Mbena Poulry Consultancy

Mbena Poulry Consultancy Tunajihusisha na uelimishaji juu ya uendeshaji wa miradi ya KUKU. KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU/WHATSAPP NAMBA: 0749201985

Lengo likiwa ni kuibua, kuendeleza, kukuuza na kudumisha sekta ya ufugaji kuku katika maeneo mbalimbali hapa nchini Tanzania.

Changamoto hii inawakumba sana wafugaji wa kuku.Sababu zinazopelekea changamoto hii ni k**a zifuatazo.1. Ukosefu wa maji...
02/03/2022

Changamoto hii inawakumba sana wafugaji wa kuku.
Sababu zinazopelekea changamoto hii ni k**a zifuatazo.

1. Ukosefu wa maji ya kutosha kwa ajili ya kunywa.
2. Wadudu k**a vile E.coli hivyo hakikisha maranda yanakuwa makavu muda wote. Matumizi ya Glucose kwa muda mrefu huchochea changamoto hii kukua kwa kasi zaidi. Ikumbukwe glucose ni chakula kizuri cha wadudu wa magonjwa, hivyo inashauriwa kuwapa kwa maji safi na salama.
3. Joto kuzidi bandani. Joto likizidi husababisha kuku kukaukiwa maji na hatimaye kusababisha kinyesi kuwa kigumu sana.
4. Ukubwa wa punje za chakula. Ikiwa punje za chakula zitakuwa kubwa hivyo baada ya kumeng'enywa kuku hupata shida kuzitoa k**a kinyesi. Mfano, usimlishe kifaranga wa siku moja Growers mash.
5. Weka vyombo vya maji mbali na chanzo cha joto ili kuzuia maji kuchemka kupitiliza na kufanya kuku washindwe kunywa.

Ahsante.

Faida ya mwanga kwa kuku. Licha ya kumfanya kuku kuona chakula na maji mwanga pia una mchngo mkubwa sana katika kuongeza...
14/02/2022

Faida ya mwanga kwa kuku.

Licha ya kumfanya kuku kuona chakula na maji mwanga pia una mchngo mkubwa sana katika kuongeza kiwango cha utagaji wa mayai.
Kupitia uwepo wa mwanga Melatonin hormone huzalishwa kutoka kwenye Pineal gland. Melatonin hormone hufanya kazi kubwa katika mfumo wa utengenezaji wa mayai kwa kuku.
Kiwango cha mwanga kinachotakiwa ni 40watt kwa 100ft².  Mwanga unahusika katika kuuandaa mfumo wa uzazi kwa kuku hivyo kuku anaye ishi kwenye mwanga huwahi kuanza kutaga.
Ili kuweka msawazo wa shughuli katika mfumo huu kuku anayetaga anahitaji kupewa mwanga kwa masaa 16 na kukaa na giza kwa masa 8. Kwa maana hii unaweza kuzima taa saa nne usiku au ukaamua kuwasha taa saa nane alfajiri ili kutimiza masaa 8 ya kukaa bila mwanga.

🇹🇿

Address

Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00

Telephone

+255746201985

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mbena Poulry Consultancy posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Mbena Poulry Consultancy:

Share