05/04/2022
~~~YOTE ALIMALIZA~~~
Kuna wakati tunajipinga wenyewe:
Sio sawa kuendelea kutafakarishwa habari za hari zetu za kale wakati tayari sisi ni viumbe vipya, wewe si tena yule wa zamani wewe ni kiumbe kipya hari yako ya zamani ilishapita na yule wewe wa zamani, imeandikwa ukiwa katika Kristo wewe ni kiumbe kipyaa! 2wakorintho 5:17
Mtu asije kukuletea habari za yule wewe wa zamani, Kristo alipoingia katika maisha yako alibadili hari yako ile ya zamani, wew3 sio katika Adamu tena wewe ni katika Kristo, wewe hauko tena chini ya laana, hauko tena chini ya kifungo chochote, hauko chini ya sheria ya dhambi, umeoshwa wewe ni safi ndivyo Mungu anavyokuona kwa maana gharama ilishalipwa wewe umegharamiwa acha kuishi maisha ya kinyonge ishi maisha ya washindi.
Usiendelee kumtafakari yule wewe wa zamani, utu wako wa kale ulishapita, tafakari habari za ule msamaha, tafakari habari za ule ushindi, Yesu akushinda kwa ajili yake mwenyewe alishinda kwa ajili yako, tafari habari za ile Neema tuliyopewa bure.
Kumbuka unachokitafakari sana ndicho kinachotokea, imeandikwa aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo, ukitafakari laana, laana zitakuandama, ukitafakari vifungo na dhambi zako vitaendelea kukuandama, usiruhusu kutafakarishwa au kutafakari mwenyewe habari za kale. Nasema usithubutu. Usijiroge mwenyewe.
yoote alimaliza pale Calvary huo wimbo sio maigizo ni halisi acha kujichanganya. Usipoelewa utapigwa sana danadana na wapigaji wa mjini maana wako kila kona.