WafugajiTz.com

WafugajiTz.com Kwa wafugaji 2

03/10/2017
15/01/2017

YAJUE MAGONJWA YA NG'OMBE
Asilimia kubwa ya magonjwa usababishwa na uchafu na vimelea vya magonjwa (micro organism) baadhi ya magonjwa yanayoshambulia ng'ombe ni pamoja na:-

*NDIGANA KALI(EAST COAST FEVER)
Ugonjwa huu hushambulia ng'ombe na nyati ambao hukaa kwenye maji.
USAMBAZAJI UGONJWA
ugonjwa huu usambazwa na kupe aina ya rhipicephalus appendiculatus ambaye humng'ata ng'ombe na kumwachia protozoa aina ya theileria ambao husababisha ugonjwa huo.
Mnyama uonyesha dalili siku 10 mpaka 25 (wastani wa siku 14).
DALILI.joto kali nyuzi joto 4(kawaida huwa na joto la 38)manyonya mgongoni husimama(rough hair coat)kuharishamatezi ya shingo huvimba.pua huwa kavu bila unyevu.

*NDIGANA BARIDI(ANAPLASMOSIS)
Ugonjwa huu unasababishwa na nzi(aina ya stomoxy's),mbung'o na kupe
UAMBUKIZAJI
Kupe anamuuma ng'ombe ili kupata chakula yani kunyonya damu,kutumia vifaa vya kitaalamu ambavyo havikuchemshwa mfano sindano.
Wanyama wanaoweza kupatwa ni mbuzi,kondoo,ng'ombe ila ndama hawapatwi

DALILIHoma Kali nyuzi joto 40 mpaka 41kinyesi kigumu chenye utando mweupekupumua kwa shida(dyspnoea)mnyama acheuimnyama kutotoa haja kubwa kwasababu ya omasum kutofanya kazi(constipation)

*UGONJWA WA MAPELE.
Ugonjwa huu unasababishwa na virusi(carpipoxvirus)
Virusi hivi huweza kukaa kwenye ngozi iliyokauka kwa siku 18

MAAMBUKIZI
Virusi hupatikana Kwenye mapele,mate na maji maji mengine ya mnyama pia unaambukizwa kwa kuumwa mbu jamii ya Andes culex baada ya kumuuma mnyama mwenye virusi.

DALILIHoma Kal iliyoambatana na kutokea mapele kwenye ngozihutokwa machozi na mak**asi mazitomapele makubwa hutokea kwenye shingo,kichwa,kiwele na miguuniuzalishaji wa maziwa hupungua na muda mwingine utupa mimba.

Chakula
29/12/2016

Chakula

FUNZA K**A VIRUTUBISHO KWA KUKU.

Funza wanaweza kupandwa ukitumia mbinu rahisi na hutumiwi k**a nyongeza katika lishe ya kuanzia vifaranga wadogo

MAANDALIZI
1.Changanya damu na mautumbo ya mnyama kwa mfano ng'ombe ama mbuzi na samadi katika chungu kikubwa kilicho wazi

2.Jaza 1/3 ya maji.

3.Nzi watataga mayai yao katika mchanganyiko huu na funza wataula.

4.kiache chungu wazi wakati wa mchana na kifunike usiku

5.Funza wakubwa wakusanye kwa kumwaga maji pole pole kwenye chungu.

6.Funza wataelea na unaweza kuwaosha na kuwalisha moja kwa moja.

KUMBUKA: Kuweka chungu mbali na watu kwani hunuka sana.

Usifuge kwa mazoea
29/12/2016

Usifuge kwa mazoea

HASARA ZA KUFUGA KUKU KWA MAZOEA
(Usisahau kushare kwa wingi na wengine wanufaike)

Kuna baadhi ya wafugaji huwa wanafuga kwa kutegemea uzoefu walio nao katika ufugaji bila kujali kuwa kuna mabadiliko kila Siku katika ufugaji

1)KUINGIZA VIFARANGA BILA MAANDALIZI SAHIHI
Wengi wengi wa wafugaji uwa wanaingiza vifaranga pasipo kufata utaratibu wa kitaalamu katika kuandaa banda pamoja na maandalizi ya kupokea vifaranga,kusafisha banda juu juu hupelekea kuifadhi vimelea vya magonjwa na kupelekea kuku huugua au kufa hatimae mfugaji hupata hasara kubwa.

2)KULISHA BILA MAELEKEZO SAHIHI
Kila aina ya kuku wana utaratibj wao wa kulishwa ukikiukwa uwezi kupata matokeo mazuri wengine wanadiliki kutumia aina moja ya chakula mwanzo mwisho yani anaweza kutumia SUPER STARTER kila siku bila kujua kila chakula kina kazi take.

3)KUTIBU KWA DAWA ISIYO SAHIHI
K**a inavyofahamika wafugaji wengi wamebarikiwa kwa kufahamu majina mengiya dawa kwa kutumia uzoefu wanatibu kuku wao magonjwa bila kupata ushauri wa dokta au mtaalamu mifugo kwa kufanya hivyo hutumia dawa nyingi tofauti hivyo hufanya ugonjwa kuwa sugu.

Chakula
29/12/2016

Chakula

Where u a, think and do. HAPA KAZI TU
27/12/2016

Where u a, think and do. HAPA KAZI TU

2po tofauti
24/12/2016

2po tofauti

HADITHI YA KUJIONGEZA

Mwita na Chuwa walipata kazi katika kiwanda cha kukamua juisi ya miwa pamoja, baada tu ya kuhitimu masomo yao. Wote walifanya kazi kwa bidii sana.

Baada ya miaka mingi kupita, Bosi alimpandisha cheo Mwita na kuwa mkuu wa mauzo lakini Chuwa alibakia pale alipokuwa.

Siku moja Chuwa alishindwa kuvumilia na kumpelekea boss malalamiko na kuomba kuacha kazi kwakua boss hathamini mfanyakazi anayefanya kazi kwa bidii bali anathamini mfanyakazi amabaye ana maneno,

Boss alijua kwamba chuwa alifanya kazi kwa bidii siku zote kwa miaka mingi, lakini ili kumsaidia chuwa aone tofauti kati yake yeye na mwita, boss alimwambia chuwa afanye yafuatayo. “nenda ukatafute yeyote anayeuza miwa sokoni, ujue kilo moja inauzwa kwa shilingi ngapi, Chuwa akaenda na akarudi na majibu kwamba, nimewaona na kilo moja ni shilingi elfu mbili.

Boss akamwambia, nitamuuliza Mwita swali hilo hilo.
Mwita pia alikwenda na kurudi na majibu: Nimeona mtu mmoja tu anauza miwa, kilo moja shilingi elfu mbili, kilo kumi kwa shilingi 19,000. Kwenye stoo ana akiba ya kilo 300 za miwa. Mezani alikuwa na miwa 200, kila muwa mmoja una kilo 20, yote ameisafirisha kutoka Morogoro siku mbili zilizopita. Bado ina afya na ina rangi nzuri na ubora unaotakiwa.

Chuwa alivutiwa sana na aligundua tofauti kati yake na Mwita. Aliamua kutokuacha kazi badala yake kujifunza kutoka kwa Mwita.

UMEELEWA NINI?

Address

Mbagala
Dar Es Salaam

Telephone

0784626875

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when WafugajiTz.com posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category