06/08/2026
MWANI WA KWALE WASAFIRISHWA CHILE
Tani 43 za Mwani zimesafirishwa kutoka kwa kundi la wakulima wa Mwani wa Kibuyuni huko Lungalunga kaunti ya Kwale hadi nchi ya Chile.
Hii ni mara ya kwanza kwa wakulima hao kupata soko kubwa la kimataifa kwa zao lao.
Akizungumza wakati wa kuaga shehena hiyo, naibu gavana wa Kwale Chirema Kombo amesema serikali ya kaunti inawekeza kwenye sekta za kilimo na uchumi wa baharini ili kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wenyeji.