Radio Salaam

Radio Salaam Adding Green to your Life Official Page of Radio Salaam. Kenya's Premier News-Talk Radio station.

KACHORI :Mahitaji :Viazi 1/2 kiloKotmiri ilokatwa katwaPilipili ya kijani 1 ilokatwa ndogo ndogoChumviGaram Masala kjk 1...
14/12/2021

KACHORI :
Mahitaji :
Viazi 1/2 kilo
Kotmiri ilokatwa katwa
Pilipili ya kijani 1 ilokatwa ndogo ndogo
Chumvi
Garam Masala kjk 1 cha chai
Manjano ya unga 1/2 kjk cha chai
Sukari kjk 1 cha chai
Tangawizi na kitunguu saumu kilichopondwa kjk 1 cha chai
Mchanganyiko wa kuchomea :
Unga wa dengu gramu.
Hamira ya soda/chapa ya maandazi kidogo .
Maji
Mafuta ya kukaangia
Maelekezo :
Kosha na chemsha viazi
Vikiwiva menya na uviponde kisha weka pilipili, kotmiri, Garam Masala, sukari, tangawizi na kitunguu saumu, chumvi na kamulia ndimu kisha changanya.
Mchanganyiko wa viazi utakuwa tayari.
Tengeneza maumbo ya mipira
MCHANGANYIKO WA UNGA:
Anza kwa kuweka unga wa dengu kwenye bakuli, kisha weka hamira ya soda na chumvi , changanya vizuri kisha weka maji kidogo
Tengeneza uji mzito kisha engeza maji uwe mwepesi kiasi
Weka mafuta jikoni yakipata moto chovya kachori kwenye mchanganyiko wa unga na uzikaange mpaka ziwe na rangi nzuri
Andaa kuliwa kwa chatine.

LEO JIKONI TUNAKUANDALIAMCHUZI WA N**I WA KAMBA(WAKAVU)MAHITAJIKamba wakavu sio fresh kilo moja• N**i 2 kubwa zilizokunw...
12/12/2021

LEO JIKONI TUNAKUANDALIA
MCHUZI WA N**I WA KAMBA(WAKAVU)
MAHITAJI
Kamba wakavu sio fresh kilo moja
• N**i 2 kubwa zilizokunwa na kutolewa tui zito vikombe 2 na tui jepesi vikombe 3
• Kitunguu thomo kilochopondwa vijiko 2 vya chai
• Curry powder vijiko 2 vya chai,manjano bizari kijiko cha chai,kitunguu maji 1 kikubwa kilokatwa katwa,
• Pilipili boga 1 lilokatwakatwa
• Tomato 2 zilokatwakatwa,embe bichi 1 lilokatwakatwa
• Chumvi kiasi chako
• Mafuta uto vijiko robo kikombe na dhania msongo mmoja
NAMNA YA KUTAYARISHA
• Safisha kamba uwatoe vichwa waoshe na uwachemshe kwa muda wa dakika 7 hivi ili walainike.
• Bandika sufuria jikoni weka mafuta uto yakipata moto mimina kitunguu maji koroga hadi kiive.
• weka pilipili boga pamoja na kitunguu thomo na ukoroge uwache viive.
• weka tomato pamoja na curry powder,bizari na chumvi.
• Koroga wacha tomato ziive mimina tui jepesi pamoja na kamba koroga wacha lichemke na kuiva hadi lishikane na kupungua,sasa mimina lile tui ziito na ukoroge vizuri.
• Wacha liive kwa dakika 5 hivi..
• Epua andaa mezani kwa sima au wali
MAPISHI YA RADIO SALAAM YAMELETWA KWAKO NA MAIMUNA FARUK.

25/11/2021

Address

P. O. Box 90445
Mombasa
80100

Telephone

+254727299995

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Radio Salaam posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share