Agronomist Brighton Dismas

Agronomist Brighton Dismas Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Agronomist Brighton Dismas, P O BOX 10954, Arusha.

USHAURI WA KILIMO CHA KIBIASHARA (AGRIBUSINESS CONSULTANCY), PEMBEJEO ZA KILIMO (AGRICULTURAL INPUTS),UFUNGAJI WA MIFUMO YA UMWAGILIAJI (DRIP IRRIGATION)
VITALU VYA MAZAO k**a NYANYA ,PILIPILI , HUDUMA ZA KUTEMBELEA MASHAMBA.

MBEGU ZA MPUNGA, SUMU ZA WADUDU, UKUNGU, MBOLEA 0745388010
29/08/2022

MBEGU ZA MPUNGA, SUMU ZA WADUDU, UKUNGU, MBOLEA 0745388010

NAMNA YA KUSIA MBEGU KWENYE TREI ZA KUOTESHEA . Germination Trays.Kila baada ya kujaza udongo maalum COCOS au Peatmoss h...
24/08/2022

NAMNA YA KUSIA MBEGU KWENYE TREI ZA KUOTESHEA . Germination Trays.

Kila baada ya kujaza udongo maalum COCOS au Peatmoss hizi zinauwezo mkubwa wa kufanya MAJI na VIRUTUBISHO visiweze kupotea ukilinganisha na UDONGO .
katika trei moja, weka punje ya mbegu kwenye kila tundu la trei, na tumia kijiti chembamba kiasi kusukumiza mbegu kuzama kwenye udongo ndani ya tundu lakini mbegu ISIZAME SANA, wala isifike KATIKATI ya tundu bali juu kiasi na iwe imefunikwa na udongo.
Fanya hivyo kwa trei zote mpaka utakapomaliza kusia mbegu zako, tayari kwa ajili ya kukuza miche.

ENEO LA KUKUZIA MBEGU KWA SIKU 2 hadi 7

Andaa kichanja kitakachotosheleza kuweka na kupanga trei zote zenye mbegu mahali penye kivuli. Unaweza hata kuweka ndani chini ya uvungu, lakini kuwe ni sehemu penye utulivu na giza.
K**a ni nje, chukua nailoni nyeusi kisha tandaza juu ya kichanja na panga trei zote juu. (Hakikisha kabla ya kupanga trei juu ya kichanja, umenyunyizia maji kidogo kulowanisha udongo kwa kutumia bomba la kupiga dawa au spray pump).

K**a trei ni nyingi, weka trei kwa kupandanisha juu ya zingine, huku ukipishanisha kuhakikisha hakuna trei inayokaa juu ya nyingine kwa mwelekeo mmoja kwani vitobo vikipandana mbegu itashindwa kuota kwa kukosa sehemu ya kutokea.
Baada ya kupanga trei zote, chukua nailoni nyingine nyeusi kisha funika trei zote vizuri tayari kwa kusubiri mbegu ichipue.

NINI CHA KUFANYA BAADA YA KUFUNIKA TREI
Katika siku ya pili jioni, anza kuangalia mbegu k**a imeanza kuchipua kwani kuna baadhi ya mbegu huchipua haraka sana. Fanya hivyo kila siku asubuhi na jioni. Ukishaona mbegu moja tu imejitokeza, ondoa nailoni na hamishia trei zote kupeleka kwenye eneo la kukuzia miche.

ENEO LA KUKUZIA MICHE LIKOJE???
Eneo la kukuzia miche linatakiwa liwe ni kichanja ambacho kwa chini hakijazibwa bali kina viupenyo. Unaweza kutumia miti migumu k**a nguzo (lakini zisiwe zile za kuliwa sana mchwa) na ukapigia mianzi kutengeneza kichanja.
Weka pia miti kidogo kwa juu kwa kuzikunja kutoa upande wa kushoto kwenda kulia ili ikusaidie kufunika kwa kuweka nailoni juu ya miche yako hasa kipindi cha mvua kubwa kwani mvua huweza kufanya miche kuvunjika na hata udongo kudondoka kwenye matundu na mwisho miche kufa.

NINI CHA KUFANYA KWENYE KICHANJA CHA KUKUZIA MICHE???
Baada ya mbegu kuanza kuchomoza, hamisha na panga trei zako zote kwenye eneo la kukuzia miche kisha anza kunyunyizia maji kwa kutumia spray pump kila siku mchana. (Usinyunyizie maji asubuhi wala jioni ili kukwepa barafu na pia kushamirisha kuwepo kwa wadudu).

Hakikisha wakati wa kunyunyiza maji, huruhusu kuingia maji mengi kwani kutafanya udongo kupotea kwa kudondoshwa na maji kidogo kidogo na mwisho udongo wote kuisha na hatimaye mbegu kunyauka na kufa.

Mara unapoona kuna magugu yanajitokeza, ondoa mapema yakiwa bado madogo sana kwa sababu zikikomaa ni ngumu kuondoa. Endelea kutunza bustani yako kwa muda ambao utaona miche iko tayari kupelekwa shambani, kulingana na aina ya zao ulilosia.

FAIDA YA KUSIA KWA KUTUMIA TREI..

+Njia hii ni rahisi sana kwa mkulima kutunza miche yake bila usumbufu.
+Miche inayokuzwa kwenye trei, mara ni vigumu sana kushambuliwa na wadudu pamoja na magonjwa kutokana na kuwa udongo uliotumika umetibiwa..COCOPEAT /PEATMOSS
+ Mkulima anakuwa na uhakika wa kiasi cha miche ama idadi ya miche aliyonayo kwa ajili ya kupeleka shambani kwake. Hii ni kutokana na kuwa kila trei linakuwa na matundu idadi fulani.
+Miche inayokuzwa kwenye trei haiwezi kufa na kila mbegu huota ilimradi tu mbegu iliyowekwa ilikuwa na kiini.
+Miche inayokuzwa kwenye trei, hushika chini haraka na kukua kwa haraka sana shambani kwani wakati wa kuhamisha, mizizi haikatwi na miche huhamishwa au kuoteshwa pamoja na udongo wake wa kutoka kitaluni.
+Halikadhalika, miche inayokuzwa kwenye trei, mara nyingi haishambuliwi na magonjwa na wadudu kwa haraka baada ya kuhamishiwa shambani kwani kupitia kwenye udongo ule huwa na ukinzani mzuri.

Si mimea yote yanayoweza kusiwa kwenye trei, isipokuwa ni baadhi ya mazao ya bustani k**a vile nyanya, pilipili hoho, kabichi, matango KWA MAHITAJI YA TREY NA UDONGO WA KUPANDIA 0745388010/0624653243 Agronomist Brighton Dismas

24/08/2022
Mbegu Bora za MPUNGA KWA KANDA ZOTE TANZANIA pamoja na ushauri wa namna bora ya ukulima wa mpunga , pembejeo 0745388010 ...
26/09/2021

Mbegu Bora za MPUNGA KWA KANDA ZOTE TANZANIA
pamoja na ushauri wa namna bora ya ukulima wa mpunga , pembejeo 0745388010 Agronomist Brighton Dismas

Huduma na ushauri kuhusu kilimo chenye tijambegu bora, madawa ya wadudu na magonjwa, mbolea na virutubishi vingine vya m...
21/12/2017

Huduma na ushauri kuhusu kilimo chenye tija
mbegu bora, madawa ya wadudu na magonjwa, mbolea na virutubishi vingine vya mimea .

*****unaweza kukabiliana na magugu hasahasa kwenye mpunga bila kung'olea inawezekana kwa gharama ndogo********KARIBU

Wasiliana na Brighton Dismas. Watsap 0743788720 call /sms 0745388010 email [email protected]

Leo tunaanza na hii

(seed treatment phosphate fertilizer)
Mbolea inayotumika kutibu mbegu zlizohifadhiwa shamban(farm saved Local) au mbegu za grade(hybrid seed)

*Inasaidia mimea kuota mapema na kunawir vyema
*nzuri kwa mimea yote inayopandwa kupitia mbegu
*ni rahis kutumia na inafanya mbegu kuvumilia ukame .
*inaongeza uzalishaji Kwa asilimia 30(30%) K**a ulikua unapata gunia 10 kabla ukitumia utapata 13(prooved) katika eneo hilohilo
*pakiti moja inatosha kuchanganya kilo 2 za mbegu
*bei rejareja n Tsh 5000/= jumla Tsh4000/=


Mfano mahindi ekari moja inatosha mbegu kilo 8 ukitumia utatumia pakiti 4tu ambazo ni Tsh 20000/= hapo utakua umepanda mbegu zako zkiwa zmechanganywa na chumvi ambayo inavirutubisho vyote muhimu kwa ukuaji wa mmea. (26g phosphate,17g potash kwenye 50g groplus )

Wakati huohuo K**a utatumia mbolea nyingine za kupandia K**a DAP itabid utumie kg 50 ambayo s chini ya Tsh 40000/=

KARIBU SANA KULIMA SIO USHAMBA
#

Address

P O BOX 10954
Arusha
ARUSHA

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Agronomist Brighton Dismas posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share