11/11/2024
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
KAMPUNI YA SHIKAMOO PARACHICHI ILIOPO NJOMBE MJINI, INAPENDA KUTAARIFU UMMA WA WATANZANIA WENYE SIFA TAJWA HAPO CHINI KUOMBA NAFASI ZA KAZI K**A ZILIVYOAINISHWA.
1.MHASIBU WA KAMPUNI NA MENEJA MASOKO -Nafasi 1
Sifa za Mwombaji
a)Awe na elimu ya kuanzia Degree ya Uhasibu na masoko kutoka Chuo chochote kinachotambulika na Serikali.
b)Awe na uzoefu usipungua miaka miwili (2) kwenye kazi ya Uhasibu na masoko.
c)Awe ni raia wa Tanzania na mwenye tabia njema.
d)Awe na umri wa kuanzia mika 30 na kuendelea
e)Awe anajua kwa ufasaha lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa kuandika na kusoma
f)Awe anajua kutumia komputa vizuri
g)Awe hakuwahi kupatikana na kutiwa hatiani kwa makosa ya jinai
2.FIELD OFFICER(AFISA UGANI) WA KAMPUNI –Nafasi 2
Sifa za Mwombaji
a)Awe na elimu ya kuanzia Diploma ya kilimo (General Agriculture) toka Chuo chochote kinachotambulika na Serikali.
b)Awe na uzoefu usiopungua miaka miwili (2) kwenye sekta ya Kilimo cha mazao na bustani.
c)Awe ni raia wa Tanzania na mwenye tabia njema
d)Awe na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea
e)Awe anajua kwa ufasaha lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa kuandika na kusoma
f)Awe anajua kutumia komputa vizuri
g)Awe hakuwahi kupatikana na kutiwa hatiani kwa makosa ya jinai.
h)Awe anauwezo wa kuandaa kalenda ya kilimo cha matunda kwa wakulima
i)Awe na uwezo wa kuwatembela wakulima na kuandaa ripoti ya kazi za wakulima
j)Awe na lugha nzuri yenye staha kwa wakulima na wadau wengine.
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI.
Maombi yawasilishwe kwa njia ya;
a)Barua pepe:- [email protected]
b)Leta barua yako kwa mkono Ofisi ya Shikamomo Parachichi, Songea Road, Majengo ya Halmashauri ya Wilaya (zamani) karibu na benki ya NMB na Tanesco Mkoa.
c)Mshahara mzuri utatolewa kwa wale watakao ajiriwa.
d)Mwisho wa kutuma maombi ni terehe 20/11/2024
NB: usaili utafanyika tarehe 22/11/2024 katika Ofisi za Kampuni, kuanzia saa tatu (3) kamili asubuhi.