Chasha Poultry Farm

Chasha Poultry Farm We are Dealing with Hatching, Selling Day one to Monthly old chicks, Training farmers on poultry keeping, selling eggs incubators

20/07/2015
Hii ni Kutoka KARI- Kenya, Ni moja ya chombo kizuri kwa kulia kuku na unaweza tengeneza mwenyewe nyumbani kwako na fundi...
15/06/2015

Hii ni Kutoka KARI- Kenya, Ni moja ya chombo kizuri kwa kulia kuku na unaweza tengeneza mwenyewe nyumbani kwako na fundi wako

Moja ya Dalili kubwa kabiza za Ugonjwa wa Kideri
15/06/2015

Moja ya Dalili kubwa kabiza za Ugonjwa wa Kideri

kuroiler c**k and hen
14/06/2015

kuroiler c**k and hen

HomeworkJinsi ya kutambua k**a kuku anataga au la
10/06/2015

Homework

Jinsi ya kutambua k**a kuku anataga au la

KWA NINI KUKU HULA MAYAI?Kuku hula mayai kwa sababu nyingi sana ambazo zingine zu zote zinaweza kuzuilika,1. Tabia yao t...
03/06/2015

KWA NINI KUKU HULA MAYAI?

Kuku hula mayai kwa sababu nyingi sana ambazo zingine zu zote zinaweza kuzuilika,

1. Tabia yao tu- Hapa utakuta ndo uzao wao wanatabia ya kula mayai hivyo kuku hufanya muendelezo wa kula mayai,

2. Kuto kupata chakula cha kutosha- Hii ni moja ya sababu kubwa kabisa inayo pelekea kuku kula mayai.

3. Kukosa madini joto- Hii inaweza kuwa ndo sababu kuu ya kwa nini kuku wanakula mayai, kuku wakikosa madini joto ni lazima wale mayai na hata kulana wao wenyewe, na jua kwamba kwenye yai kuku huwa anatafuta lile ganda la juu pekee sema anapo donoa na kulipasua yai hujukuta anakula na ute na kiini ila yeye lengo lake hasa ni ganda la juu

4. Kuku kutagia sehemu nyeupe sana yenye mwanga mkari hupelekea kuku kula mayai.

5. Mayai kukaa muda mrefu bila kukusanywa baada ya kutaga- Hapa ni kwamba mayai yanapo kaa muda bila kukusanywa na k**a yapo sehemu ya wazi sana hupelekea kuku waanze kutest na some time kusangaa nini hiki cheupe? katika kushangaa ni kitu gani hiki cheupe cha mviringo hujikuta wanatest kudonoa na matokea yake ni kupasua yai.

FANYA HIVI.

1. Chakula cha kutosha ni muhimu sana, ili kuwafanya wasitake kula mayai ili kushiba.

2. Mayi yakusanywe mara tu anapo taga na usiyaache muda mrefu bandani.

3. Sehemu ya kuragia iwe na giza la kutosha ili kufanya kuku ashindwe kuona yai alilo taga.

4. Madini joto ni muhimu sana.

5. Kuku wenye tabia za kula mayai unaweza chinja au kuuza.

ANGALIZO

Some time unaweza zania kuku wanakula mayai kumbe sio wao na wanasingiziwa tu, unaweza kuta ni vijana wa kazi/wafanya kazi wanakula au kwenda kuuza, paka, mbwa na hata nyoka so check out

02/06/2015

We’ll be sussing out the health risks of sugar overdose this Sunday. And, we look at Grethe Koen’s sugar scale, which has some surprising results...

Production ya Mayai kushuka kipindi cha baridi.Kuna sababu kuu mbili zinazo pelekea utagaji ushuke kipindi hiki cha bari...
02/06/2015

Production ya Mayai kushuka kipindi cha baridi.

Kuna sababu kuu mbili zinazo pelekea utagaji ushuke kipindi hiki cha baridi na hii ni kwa watu walioko kwenye mikoa yenye baridi sana k**a vile, Arusha, Morogoro, Mbeya, Iringa, Kilimanjaro, Manyara na hata kanda ya kati.

SABABU
1. Kipindi cha Baridi kuku hutumia chakula kingi kwa ajili ya kujikinga na Baridi,na kiasi kidogo huenda kwenye kutengeneza mazingira ya kutaga.Hivyo production kushuka

2. Giza, kipindi cha baridi mara nyingi huwa hakuna jua kitendo ambacho kwa kuku hukitafasiri k**a usiku, na kuku ili aweze kutaga anahitaji mwanga wa kutosha,

Hizo ndo sababu kuu ambazo hupelekea utagaji kushuka.

CHA KUFANYA

1. Kuongeza kiwango cha chakula cha kuwapatia kuku wako hasa wa mayai, kipindi hiki ni lazima uongeze kiwango hivyo kitawasaidia sana ku maintain utagaji.

2. Wawekee taa za joto au wawashie jiko.

3. Kwa ishu ya Giza wawekee taa za kutosha za mwanga ambazo zitawasaidia katika kutengeneza yai.

22/05/2015

MCHANGO WA FAMILIA KATIKA PROJECT ZAKO.

Familia ina mchango mkubwa sana katika kufanikisha mradi unao uiendesha uwe ni kilimo, ufugaji au hata biashara za kawaida, mafanikio hapa hutegemea familia.

Familia inategemewa katika maeneo kadhaa k**a vile

1. Kutoa sapoti ya fedha

2. Kutoa sapoti ya man power

3. Kutoa saport ya kukutia moyo wewe initiator wa Idea

4. Kuja kuwa wasimamizin wa mradi wapo endapo, utakuwa uko mbali, unaumwa au hata kufariki dunia.

WANAO TAKIWA KUTOA SAPOTI.

MAMA/BABA

Mara nyingi tumekuwa tunaendesha miradi pekee yetu, either utakuta ni Mama ana mradi wake wa Ng'ombe au kuku au mbuzi au Nguruwe au hata shamba na Baba hana time na wala hana hoby hizo kabisa, yaani mama hoby yake ni kufuga mzee hobby yake ni magari, na upande wa pili wa hivyo hivyo.
Mke/mme ni lazima awe bega kwa bega na project ya mwenzake na kuhakikisha kwamba project inasonga mbele,
Kwa staili hii mafanikio huwa ni vigumu sana kupatikana.

WATOTO
Watoto ni lazima wawe wanatoa sapoti ya kutosha hasa sapoti ya man power,
Unaweza kuta mzee ni mkulima au ni mfugaji mzuri sana wa Nguruwe au kuku au Ng'ombe na watoto ndo kabisa hawana habari kwanza hata kuona kinyesi cha ng'ombe kwao ni kinyaa cha hari ya juu.

Unaamka asubuhi kuingia kwenye banda la Ng'ombe au kuku watoto wanaachwa wamelala au wako bise kucheza game,

Unaenda shambani, asubuhi huku nyuma unaacha watoto wakiwa wamelala au wanacheza,

Ni makosa makubwa sana yanafanyika ukizania unawapenda watoto wako,

NI LAZIMA WATOTO WAKO WAJUE HAYA.

1. Wajue kuendesha shughuri zako ziwe ni za kilimo au ufugaji au duka,

2. Wajue madawa yote unayo tumia kutibu

3. Wajue wateja wako/marafiki wa mradi wako

4. Ukienda shamba au bandani lazima wawepo hata kwa nusu saa kuona mambo yanavyo enda.

5. Lazima uwape hamasa kwamba watakapo maliza masomo yao basi wanatakiwa kuja kuendeleza kile unacho fanya wewe

MADHARA YA KUKOMAA NA PROJECT PEKE YAKO NI K**A HAYA.

1. Endapo una project yako ya kuku/mbuzi/shamba/hoteli/ng'ombe au nguruwe na ukaugua muda mrefu na hapo nyumbani hakuna anaye jua hata yai linaokotwa vipi, itakuwa ni shida sana na matokea yake ni mradi wako kufa

2. Ukiwa hauko duniani na mradi wako utakufuata huko huko since walio bakia hakuna anaye jua chochote kile, ndo ile huwa unaona mzee kafa na baada ya mwezi biashara nayo haipo tena hii ni kwa sababu hakuna sapoti alio kuwa anapata toka kwa familia yake yeye alikuwa na spiri ya biashara huku famuilia ikiwa na hoby nyingine kabisa.

20/05/2015

NINI CHA KUFANYA UNAPO KOSA SOKO LA UHAKIKA LA PRODUCT ZAKO? AU MADALALI WANAFAIDI ZAIDI YAKO? Kwa Product k**a vile:
1. Nguruwe
2. kuku
3.Mbuzi
4. Maziwa
5. Na mazao mengine

1. Kwa Maziwa- Hapa anza kuwaza kusindika ,maziwa yako mwenyewe endapo wateja wanazingua au faida ni ndogo, sindika na anza kuuza mtaani kwako hata anza na majirani zako kwanza.

2. Kuku-Hapa unaweza either sindika au ukaanzisha mgahawa wako mwenyewe special kwa ajili ya kuuza kuku wako wanao toka shamba, k**a mtaji unaruhusu basi unaanzisha mgahawa wako na mgahawa wako utadili na kuku pekee na kuku watatoka shambani kwako.

Kwa Mayi- Hapa unaweza fikiria kupack na vile vile kuuza kwenye mgahawa wako.

3. Kwa mbuzi wako-The same unaweza fungua mgahwa special wa kuuza nyama ya mbuzi kwa mapishi ya kila aina.
4.Kwa mazao ya Bustani nayo badala ya kuhanagaishwa na madalali- fungua mgahawa wako au duka la kuuza product zako ambapo kunakuwa na vifaa vya kuzihifadhi kwa muda kadhaa ili zisharibike.
Njia hizi zinaweza kuwa suluhisho pia la Madalali ambao wananufaika zaidi.
Utakapo kuwa ma either Mgahawa wako wa kuuza nyama ya kuku, mayai, mbuzi, maziwa na mboga na matunda kutoka shambani kwako utakuwa kwanza umeongeza thamani kwa kiwango kikubwa sana na kwako swala la soko halitakuwa tatizo tena.

Address

Arusha

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Chasha Poultry Farm posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share