja vitu hasi vioe vile

1. Utajua dhahili unataka mungu akufanyie nini?
Usiseme tu nataka kufanikiwa, sawa lakini katija sehemu gani? Andika mahali kitu unachotaka kufanikiw mfano Nataka kufungua duka la nguo za watoto

2. Imani juu ya kile unachotaka kukipata na hisia utakayokuwa nayo baada ya kukipata
Imani ni kuanza kufurahia mafanikio kabla ya uhalisia, ona tayari unalo duka kubwa sana, lenye kila kitu kuhusiana na watoto, unawahudumia wateja wengi sna na wanafurahia huduma yako na wewe unafurahi sna kwa sababu watu wanafurahis huduma yako na unaweza kulipa bill zako kutokana na kipato chako

3. Vitendo

Imani bila matendo ni bure, baada ya kuona mafanikio, njoo uanze kufanya kwa vitendo taratibu taratibu imani yako ikikuongoza yaan utajikuta tu una duka kweli katika ulimwengu wa kawaida

Nimeitumia sana njia hyo kwenye maisha yangu na inafanya kazi k**a utaamini, yaan utakuwa unashangaa tu vitu vinakuja bila kutumia nguvu.. msingi wa hii njia ni imani tu

NATAMANI NINGEJUA SIRI HII MAPEMAwatu tumekukuwa na mipango mizuri ya kufanikisha ndoto zetu lakini kutekeleza mipango y...
09/01/2024

NATAMANI NINGEJUA SIRI HII MAPEMA

watu tumekukuwa na mipango mizuri ya kufanikisha ndoto zetu lakini kutekeleza mipango yetu imekuwa kitendawili kisichokuwa na majibu

Yaan unapanga kabisa mwaka huu hauishi bila kuanzisha bakery, kufungua duka la nguo au vyombo, kuanzisha shule, n.k

Umekusanya hadi mtaji wa kuanzia, unaona kabisa unaenda kufanikiwa lakini kuanza unashindwa

Wengine wanafanikiwa kuanza ila baada ya mwezi au miezi kadhaa utakuta ameshakata taa hawezi tena kuendelea kupiga hatua

Ngoja nikwambie sababu ni nini, ni kwa sababu huna "sababu yenye mashiko" inayokusukuma kufanya unachokifanya.

Jitafari kwa umakini kabisa hiyo biashara au kazi unayoifanya unaifanya kwa sababu gani? Je ni kwa sababu umeambiwa inafaida kubwa? Au rafiki yako anafanya na wewe umeona ufanye? Umeona watu wengi wanafanya na wewe unafanya?

Maana yake huna sababu zenye mashiko ambazo zimesimika mizizi ya upendo na juhudi ndani yako, hivyo ni rahisi sna wewe kuanguka unapokuta matalajio yako yapo kinyume au ulivyoambiwa na watu ni tofauti na uhalisia

Tafuta sababu yenye mashiko yaani tofauti na kupata hela kuna sababu gani nyingine itakayokuwa inakusukuma kuendelea kufanya kurudia na kurudia tena mpka pale maono yako yatakapo kuwa uhalisia

Mfano wa sababu
1. Ninajivunia na kufurahi k**a nitawasaidia watu wa inch yangu

2. Nitajivunia kuona watoto wangu wanasoma shule nzuri kutokana na kipato nitakachikiingiza kupitia shughuli hii ninayoifanya

3. Ninafuraha kwa sababu ninachokifanya kinanipa uhuru na amani

4. Nitajivunia na kufurahi k**a jina langu litatajwa na kukukumbukwa kuwa moja ya watu walioisaidi jamii yangu

5. Nitajivumia k**a nitaishi maisha ya ndoto yangu n.k

Kuwa na sababu zenye mashiko, zitakusaidia kukurudisha kwenye reli kila utakaposikia roho ya kukata tamaa

SIRI YA AKIBA1. Jua vyanzo vyako vya mapato na ni kiasi gani2. Weka lengo la kutimiza mfano: kuanzisha biashara, kununua...
09/01/2024

SIRI YA AKIBA
1. Jua vyanzo vyako vya mapato na ni kiasi gani
2. Weka lengo la kutimiza mfano: kuanzisha biashara, kununua gari, ada, vacation nk
3. Weka mpango wa kuweka akiba kwa kila mwezi
4 . Jua matumizi yako kwa mwezi
5 punguza matumizi yasiyo ya lazima

SIRI YA KUFUATA ILI UWE NA SIKU YENYE FAIDAUkiamka asubuhi vuta pumnzi ndevu na shusha pumzi kidogo kidogo mara tatuIpe ...
08/01/2024

SIRI YA KUFUATA ILI UWE NA SIKU YENYE FAIDA

Ukiamka asubuhi vuta pumnzi ndevu na shusha pumzi kidogo kidogo mara tatu

Ipe nafsi yako utulivu, futa kumbu kumbu zote mbaya

Mshukuru mungu kwa kukupa kukupa siku nyingine ya kutimiza ndoto zako, kukutanisha na watu sahihi wa kukusaidia kufanikisha ndoto zako, akupe busara ya kuwasiliana vizuri na watu, akuepushe na hasira akupe hekima ya kung'amua mambo

Soma ratiba ya shughuli zako utakazo zikamilisha kwa siku hiyo kuelekea kutimiza ndoto zako

Hakikisha unavaa vizuri na kupendeza kulingana na bajeti yako,nukia vizuri k**a unapenda

Save itakufaa
Ikikusaidia tafadhari share kwa wengine wajifunze na comment imenifaa

UNATAMANI KUBADILISHA KITU TABIA FULANI LAKINI UNAJIKUTA UNARUDIA TU? FANYA HIVI KUKOMESHA HIYO TABIA1. Kabla ya kulala ...
07/01/2024

UNATAMANI KUBADILISHA KITU TABIA FULANI LAKINI UNAJIKUTA UNARUDIA TU? FANYA HIVI KUKOMESHA HIYO TABIA

1. Kabla ya kulala andaa ratiba yako ya kesho, utakachoanza nacho na kumaliza nacho

2. Pitia malengo yako kila siku kabla ya kulala

3. Practise gratude

K**a kuna kitu unakosa majibu yake fanya hivi kujua majibu yake iulize nafsi yako niamini mimi inayo majibu na ukiyafanyia kazi majibu hayo utaona matokeo makubwa sana maishani mwako

Mfano; nitafanyeje ili kutimiza ndoto zangu?

Sikiliza kile unachotaka kukifanya halisia kwenye maisha yako

Find your passion

Acha kabisa tena kabisa kujilinganisha na mtu yoyote kwa sababu watu tumetofautiana katika talanta na vipaji, tumetofaut...
06/01/2024

Acha kabisa tena kabisa kujilinganisha na mtu yoyote kwa sababu watu tumetofautiana katika talanta na vipaji, tumetofautiana katika historia zetu za maisha, tumetofautiana katika genetics
Usipime ubora wako kwa kuangalia muonekano wa mtu mtandaoni, usipime ubora wako kwa kipimo chs mafanikio ya rafiki yako kila mtu anachangamoto zake na fursa katika mazingira yake

Acha kuonea wengine wivu, maana madhara yake ni makubwa kuliko faida zake, wivu utskufanya uchukie watu bila sababu, ugombane na watu bila sababu, ushindwe kupata fursa za kufanikiwa kwa sababu tu akiri yako inaami vitu negative maana kumuonea mtu wivu hakutabadilisha ukweli wa kwamba amekuzidi ila badala ya kumuonea mtu wivu tengeneza urafiki ili ujifunze amefaniwa vipi

Usifanye vitu kwa ajili ya maonyesho ili uonekane umetusua maisha ila kiuhalisia una maisha magumu au unajikamua sana ili kuwaonyesha watu kuwa umefanikiwa, chagua kuishi maisha binafsi usitake kila kitu kukuhusu watu wakijue maana ukifuria inakuwa rahisi sana watu kujua na kukucheka lakini ukiwa kimya hakuna atakayejua unaishije wataishia kuhisi tu yaani hawana taarifa zako rasmi

Usipende kushinda kwenye kila kitu, mara moja moja jishushe utapata vitu hata vilivyojificha ila usisahau kuwa na msimamo

UKITUMIA NJIA HII UTABADILI KABISA MAISHA YAKOSema maneno haya kila siku1. Najipenda mimi kwanza kabla ya kumpenda mwing...
05/01/2024

UKITUMIA NJIA HII UTABADILI KABISA MAISHA YAKO

Sema maneno haya kila siku

1. Najipenda mimi kwanza kabla ya kumpenda mwingine,hata k**a wengine hawatanipenda haitonifanya nijichukie

2. Najiamini na kuamini uwezo wangu, hata k**a wengine wasipoamini uwezo wangu, sitoacha kuonyesha kile nilichojaliwa.

3. Najijali mimi na kujali hisia zangu kwanza hivyo sitokubali mtu anidhalilishe ili kufurahisha nafsi yake

4. Nitasikiliza nafsi yangu kwanza kabla sijaruhusu mawazo hasi ya watu wwngine kuvuruga mfumo wangu wa maisha

5. Nitaiamini dhamira yangu ya ndani kuwa ni ya ukweli hata watu wengine wakinihukumu sitojihukumu.

6. Nitajisamehe kila ninapokosea na kuboresha mapungufu yangu sitokubali watu wengine wanihukumu

Nafsi yangu, moyo wang, akiri yangu na mwili wangu ni vya thamani sana, sitaruhusu mawazo ya watu wengine yaongoze maisha yangu.

Ninaimiliki thamani yangu na ninajua nini nataka, sitoruhusu kuteteleka kwa maneno ya watu, chuki na hukumu zao.

Je unaijua sababu yako kuumbwa au kuzaliwa?Kila mtu alipofika duniani anakuwa na mission/ kazi yake ya kufanya na unapok...
04/01/2024

Je unaijua sababu yako kuumbwa au kuzaliwa?

Kila mtu alipofika duniani anakuwa na mission/ kazi yake ya kufanya na unapokufa ndo maana tunasema kazi ameimaliza

Unawezaje kujua hii ndio mission yang au kazi niliyopangiwa kuifanya
Inaweza kutokana na

1. Angalia ni kitu gani unaweza kufanya bila kufundishwa au ukifundishwa kidogo tu unakuwa umeshaelewa na mpka unaweza kumfundisha mtu mwingine(kipaji/talent)

2. Vitu unavyopenda kufanya na unapofanya vinakupa furaha yaan hata k**a unahasira unajikuta hasira zimeshaisha( hobby)

3. Kitu ulichosomea(professional) na unapokifanya unafurahia, na unatamani kujifunza zaidi na zaidi kuhusiana na kazi yako

4. Unapata hisia gani unapopata matokeo kazi fulan kwenye kutimiza majukumu yako?

4. Unatamani kutatua tatizo gani duniani yaan k**a utapewa nafasi ya kuwasaidia watu utawasaidia katika kitu gani? Ukishapatw tatizo hiyo ndo inakuwa missiom yako ya kukamilisha

KAMWE USIOGOPE KUPOTEZA WALA KUHOFIA KESHO YAKO K**a mungu alimleta mume uliye naye sasa, kazi uliyonayo sasa, maisha ul...
02/01/2024

KAMWE USIOGOPE KUPOTEZA WALA KUHOFIA KESHO YAKO

K**a mungu alimleta mume uliye naye sasa, kazi uliyonayo sasa, maisha uliyo nayo sasa, marafiki na kila kitu, yeye alikubariki bila kumuomba au ulimuomba lakini alikubariki kwa wakati wake
Usiogope kuvipoteza, hata ukivipoteza sasa mungu atakupa vingine vizuri na vilivyo bora zaidi

"Waheshimu watu ila usiwaabudu maana wa kuabudiwa ni mungu wako tu"

"Wapende watu lakini usiwaamini kupita kiasi"

"Huwezi kubadilisha yaliyopita ila unaweza kuitengeneza leo ya dhahabu"

"Huwezi kuijua kesho yako hivyo usihofu kuhusu kesho yako kwani hilo ni fumbo na amayeweza kulifumbua ni mungu peke"

Idharau shida yako acha kujinene mabaya maana maneno huumba

Jinenenee mafanikio, jipongeze unapofanikiwa jisamehe unapokosea, chukua funzo.

unapoteleza ndipo siri ya mafanikio ilipo.

FAIDA ZA KUSEMA HAPANA KWA MTU ANAYETAKA KUFANIKIWAWatu wengi tunatatizo la kuogopa kukataa ofa mitoko nk tukihofia kuwa...
02/01/2024

FAIDA ZA KUSEMA HAPANA KWA MTU ANAYETAKA KUFANIKIWA

Watu wengi tunatatizo la kuogopa kukataa ofa mitoko nk tukihofia kuwaumiza marafiki zetu, ndugu zetu n.k lakini kuna nguvu kubwa sana katika kusema neno hapana

Kuna sababu kadhaa ambazo mtu anaweza kusema "hapana." Baadhi ya sababu ni k**a vile kutokubaliana na jambo fulani, kutokuwa tayari, kulinda mipaka, kutokuwa na uwezo, au kutotaka kufanya kitu fulani kulingana na maadili au imani za mtu, linaweza kukuletea madhara,kwa sababu unajisikia tofauti, huna nia, au haitaki kufanya kitu fulani au hata huna muda

FAIDA ZA KUSEMA "HAPANA"

1. Kulinda mipaka yako: Inakusaidia kuheshimu mipaka yako na kujisikia huru kutoa ridhaa au kukataa mambo ambayo hupendezwi nayo.

katika maslahi yako,

2. Ufanisi wa wakati: Kukataa mambo ambayo si muhimu kwako inakupa fursa wa kutumia muda wako vizuri kwa ajili ya shughuli zinazokuza malengo yako na maendeleo binafsi.

3. Inakupa uwezo wa kufanya maamuzi ya busara kwa kujua unachotaka na usichotaka.

4. Kujijengea heshima: Kusema "hapana" kwa njia inayoheshimika inaweza kuongeza heshima yako kwa kuonyesha uhakika na msimamo wako.

5. Kujali afya ya akili: Inaweza kupunguza msongo wa mawazo kwa kukubali kusema "hapana" unapohisi mzigo mkubwa.

6. Itakusaidia Kuwajibika kwa mahitaji yakozaidi : Kukataa inaweza kuwa ni njia ya kuweka kipaumbele kwa mahitaji yako mwenyewe na kujali afya yako ya kimwili na kihisia

Kusema "hapana" ni muhimu kwa sababu inaweza kuweka mipaka, kulinda mipaka yako, na kuhakikisha unafanya maamuzi ambayo ni sahihi kwako na yanakulinda. Kuweza kusema hapana kunaweza kukuwezesha kuweka kipaumbele kwenye mambo muhimu na kukataa mambo ambayo hayalingani na malengo yako au maadili yako.

Namna nzuru ya kusema hapana bila kuharibu uhusiano na watu wengine

Kuwaheshimu watu wengine wakati unakataa jambo ni muhimu. Unaweza kutumia njia nzuri ya kuelezea kukataa kwa heshima. Badala ya kutumia "hapana" moja kwa moja, unaweza kusema kitu k**a;
1. "Asante kwa kuniuliza, lakini siwezi kufanya hivyo kwa sasa."

2. Ningependa kusaidia, lakini sina uwezo wakati huu."

3. "Ninathamini sana, lakini kwa bahati mbaya siwezi kukubaliana na ombi lako."

4. "Napenda sana fursa hii, lakini haitawezekana kwangu kufanya hivyo."

Kukataa kwa heshima na kwa upole kunaweza kusaidia kuzuia kuumiza hisia za wengine wakati unapoendelea kuwa mkweli kuhusu hisia zako.

Kusema hapna sio kukosa heshima, au kutojali hivyo usiogope kusema hapana kwa boss wako, mume wako, watoto wako, rafiki zako, majirani n.k

SIRI 5 ZA KUFANIKISHA MALENGO YAKO MWAKA 2024 Watu wengi wanapanga malengo mazuri kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kufi...
01/01/2024

SIRI 5 ZA KUFANIKISHA MALENGO YAKO MWAKA 2024

Watu wengi wanapanga malengo mazuri kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kufikia ndoto zao lakini matokeo yake wanajikuta hawajatimiza hata lengo moja kwa sababu mbali mbali k**a vile

1. Kuogopa mitazamo na mawazo ya watu wengine juu ya maamuzi magumu wanayotaka kuyachukua kuhusiana na mafanikio yao

2. Kufuata ndoto za wengine baada ya kukatishwa tamaa juu ya ndoto zao

3. Kupuuzia mambo madogo madogo kusiana na ndoto zao

Siri za kufanikisha ndoto zako

1. Usiogope watu watasema nini kuhusiana na wewe maana hata wao wanasemwa sana tena vibaya, hakuna mwanadamu ambaye hasemwi hapa chini ya jua, ukiona watu wengi wanakuponda jua kuna mafanio mbeleni kwani mti wenye matunda ndo husongwa sio mwarobaini.

2. Hakuna mwanadamu ambaye hakosei, kukosea ni sehemu ya maisha yetu utakapoanguka amka tena na tena mpka kiwe halisia kile unachokiota
Kukosea+ kujisamehe+chukua funzo+ boresha makosa+ endelea na safari=mafanikio

3. Jifunze kusema hapana; usiwe mtu wa kila kitu ndio tu, unapoona mazingira yanakubana sema hapana hii itakutengeneza mipaka na kulinda heshima yako

4.fuata kile ulichokipanga, kila kitu kinafaida k**a utakifanya kwa bidii na ukakubali kujifunza kwa kila kitu kuhusiana na ndoto yako

5. Tengeneza ratiba itakayoongoza shughuli zako za siku, wiki hata mwezi na kwa hatua ndogo utakayoichukua kuhusiana na ndoto yako jipongeze na kwa kosa dogo utakalolifanya juu ya ndoto yako lirekebishe kabla halijawa kikwazo kufikia ndoto zako

Address

Mwanza

Telephone

+255783914484

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Donnie_collection posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Donnie_collection:

Share