25/01/2021
Bunge jipya Uganda: Akina nani wanaunda na ipi ni nguvu na udhaifu wake?
Ezekiel Kamwaga
Mchambuzi
Saa 3 zilizopita
Wabunge kutoka NRM watakuwa wengi na wanatoka katika karibu maeneo yote ya Uganda.
Uganda imemaliza uchaguzi wake wa Januari 14 mwaka huu na ingawa bado kuna sintofahamu kuhusu matokeo yake - walau matokeo rasmi yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Uganda yametoa picha ya hali ya kisiasa ya taifa hilo kuanzia sasa hadi utakapokuja uchaguzi mwingine miaka mitano ijayo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Uganda (EC), Jaji Simon Byabak**a, katika uchaguzi huo, chama tawala cha National Resistance Movement (NRM) kimepata kura 5,851 037 sawa na asilimia 58.64 ya kura zote zilizopigwa huku mshindani wake wa karibu, Robert Kyagulanyi - maarufu kwa jina la Bobi Wine akipata kura 3,475 298 sawa na asilimia 34.83 ya kura zote zilizopigwa.
Pamoja na mambo mengine, uchaguzi huu umekigeuza chama kipya cha Nationa; Unity (NUP) kilichoanzishwa Julai mwaka jana kuwa chama kikuu cha upinzani nchini Uganda, kikipiku chama cha Forum for Democratic Change (FDC) kilichokuwa chama kikuu cha upinzani nchini humo kwa zaidi ya miaka 20 sasa.
Katika uchaguzi wa mwaka huu, FDC kimepata chini ya asilimia tano ya kura zote zilizopigwa huku kikizidiwa na NUP hadi katika viti vya ubunge. Wakati NRM ikitangazwa kupata viti 316 vya Bunge, NUP kimepata viti 61 kwenye uchaguzi huo.
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2016, mgombea wa FDC, Dk. Kizza Besigye, alipata asilimia 35.4 ya kura zote zilizopigwa huku NRM ya Museveni ikipata asilimia 60.
Nini kimetokea katika uchaguzi huu?
Ni muhimu kwanza kupata muktadha wa uchaguzi wenyewe kabla ya kuingia kwenye siasa za bungeni. Katika uchaguzi huu, NUP ya Bobi Wine imepata ushindi wa takribani asilimia 72 dhidi ya chama tawala cha NRM kinachoongozwa na Rais Yoweri Museveni.
Museveni na chama chake wamedai kwamba kushindwa kwao na Wine katika eneo hilo kumesababisha na siasa za ukabila kwa sababu Wine anatoka katika kabila la Baganda lenye makazi yake katikati ya nchi hiyo.
Hata hivyo, nje ya katikati ya Uganda, Wine amepata viti viwili tu. Wakati huohuo, FDC imepata viti 33 lakini tofauti na NUP, chenyewe kimepata viti katika maeneo tofauti ya nchi hiyo. Hii maana yake ni kwamba chama hicho kimesambaa katika maeneo mengi ya taifa hilo kuliko kile cha Bobi Wine.
Kitendo cha NRM na FDC kushindwa vibaya katika eneo la katikati ya Uganda ni pigo kubwa kwa vyama hivyo vikubwa - hasa kwa Museveni ambaye kwa sababu alianzishia vita yake ya msituni akitokea katikati ya Uganda, alikuwa akiita eneo hilo "Makkah ya NRM". Kushindwa huku kutakuwa kumemuuma Museveni.
Kihistoria, kwa mujibu wa mwandishi maarufu wa Uganda, Andrew Mwenda, Museveni amekuwa akifanya kampeni za kuongoza nchi hiyo kwa kanuni rahisi tu; kwa kuatamia kura za atokako yeye (Magharibi mwa Uganda), kuishika Uganda kati na kutafuta kura za makabila ya Mashariki
Hakujali sana k**a angeshindwa Kaskazini.
Kwa mara ya kwanza katika mfumo wa vyama vingi vya Uganda, Bunge la nchi hiyo - safari hii likifahamika k**a Bunge la 11, sasa litakuwa chini ya Kambi ya Upinzani inayoongozwa na chama kipya cha upinzani cha NUP. Bobi Wine hakuwania ubunge na hivyo yeye hatakuwa bungeni kuongoza mashambulizi.
Kuhusu Bunge la Uganda
Bunge la Uganda lina jumla ya wabunge 529. Wabunge hao wanatokana na majimbo 353 ya nchi nzima, wabunge wa viti maalumu wanawake 146, wabunge watano kutoka kundi la vijana, wabunge watano kutoka vyama vya wafanyakazi, wengine watano wanaoingia katika kundi la wazee huku wanajeshi kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF) wakiwekewa wamepewa nafasi 10 za kuingia bungeni.
Uchaguzi huu umeipa NRM nafasi ya kutamba bungeni, ikiwa imesambaratisha wapinzani wake katika mikoa ya Kaskazini mwa taifa hilo.
Hilo ni eneo ambalo kwa muda mrefu limetawaliwa na watu wa vita, na wananchi wake - kwa kura nyingi walizompa Museveni mara hii, inaonekana ukosefu wa amani kwao unahitaji chama tawala kibaki madarakani kuwalinda.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni
CHANZO CHA PICHA,OTHER
Aliyekuwa Mnadhimu wa Upinzani Bungeni, Ibrahim Nganda, wa FDC ni mmoja wa wabunge wachache wa FDC walilioshinda uchaguzi wao katika eneo la katikati ya Uganda na kwa matokeo ya uchaguzi huu, inaonekana itabidi aachie ngazi. NUP sasa itakuwa na kazi kubwa ya kutengeneza kambi hiyo.
Kwa sababu ya wingi wa wabunge wake kutoka katika eneo moja la Uganda, hakuna shaka kwamba ili kuwe Kambi Rasmi ya Upinzani inayowakalisha Waganda wote; ni muhimu kwa viongozi wa NUP kufikiria kuhusu muungano huo.
Katika Bunge la 10, nafasi ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni ilikuwa ikishikwa na mwanamama, Betty Aol Ochan aliyekuwa Mbunge kutoka Wilaya ya Gulu nchini Uganda.
Gazeti la Daily Monitor la Uganda limebashiri kwamba wabunge wawili; Medard Lubega Ssegoona wa Busiro Mashariki na Mathias Mpuugwa wa Nyendo- Mukungwe, wote wanaitaka nafasi hiyo lakini chama kitaamua nani wa kumpa.
Jambo hili linaweza kuonekana dogo kwa wengi lakini uzoefu unaonyesha kwamba chaguzi za namna hii za kuchagua watu wa vyeo vikubwa miongoni mwa wanasiasa, huwa ndiyo mwanzo wa migogoro inayotokea.
Kwa hiyo, ni muhimu sana kwa Bobi Wine na wenzake kukaa chini na kuangalia ni nani atafaa kuwa kiongozi wa upinzani bungeni.
Ana bahati pia kwamba wabunge wazoefu wa upinzani k**a Nathan Nandala Mafabi, wameshinda uchaguzi na wanaweza kuwa msaada mkubwa kwa wabunge wapya watakaokuwa wamepewa majina ya kujiunga nayo.
Vyama vingine mashuhuri k**a DP cha Norbert Mao na TNT cha Jenera;i Gregory Mugisha Muntu vimeambulia patupu katika uchaguzi huo wa aina yake.
Nguvu na udhaifu wa Bunge la 11 la Uganda
Wabunge kutoka NRM watakuwa wengi na wanatoka katika karibu maeneo yote ya Uganda.
K**a Bobi Wine atataka kuwa na maisha marefu katika siasa za Uganda, hatakuwa na ujanja zaidi ya kukubali kutengeneza kambi ya pamoja na wenzake kutoka vyama tofauti - hasahasa kutoka FDC.
Katika muktadha huo, nguvu kubwa ya Bunge la 12 itakuwa kuhusu ni kwa namna gani wabunge hao watashirikiana katika mambo ya kitaifa.
Kurejea bungeni kwa wanasiasa ambao wengine walikuwa ndani ya chombo hicho baada ya vita ya msituni iliyomwingiza madarakani Museveni kwa mara ya kwanza mwaka 1986 ni panga lenye makali pande zote mbili.
Wabunge hao ni k**a Kahinda Otafiire, Jim Muhwezi, Rebecca Kadaga na wengineo wa aina hiyo. Umuhimu wao ni kwamba Bunge litakuwa na watu wenye uwezo wa kufanya mambo na kumbukumbu ya mat
Upande mwingine, wapo wanaoamini kuwa kundi hili la siasa wanasiasa wakongwe ni mojawapo ya sababu za kwanini Uganda iko hapa ilipo sasa kiuchumi. Hawa, kwa kundi mawazo ya kundi hilo, ndiyo wanafaidi matunda ya uhuru wao.
Kwa vyovyote vile, udhaifu mkubwa kuliko wote wa wabunge wa NUP ni kwamba wanatoka katika eneo moja pekee la Uganda - katikati.
Namna pekee ya kuondoa dhana hiyo na kudhibiti propaganda za ukabila dhidi yake kuenea kuanzia sasa, ni lazima Bobi Wine na wenzake watafute namna bora ya kuonesha kwamba yeye na chama hawako kwa kwa ajili ya kutetea maslahi ya watu kutoka sehemu moja.
Ndiyo changamoto kubwa ya Bunge jipya la Uganda.