TYUN ft Taicol

TYUN ft Taicol Tsumo Agricultural Investments Company Limited

I miss my mother 😭. Inallilahi waina illahi rajiun.
28/04/2023

I miss my mother 😭. Inallilahi waina illahi rajiun.

23/09/2021

HII NDIO HOTUBA YA MWISHO YA HAYATI MUAMMAR GADDAFI....
QADAFFI ANAANZA HIVI: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu (Allah), Mungu mpaji, na mwenye rehema....
Kwa miaka takribani 40 ama ilikuwa zaidi sikumbuki. Nachokumbuka ni kuwa nilifanya kila nilichoweza kuwapa watu wangu nyumba, hospitali na shule. Na kila walipohisi njaa niliwapa chakula. Niliifanya Benghazi kutoka jangwa kuwa ardhi nzuri ya kilimo.
Nilisimama imara dhidi ya Ronald Regan (Rais wa zamani wa Marekani), alipomuua binti yangu niliyemuasili. Alikua anajaribu kuniua mimi lakini akamuua yule binti yatima masikini. Niliwasaidia kaka na dada zangu waafrika fedha kupitia AU.
Nilifanya kila nililoweza kuwafanya watu wangu waelewe maana halisi ya demokrasia; ambapo watu wa tabaka la chini niliwapa madaraka.
Lakini hawakuridhika. Hata aliyekuwa na nyumba ya vyumba kumi, nguo mpya, na fanicha nzuri, hakuridhika. Alihitaji zaidi.
Kwa jinsi walivyokuwa wabinafsi walihitaji zaidi. Hivyo wakawaambia Marekani kuwa wanataka "demokrasia" na "uhuru". Hawakujua kuwa "demokrasia" waliyoitaka ilikua ni mfumo wa unyonyaji ambapo mbwa mwenye nguvu zaidi huwala mbwa wadogo.
Walikua hawasikii wala hawaoni. Walitaka "demokrasia". Wakasahau kuwa hata Marekani hakukuwa na huduma za afya za bure, dawa bure, elimu bure na chakula cha bure. (Huduma hizi za bure zilipatikana Libya tu).
Nchini Marekani mtu masikini/fukara hana cha bure. Labda awe ombaomba au avuje jasho kuhemea.
Haikujalisha nilifanya kwa kiasi gani bado hawakuridhika. Lakini wapo waliojua mimi ni mtoto wa Gamal Abdel Nasser, mwarabu pekee halisi na kiongozi wa kiislamu tuliyewahi kuwa nae tangu enzi za Salah-al-Deen.
Wakati Nasser anapigania mfereji wa Suez kwa watu wake nami nilikua naipigania Libya kwa watu wangu. Nilikua najaribu kufuata nyayo zake ili kuwaweka watu wangu huru kutoka kwenye makucha ya wakoloni wanaotuibia.
Lakini kwa sasa niko mateka katikati ya majeshi makubwa ya dunia katika historia. Mwanangu mpendwa mwenye asili ya Afrika, Obama anataka kuniua.
Ili achukue uhuru wetu, achukue haki yetu ya huduma za bure za afya, huduma za bure za elimu, na chakula chetu; na kutuletea mfumo mpya wa kimarekani wa kuiba uitwao "Ubepari"
Lakini wote katika dunia ya tatu tunajua maana yake. Maana yake ni kuwa "washirika" wanatawala mataifa, wanatawala dunia, na watu wanaishia kuteseka.
Kwa hiyo hakuna mbadala kwangu. Lazima niwe na msimamo. Na k**a Mungu atapenda nitakufa kwa mapenzi yake.
Mapenzi yake yaliyofanya nchi yetu kuwa na ardhi yenye rutuba, chakula bora, na huduma bora za afya. Mapenzi ya Allah yaliyowezesha tukawasaidia kaka na dada zetu waafrika na waarabu waliokuwa na shida.
Sipendi kufa; lakini k**a nitakufa ili kuiokoa ardhi hii, kuokoa watu wangu, na wengine ambao ni k**a wanangu; acha nife.!
Acha sauti hii iwe agano langu kwa dunia kuwa nilisimama kupinga uvamizi wa NATO. Nilisimama kishujaa kupinga usaliti wa nchi za magharibi na nia mbaya za kikoloni. Na hapa nimesimama na ndugu zangu waafrika, kaka na dada zangu waislamu k**a ngao yangu ya matumaini.
Wakati wengine walipokuwa wanajenga majumba ya kifahari, mimi niliishi kwenye nyumba ya kawaida na kwenye mahema. Siwezi kusahau maisha yangu ya utoto kule Sirte.
Sikutapanya rasilimali za nchi yangu kipumbavu. Na k**a alivyokua Salah-al-Deen, kiongozi wetu katika uislamu, nilichukua kidogo sana kwa ajili yangu, na sehemu kubwa niliwapa wananchi.
Watu wa magharibi wameniita "kichaa", "mwendawazimu" lakini wanajua ukweli kuwa mimi si kichaa wala mwendawazimu; ila waache waendelee kudanganya. Wanajua hii ardhi ni huru na haipo kwenye himaya ya kikoloni. Huu ndio msimamo wangu na dira yangu na imekuwa wazi kwa watu wangu.
Nitapambana hadi pumzi yangu ya mwisho ili watu wangu wawe huru. Mwenyezi Mungu atusaidie tubaki waaminifu na tuwe huru.
-- Mu'uammar Qaddafi

26/04/2020

After corona challenge we will call for the interview for all those who applied for the post, for now our office is closed all jobs are done online.Thank you.

13/04/2020

Taicol head office. One vacant.

24/12/2014

Address

Tyunmovement@gmail. Com
Msambweni
P.OBOX151-80404

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TYUN ft Taicol posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to TYUN ft Taicol:

Share