Msheshe Rashid

Msheshe Rashid Ukurasa wa msese wa kondeni Ukurasa huu waakisi kazi za uandishi unaokuza Kiswahili

20/03/2026
23/10/2024

sisi si maua wala,hatukai mabunduki,
sisi si manyau wala,hatupendelei dhiki,
sisi si mabomu wala,zana za kuzima haki,
tupo zaidi ya kito,utu huvai jeuri.

28/03/2024

Kuwa na SUBIRA utahitaji IMANI.
Kuwa na imani utahitaji USULI WA MAMBO
Kuwa nao usuli wa mambo ndio MWANZO WA KUJITAMBUA.
Ishi maisha.

Sasa. Makusudi akiwa kizimbani mahak**ani,alitetema sana ijapo alijipigia moyo konde kila dakika za muda. Alikuwa tayari...
17/06/2023

Sasa. Makusudi akiwa kizimbani mahak**ani,alitetema sana ijapo alijipigia moyo konde kila dakika za muda. Alikuwa tayari kujitetea kwa hali na mali angaa apate kuunjoa uhuru wake kwa mara nyingine tena. Alisimama titsi akimsubiri jaji- mtu mwenye hatima yake afike.

Ubongoni mwake. Hapo kizimbani. Alijiona sawa na mangisi ijapokuwa hali zao zi tafauti sana. Walisubiria kifo ingawa mmoja wao ywafa kifo cha halali yake na mwengine ywakipokea kwa haki yake. Mmoja wao ndiye mhalifu na mwengine ni kitoweo tu.

Alijichukua kuwa kuku kwa sababu ya utawa wa shida ulioanza kumnogea utamu wa kuteseka huku jibu lake la kuijifanya msiri kati ya watu likitishia kumchubukia kwenye kipindi cha hukumu ya leo. Alikuwa kuku anayesubiri kuchinjwa kichikichi kwa hanjari ya chinjachinja! Hana bahati ya mtende.

Wingu la hisia za soni na simanzi lililovurugika,lilizidi kutambaa pale kortini pindi tu hakimu alipotia guu. Mimi,kina Chachania pamoja na wote wamjuaye Makusudi,tulktundika macho ya huruma tukisubiri kwa hofu na wahaka yatakayojiri kadamnasi yetu. Pasi na kujua la kutenda. Tungefanya nini jamani? Tumtetwe vipi rafiki na ndugu yetu? Dua tu...

"Leo hii,tulijua eti, uwongo wa sikio si ukweli wa macho! Ukweli huu ndio unaomchoma sana Makusudi. Aliyoyatenda,yalikuwa wazi kana kwamba ni doti jeusi tititi kwenye kitambaa cheupe pe cha Malkia." Haya basi.

Hakimu wa kuikata daawa hii alifaa kuwa Siti Kaliamti. Mkazi wa Kichakamkwanjuni karibu na mtaa wa Mapona Kaskazini.....
Kipi kilitokea?
Tuzidi kusoma.
Ahsanteni nyote kwa kunidhamini na kunisoma

Salamu za dhati,Wanafunzi wa darasa la Nane na gredi ya sita,msijesema hayapo yaliomshinda popo kupapia moyo kichwagoma!...
12/07/2022

Salamu za dhati,

Wanafunzi wa darasa la Nane na gredi ya sita,msijesema hayapo yaliomshinda popo kupapia moyo kichwagoma!
Mia fil mia utabiri wa maudhui
insha na soma la lugha yanaelea viziri tu kwenye visa vya kitabu hiki.Jipatie nakala,usome na ifaidi faida iso kifani.
Wasalaam
Msese wa Kondeni

MKANDA WA MSIBA.Msheshe Rashid   Mshale wa saa yangu  mkononi, iliashiria muda wa saa tatu na dakika kumi na tatu hivi. ...
02/04/2022

MKANDA WA MSIBA.
Msheshe Rashid
Mshale wa saa yangu mkononi, iliashiria muda wa saa tatu na dakika kumi na tatu hivi. Wakati huo,nilikuwa tayari stanini. Nilikuwa hapo asubuhi mbichi ya siku yenyewe. Nilitulia kwenye viti vya steji nikisubiri gari la kuabiri.
Kulingana na kukurukakara za mawio yale, matwana nyingi zilikuwa bado hazijaingia steshenini. Baada ya saa moja,basi nililolitarajia lilifikana kuwasili. Nilibeba kikoba changu na kuingia garini chapuchapu. Nikajichagulia kochi na nikawa abiria wa safari yangu iliyoanza muda mchache la dakika.
Basi nililolichagua,liling’oa nanga . Dereva tuliyemtarjia aliliendesha motokaa. Dereva tuliyemtarjia aliendesha motokaa hiyo kwa ustadi na kasi k**a chui mwindaji. Gari lilitafuna mwendo na kupasua upepo.
Safari ya hatua moja ya gurudumu ikawa masaf ya kitalifa kingi. Mwendo wetu ulizidi kuiva kwenye barabara kuu ya lami hadi pale polisi wa trafiki alipolilegezea spidi kwenye kizuizi cha barabarani. Afisa mmoja wa trafiki aliingia ndani ya basi na kuanza shughuli yake.
Alitupa macho huku na kule . Alishika hap na pale na akachunguza huyu na yule aliyekuwa abiria. Hakuna aliyemshughulikia wala kuma fikira kwa kuwa hiyo ndiyo kazi yake mlinda usalama. Akakagua kwa tathmini zake zote hadi aliponifikia nilipokaa. Nilikuwa nimezubaa zube nikisikia midundo ya ngoma fulani. “ Maisha ni fumbo “ k**a sijakosea.Mwimbaji akiwa Siti Jennifer Mgendi iwapo kumbukumbu zangu hazijatitimia mawazo mengi.
Bahati pengine haikunitunza. Polisi yule aliponifikia,alinikodolea macho. Alinitazama kijeshi kana kwamba nina uhalifu usoni. Hata hivyo sikumrudishia mtazamo wake. Nilitikisa kichwa kwenda na mdundo wa muziki ulionikosha masikioni. Kunifikia mimi ilikuwa mwanzo tu wa matembezi ya ndege mbaya.......
POLISI: (akinitazama kwa makini) Wewe, mbona hauna mkanda?
ABIRIA:Mkanda ninao afisa! (nikionyesha mshipi kiunoni.)
POLISI: (Amekasirika) Sasa unanichezea akili?
ABIRIA: (kwa mshangao) La hasha! Siwezi kabisa! Nimevaa mkanda mkubwa.
POLISI: Yaani hatuelewani. Ebu nionyeshe mkanda wako. Uko wapi?
ABIRIA:Ndio huu hapa askari. Umenikaa vyema kwenye suruali. Mshipi wa ngozi ya mamba.( sijui mbona nilinjibu vile)
POLISI: Kha,Sipendi mzaha! Ebu simama utoke nje! Haraka!
ABIRIA: Ala,nimefanya kosa gani sasam mkuu? Si mshipi ndio huu!Ama....
POLISI: Ama nini? Wewe ongea ukiwa nje kule. Sawa?
ABIRIA: Shida i wapi afande?
POLISI: kijana, kwani hujui mkanda wa usalama? Umenionesha nini? Wewe songa huku. Unaujua mkanda?
ABIRIA: Naufahamu mkubwa.
POLISI: basi! Toka nje una hatia!
ABIRIA: Jamani,basi hili halina mishipi ya usalama. Ningefunga nini?
POLISI: Eti ungefunga nini.! Wewe ni mbuzi ufungiwe kamba!
ABIRIA: Sifanani na mbuzi ama umekuwa chui?
POLISI: wewe ni mjeuri sana sio? Una pembe za ndovu? Ona pale,ile ni kamba ya ajali?
ABIRIA: Hapana. Ni mkanda wa usalama.
POLISI: Vizuri. Umeona kosa lako?
ABIRIA: Sina kosa mzee wangu.
POLISI: Nani mzee hapa? Songa twende nje.
ABIRIA: Subiri basi nishuke taratibu.
POLISI: funga mdomo ndugu yangu. Usijifanye mjuaji.
ABIRIA: lakini,wewe mwenyewe unaliona gari lenyewe. Mikanda haipo kwenye viti vyote. Hatia zangu zi wapi?
POLISI: Hatia ni zake nani? Nani amek**atwa? Ama una chako?
ABIRIA: Afande,tafadhali uwe na huruma. Tena samahani sana,mimi sina chako.m Mwenye hatia ni mwenye gari ama dereva wetu. Ebu muulize kuhusu mikanda.
POLISI: Upuzi. Ngoja ufike kortini ndipo uyaseme usemayo. Mimi sitaki hadithi za Abunuwasi. Nakutia mbaroni.
Aksari aliniingiza kwenye karadinga. Gari la polisi hilo likauma lami hadi kituoni. Huko nilisailiwa kiasi kisha nikaagizwa niingie korokoroni. Nilitulia humo selini nikisubiri hatima yangu ya uamuzi wa tuhuma zangu.
“Askari aliyeshika alidai kuwa nimekaidi kuvaa mkanda wa usalama na kumwonyesha mshipi wangu ulio kuwa ajali kubwa. Pengine nilipitilizwa mawazo. Mungu anifariji,kosa langu lipi?”
Ndivyo nilivyowazia. Mavazi hayo yaliganda pundit tu mlango Wa deli ulifunguliwa.

K**A SITUNGI SHAIRI!!Ni barua mwafulani,kwako wewe mahiri,Utungae kila fani,mjuvi na  mjasiri,Leo waja na ughani,wanena ...
30/03/2022

K**A SITUNGI SHAIRI!!
Ni barua mwafulani,kwako wewe mahiri,
Utungae kila fani,mjuvi na mjasiri,
Leo waja na ughani,wanena bila kipuri,
K**a situngi shairi,nitungayo ni upupu!
/
Awali ninakiri,usemayo ni nasaha,
Ulo mwema na mzuri,tena usionihaha,
Kando na kushika hari,wanikosea furaha,
K**a situngi shairi,nitungayo ni upupu!
/
Sina haja na kaida,k**a ndugu ywapinda,
Yule kaka yule dada,nitungapo namwinda,
Mawi aasi kudoda,k**a mkosa mkanda,
K**a situngi shairi,nitungayo ni upupu!
/
Ni hofu kwa awashwaye,asomapo ywabipu,
Vibaya tumdhaniye,yu jitu bila ya zipu,
Yu mzaha aonaye,eti nafuma majipu,
K**a situngi shairi,nitungayo ni upupu!
/
Asijifanye dubu,wa jangwa mgeni,
Asutwapo yu bubu,akitenga masitoni,
Hoja zinapodhurubu,hujitia hamsini,
K**a situngi shairi,nitungayo ni upupu!
/
K**a nakubetua,vina chenga vyakupiga,
Ndipo wajibibitua,kwa kebehi za kukoga,
Mwenzio ninabenjua,hadi tungo zajibwaga,
K**a situngi shairi,nitungayo ni upupu!
/
Nakuasia mwenzangu,mimi si k**a wao,
washairi wenye majungu,watungao bila mwao,
Usitunge mapurungu,ukidhani una bao,
K**a situngi shairi,nitungayo ni upupu!

/

Waraka ninaufunga,ninaweka wasalamu,

Iwapo nimedhulumu,mniridhie kaumu,

Mja hapiki sumu,kunywa kisha kulaumu,

K**a situngi shairi,nitungayo ni upupu!

©msese wa kondeni.

Tilte; I'M WRITING NOT.Poem collection; SCARED AND SCORCHEDPoet; Msese wa kondeni.I'M WRITING NOT..Am not writing,For in...
10/10/2021

Tilte; I'M WRITING NOT.
Poem collection; SCARED AND SCORCHED
Poet; Msese wa kondeni.

I'M WRITING NOT..

Am not writing,
For ink isn't my sting,
Like a pollen bee with fairly wings,
Why should I write,
When shadows don't foresee,
Their intentions as the see,
Why must I write,
When perceptions prostate,
Far from any reality of state,
It's my silence that keeps haunting,
I'm writing not.

Silence is in me,
Is it part of life?
Or may I deqoute this way,
it's related to our sacrifices!''
''Fate and miss-fortunes''
''Deaths and destinies'',
An old mole knows the earth's tremors well,
And so I conjuorn.
I'm writing not.

In silence,
It's eleven thirty minutes ago,
Still,stiffy, staunched and staffed by the chair,
By my wooden table,
By my solo-contained house,
With a wreckage of ancient books,
Papers, letters and shredded articles,
Maybe torn apart to my frastrations
Unfortunately it's my dislikes,
Still looking for my piety,
To throw them away like trash,
To reseek and redeem their use,
Just there,
By myself,
And my lone friend,
In crystal silence.

The silence in me,
I'm re-thinking, re-setting,
Re-adusting to re-focus on no mirror,
I don't want shadows that haunt me by looks,
I'm bored to such extent.
All alone with my solace intent,
Still in silence,
Dusk,that was lurking,has fade into the night,
My sleep as well frozen like a piece of ice,
Visitors from my norm encircle me,
Feelings and emotions,senses and thoughts,
Quire is their trait,
Doubtlessness in character,
Of which today turn me an orator,
Of my own ink,
I write not.

The silence in me,
Is it not for foolishness?
The silent movements of a tiger,
Aiming and targeting, attentively,
Or is it a calculation for accuracy?

The silence in me,
Reflections of hidden voices,
Voices of dear choices,
Choices have degnity,
Or may I requote myself,
Silence is a true friend,
who never betrays,
I'm writing not.

© All Copyright preserved.
©®Msese wa kondeni.

AUGUAYE HUANGALIWA.//Tatizo hutatuliwa,tata likatatuka,Riziki hujuhudiwa,mlo ukatarazika,Na baya huambuliwa,mbali likaji...
16/08/2021

AUGUAYE HUANGALIWA.
//
Tatizo hutatuliwa,tata likatatuka,
Riziki hujuhudiwa,mlo ukatarazika,
Na baya huambuliwa,mbali likajizika,
Dama ndivyo hivyo huwa,muugua hwangaliwa.
//
Ni yakini maridhawa,ganga ganga kuganguka,
Muwele anouguwa,kutunzwa na kutunzika,
Ili nafuu ya kuwa,impate kwa haraka,
Dama ndivyo hivyo huwa,muugua hwangaliwa.
//
Auguaye suluhuwa,anayo tiba tibika,
Si Dawa tu kubuhuwa,na pia kushufahika,
Mathali gahugahu wa,gehugehu akiruka,
Dama ndivyo hivyo huwa,muugua hwangaliwa.
//
Kuseneka kukipowa,Siha na hutatarika,
Ukajyona Umetowa,zito lotasawarika,
Mwenye shida hutasuwa,maono kusaidika,
Dama ndivyo hivyo huwa, muugua hwangaliwa.
//
Khamsani natongowa,tongoo kutafitika,
Vina vinakoma vya Wa,vinasita pia vya Ka,
Takilifu ikikutuwa,kite si dhema kuwika,
Dama ndivyo hivyo huwa,muugua hwangaliwa.
©msese wa kondeni.

Address

Bahati
Nairobi

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00

Telephone

+254719544381

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Msheshe Rashid posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Msheshe Rashid:

Share