15/08/2021
Kuitwa Mbwa sababu nilimwumbua- Uhalifu wangu Umi
Mfanyakazi huyo kwa mda alikua hana nia nzuri na mimi kwa sababu nilimfumania klabuni na baba watoto miaka kadhaa zilizopita, 2013. Alipokua ameletwa kupata ujuzi wa kazi ya uwakili. Kwa kuwa sikumhadaa wala kumdhuru kwa vyovyote baada ya tukio hilo lililo tokea miezi mitatu ndo nimejifungua mwanangu wa pili Jibril.Ila yeye alinipangia ikiwa tayari anaifikia faili yangu ya kortini baina yetu na mkuu wa chuo wakati huo.Jambo ambalo sikujua atajaribu kutumia kuniharibia maisha.Mwezi wa nane, Agosti mwaka huo huo wa 2013. Tumeshatoka mazishi ya babu ya watoto.Ilikua mida ya saa saba usiku wa manane maeneo ya hurlingharm Nairobi.Kwenye mkahawa inayofahamika kwa jina la Tamasha.
Kabla ya mazishi ya mzee, alikuwa akinifanyia makusudi mabaya na kunifanyia mambo mengi ya kiroho na kiimani ndo ile mimba iweze kutoka. Lakini hakuweza. Yaliokuwa yakinikumba ni baina yangu, "rafiki wa ndani wa baba watoto" na Allah(SWT).Hadi kufikia kumfumania kwenye mkahawa huo, alikua amefanya mengi makubwa kwa madogo.Na kuenda hadi jijini Tanga.Ukiniuliza najuaje?
Majivuno na madharau aliokuwa nao haikuwa ya kawaida.Sijui ni kwa vile alivyodhani sina akili nzuri tena ya kukamilisha masomo yangu chuoni Kenyatta. Yani nimekwisha haribikiwa na hasa pia eti niliharibiwa jina na sura na wandani wangu ambao pia walikuwa akimpa nguvu kipindi hicho. Alitaka niage dunia kupitia majini, hakufaulu. Akatumia jamaa na marafiki kunitegea sumu na madhambi, ikapita nusu.Akaendelea kuwatuma wachawi na washirikina kuwaroga mamangu na babangu wanifungie milango ya riziki na kunipa laana.Kwa kweli walijaribu.
Kwahiyo kuniona pale afisini kwa baba watoto alichukia kufikia kunitukana mbwa na kunifukuza nje.Nilipomjibu kwa maneno na vitendo, ndipo aliponiitia mapolisi. Mapolisi k**a wanne hivi.Walinikuta afisini nikifanya usafi
tukazungumza, tuk**alizana mmoja wao akinionya kua yule mfanyakazi binti, hana nia nzuri kabisa na mimi.Na endapo nitarudi pale, nitakua nahatarisha maisha yangu.Na akanishauri nichukuwe faili yangu nitafute wakili mwingine.
Na tena,ikiwa k**a ni baba watoto namtafuta, nikamsubirie nyumbani.
Nilimsikiza afisa wa polisi na mimi nikamweleza kuwa ningependa kuja kituoni niandikishe mashataka pia kwa jinsi yalivyotukia.Alinikubalia ila akanionesha kituo kilichokua ndani ya uwanja wa mchezo wa Moi.Wakanirudisha tena juu kwenye kituo cha upper hill ambapo kwanza walikataa kuniandikisha wakisema nimewahiwa kufika na mdada yule mfanyakazi.Tukio hapo la kusukumwa na kutukanwa ni baada ya masimu kupigwa na afisa mmoja kule ndani kuongeleshwa.
Asubuhi ilipofika, nilifanyishwa kazi ajabu baada ya kupewa kikombe cha chai na mandazi.Nikafunguliwa mashtaka (Milimani Law Court) na baadae kuandikiwa kifungo cha miaka sita jela na jaji Muthoni Nzibo. Jaji ambae mfanyakazi huyo alisifia kuwa walikuwa wanajuana kwa kuwa walisoma pamoja.
Mengi yalisemwa na wadau wengi.Sijui sisi wanadamu tumeumbwaje?
K**a si Mungu ningeharibiwa maisha hivyo tu.
?