12/05/2024
HAPPY BIRTHDAY TO ME.
-----------------------------------
Leo namba zimebadilika kwenye CV ya umri wangu. Ashukuriwe Mungu wetu kwa hii zawadi bora ya afya njema na uhai. Sio k**a kitabu cha maisha yangu kimejaza kurasa nyingi za matendo ya utakatifu, hapana.
Sio k**a mimi ni mtu special kuliko waliolala mauti kabla ya kufika umri niliofikia leo.
Huenda Mungu ameniachia pumzi hii k**a bonus tu. Akitaka nizitathmini nyendo zangu kwa kina na utulivu uliomakinika. Na nitakapogundua sehemu pana hitilafu basi nipafanyie marekebisho ya toba.
Hili hata siku nikiimaliza safari yangu chini ya jua, nilikute jina langu kwenye kitabu cha orodha ya wanadamu wema.
Napenda kushukuru mchango wa kila binadamu aliyewahi kugusa maisha yangu mpaka kufika umri huu leo. Nashukuru kwa ndugu, jamaa, na marafiki.
Mwisho, najitakia kumbukizi njema ya kuzaliwa. Mungu azidi kunikuza katika kimo, hekima, busara na maarifa. Nizidi kukua nikiyatenda mema. Yatakayompendeza Mungu na wanadamu siku zote za kuishi kwangu.