Dunia Mkononi

Dunia Mkononi Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Dunia Mkononi, Business service, Nyegezi.

28/02/2023

Mambo vipi? Mchana huu tumekuandalia machache kati ya mengi tuliyokuandalia na mtandaoni utakuwa nami Elisante Kivuyo , na hizi ni baadhi ya taarifa utakazozisikia:

📍Uingereza na Umoja wa Ulaya zimetangaza "ukurasa mpya" katika uhusiano baada ya miaka mingi ya mvutano wa Brexit, huku wakikubaliana kuhusu marekebisho ya sheria za biashara huko Ireland Kaskazini

🎧Ukraine imesema kuwa vikosi vyake vipo chini ya shinikizo katika mji wa Bakhmut, ambao umeharibiwa vibaya katika jimbo la mashariki la Donetsk, ambalo Urusi imekuwa ikijaribu kulikamata kwa miezi kadhaa

✔ Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya nchi 30 zimeahidi kutoa msaada wa kiutu wa takribani dola bilioni 1.2 kwa ajili ya mamilioni ya watu wa Yemen

✍ Matokeo ya awali katika uchaguzi wa Nigeria uliofanyika mwishoni mwa wiki yanaonesha Bola Tinubu kutoka chama tawala akiwa kileleni.

:DW

27/02/2023

Habari za wakati huu, Natumai umekua na mapumziko mema ya mwisho wa juma.
Tukiwa njiani kabisa kuanza wiki mpya nipende kukusogezea karibu machache kati ya mengi tuliyokuandalia.

1. Huko nchini Kenya uamuzi uliowekwa na mahakama kuu kuwaruhusu watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kuwa na mashirika yao umepingwa vikali na viongozi wa makanisa.

2. Corneille Nangaa mwekiti wa zamani wa tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemocrasia ya Kongo mwishoni mwa wiki jana lizindua chama chake kipya cha kisiasa nchini umo ikiwa imesalia miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Disemba.

3. Huko nchini Nigeria tume ya taifa ya uchaguzi imeanza kutangaza matokeo ya uchaguzi katika majimbo kadhaa mara baada ya kukamilika kwa zoezi la uchaguzi mkuu jana jumapili, huku kukiwa na malalamiko kwa kile kinachosemekana kumekuwepo mapungufu kadhaa katika zoezi zima la uchaguzi.

4. Maafisa wa Israel na Palestina wamekubaliana kusitisha mapigano mara baada ya mazungumzo ya nadra nchini Jordan.

Hata hivyo!
Mawaziri na wakuu wa nchi zaidi ya 100 wanashiriki leo jumatatu kikao cha Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za binadamu kitakachoshughulikia maswala kadhaa, ikiwemo madai ya uhalifu wa kivita wa Urusi walioufanya nchini Ukraine.

Address

Nyegezi

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dunia Mkononi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share