05/06/2020
Jinsi gani hackers wanaiba taarifa kwenye http/https pages
Japo kuwa https no secure sana
Kwa wale mnaopenda kutumia
Wi-Fi ya bure au internet ya bure kwenye ofisi au sehemu mbalimbali mko hatarini sana kuibiwa taarifa zenu
Twende sawa.
Kuna hivi vitu viwili SSLSTRIP na DSNIFF hizi ni tools ambazo Hacker hutumia kulazimisha router badala ya kupelekea traffic (maulizo) kwa mhusika bali maulizo yaanzie kwake halafu mlengwa atapata maulizo kutoka kwa hacker kwa kupitia port number 8080 inayotumiwa na SSLSTRIP
Jinsi inavyofanya kazi
Mfano umeulizia https://google.com
Hii page inatumia https, router inapokea hii page na haiwezi kukuletea majibu wewe uliyeomba moja kwa moja bali itaanzia kwa hacker kwa kuwa imekuwa redirected huko then kutumia SSLSTRIP hii tool inauwezo wa kubadili kutoka https kwenda http://google.com
Kwa hiyo wewe utapokea page uliyokuwa kwenye computer ya hacker na ukiandika chochote kwenye hiyo page ( personal informations) yeye anaona vyote in a clear format kupitia SSLSTRIP LOG FILE
HTTP
Hii ni protocal ambayo haifichi taarifa zako, taarifa kati ya client (wewe) na server zinakuwa wazi inaweka bayana kila unachofanya kwenye website husika kwa kuwa haitumii algorithms za kuficha (encrypt) taarifa (data) mbalimbali za mitandaoni.
MWENYE SWALI AULIZE