Afya ya mzazi na mtoto

Afya ya mzazi na mtoto Mbinu mbali mbali za kuboresha Afya ya mzazi na mtoto

WA NINI PID NA FANGASI SUGU ZIKUTESE?WENZIO   NA HAWATOKI TENA   WALA HARUFU MBAYANJOO TUKUSAIDIEDALILI ZA PID (K**A UNA...
25/11/2021

WA NINI PID NA FANGASI SUGU ZIKUTESE?

WENZIO NA HAWATOKI TENA WALA HARUFU MBAYA

NJOO TUKUSAIDIE
DALILI ZA PID (K**A UNA MOJA YA HIZI DALILI BASI FAHAMU UNA PID WAHI TIBA HARAKA KABLA WADUDU HAJAKUHARIBU AU KANSA)
➡️UTI za mara kwa mara
➡️Maumivu ya tumbo chini ya kitovu ambayo yanaweza kuwa upande mmmoja au pande zote kulia na kushoto pamoja na maumivu ya kiuno k**a cha period na mgongo
➡️Sehemu za siri kuwa na ulaini sana na kutokwa na uchafu unaonuka na miwasho mikali
➡️sehemu za mwanamke kuwa kavu na Kupata maumivu wakati watendo la ndoa wakati mwingine kupeleekea kuvuja damu wakati na baada ya tendo na hivo kukosa tena hamu ya tendo la ndoa
➡️Kuvurugika kwa hedhi na mfumo wa homoni
➡️Kutokwa na majimaji sehem za kusiko kawaida hasa yenye rangi ya njano na kijani
➡️ Harufu mbaya sehemu za siri
➡️Maumivu wakati wa
➡️Kupata maumivu wakati wa choo
➡️Mimba kutokatoka
➡️Mimba kuharibika
➡️Miwasho
➡️Kupata dalili za homa k**a kizunguzungu, mwili kukosa nguvu, kukosa hamu ya kula na uchovu mwingi.

NJOO TUKUPATIE SULUHISHO LA KUDUMU
Piga simu au tuma ujumbe Whatsapp 0685091472

Ute wa mimba ni ute unaovutika, ni ute muhimu sana linapokuja suala la kutungwa kwa ujauzito.Ute huu ambao huvutika mith...
16/11/2021

Ute wa mimba ni ute unaovutika, ni ute muhimu sana linapokuja suala la kutungwa kwa ujauzito.

Ute huu ambao huvutika mithili ya yai husaidia mbegu kuogelea na kupenya kwenye mlango wa kizazi na kwenda kulirutubisha yai kwenye mirija.

Baadhi ya njia za uzazi wa mpango zinapelekea kukosa ute wa mimba ili usishike mimba isiyotarajiwa.

Tatizo la kukosa ute wa mimba linachangia pia uchelewe kupata ujauzito. Baadhi ya wanawake watahitaji kutumia kwanza dawa za kuongeza ute ili kushika mimba.

Ute ute laini unaovutika ni wa mhimu ili kuweka mazingira mazuri ya kushika ujauzito.

Siku chache kabla ya mimba kutungwa ute ute laini unaovutika huanza kuzalishwa kwa wingi kwenye mlango wa kizazi.

Katika ulaini wake ute huu unaleta mazingira mazuri kwa mbegu za mwanaume kuogelea kupenya mlango wa kizazi.

Changamoto yoyote kwenye ute maana yake mbegu haitapenya na mimba haitatungwa.

SABABU 4 ZA KUKOSA UTE WA UZAZI

1. K**a madhara ya matumizi ya baadhi ya dawa
2. Umri
3. Matumizi ya Dawa za kupevusha mayai za Clomid
4. Kuwa na uzito pungufu
5. Maambukizi kwenye mji wa uzazi
6. K**a homoni zako zimevurugika
7. Kusafisha uke kupita kiasi (Douching)

Share Post hii na wengine wanufaike.

PID ni maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke,pid ni miongoni mwa maambukizi hatari na yenye madhara makubwa kwa m...
15/11/2021

PID ni maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke,pid ni miongoni mwa maambukizi hatari na yenye madhara makubwa kwa mwanamke. Anapoamkukizwa huweza kuathiri mfumo wa uzazi hata kupelekea kupata tatizo la ugumba.

☞ pid husababishwa na vimelea aina Ya Neisseria Gonorrhoe,chlamydia Trachomatis na mycoplasma hominis hivi ndivyo vimelea vinavyo husiswa zaidi katika maambukizi ya pid.

Dalili za maambukizi kwenye mfumo wa uzazi{ pid }

☛ Mwanamke kupata maumivu ya tumbo hasa chini ya kitovu.
☛ kupata maumivu ya mgongo eneo la kiunoni
☛ kupata maumivu wakati wakushiriki tendo la ndoa
☛ kutokwa na Damu kwa muda mrefu wakati wa hedhi
☛ kuhisi kichefuchefu na kutapika
☛ kutokwa na uchafu sehemu za siri

Vipimo vya pid
➡ Ili kuweza kutambua k**a unamaambukizi kwenye mfumo wako wa uzazi, pindi unapoona dalili hizo ni vyema kufika hospital au kwa wataalumu wa afya ili ufanyiwe uchunguzi na vipimo.......
👉 mkojo : uchunguzi wa mkojo hufanywa maabara ili kubaini aina ya vimelea,pia huweza kuoteshwa ili kubaini aina nyingine za vimelea wanaosababisha maambukizi pia.
👉 Full blood picture:kupima damu ili kubaini madhara kwenye chembechembe za damu
👉 cervical culture : kuchukua utando uliopo kwenye shingo ya kizazi ili kuotesha maabara.
👇Gynecological ultrasound : kuangalia mfumo wa uzazi wote na

MADHAYA YANAWEZA KUTOKEA
💬kumbuka pid yamuda mrefu au ya kujirudua inaweza kupelekea
▶ugumba
▶Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi

K**a tayari una tatizo hili tunaweza kukusaidia kukupa virutubisho Tiba ambavyo vinaweza kusaidia kupona P.I.D Kirahisi kabisa.

piga simu 0685091472

14/11/2021

Taja Magonjwa Mawili Ambayo hayana Tiba.

UTAJUAJE K**A UNA FANGASI SUGU__________________________________________________________________________ Kuna dalili nyi...
14/11/2021

UTAJUAJE K**A UNA FANGASI SUGU
__________________________________________________________________________

Kuna dalili nyingi zinazoonyesha kuwa una fangasi ukeni k**a zifuatazo;
1.Kuwa na miwasho sehemu za siri mara kwa mara
2.Vipele vidogo vidogo ukeni
3.Kutokwa na uchafu mweupe au wa rangi ya kijivu ukeni wenye harufu mbaya
4.Vidonda au kuwa na michubuko ukeni
5.Kutokwa na harufu mbaya ukeni
6.Kupatwa na maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.
7.Kuvimba au kuwa mwekundu katika mdomo wa nje ya uke.
8.Kuwaka moto ndani na nje ya uke.

Huenda ukawa nimhanga Sana wa hili karibu usaidiwe .

Jifunze na chukua hatua yako ya kiafya

UTINDIO WA UBONGO/ULEMAVU WA AKILI(CEREBRAL PALSY)Ni tatizo la mfumo wa fahamu(Neurologia) unaohusisha ubongo na mfumo w...
27/10/2021

UTINDIO WA UBONGO/ULEMAVU WA AKILI(CEREBRAL PALSY)

Ni tatizo la mfumo wa fahamu(Neurologia) unaohusisha ubongo na mfumo wa neva za fahamu.Tatizo hili hasa huathili sehemu ya ubongo ambayo inahusika na misuli ya mwili ,Na tatizo hili hutokea k**a ...
✨Ubongo haujakamilika katika ukuaji wake au
✨Kupata shida wakati wa kukifungua au baada ya kujifungua.
💧Mara nyingi sana watu huhusisha tatizo hili na mambo ya kishirikina mfano watu wanasema wazazi wamefanya hivyo ili kujitajirisha kitu ambacho sio kweli, kutokana na ili wazazi huweza kupoteza pesa na mali kwa waganga na uhai

SABABU TATIZO ILI
💧Kuna sababu nyingi za mtindio wa ubongo Baadhi ni
✅maambukizi anayopata mama wakati wa ujauzito
✅kupata matatizo wakati wa kujifungua k**a kumbana mtoto au kutumia mda mrefu wakati wa kujifungua au kujifungua kabla ya wakati( premature birth).
✅kutokwa kwa damu kwenye Ubongo wa mtoto.
✅kubadilika kwa mfumo wa vinasaba(genes) ambazo zinaweza kuathiri ukuaji wa ubongo wa mtoto
DALILI ZA TATIZO
Dalili za matatizo ya Akili huonekana sana katika kipindi cha umri wa miaka *mitatu* ya mwanzo ya ukuaji baada ya kuzaliwa,Dalili hizo ni k**a:-
✅Kukaza kwa misuli au misuli ya mwili kushindwa kufanya kazi ( hypotonia).
✅kulegea au kuishiwa nguvu kwa misuli.
✅Kutokuwa na uwezo wa kuuzuia na kuufanya mwili anavyotaka ( balance and co-ordination problem).
Note;Dalili hizi zinaweza kuonekana sehemu mbali mbali za mwili na inategemea na kiasi gani Umeathiriwa na tatizo hili,Watoto wengine wanaweza kuwa na matatizo madogo madogo ila wengine inawapelekea hadi ulemavu.
💧Watoto wengi wenye mtindio wa ubongo huwa wanapata matatizo k**a ..
✨Kifafa katika ukuajia
✨kushindwa kutafuna na kumeza chakula
✨kutoweza kuongea
✨kupata choo kigumu au kwa shida( constipation)
✨kutoweza kuzuia mkojo kutoka
✨matatizo ya kuona na kusikia,
✨matatizo ya kiunzi( skeleton) k**a kupinda kwa uti wa mgongo ( curved spine)
✨Mifupa kukaa sehemu tofauti k**a mfupa wa paja( hip dislocation)

NAMNA YA KUTAMBUA MTOTO MWENYE MATATIZO YA AKILI
✨Mtoto kuchelewa kukua k**a watoto wengine.
✨Mtoto kuchelewa kukaa au kukaza shingo vizuri,
✨Viungo kukak**aa mara kwa mara au kulegea kupita kiasi.

USHAURI NA UFUMBUZI
✨Wapo watoto wengi ambao wanatatizo ili na hata wazazi wao wamekata tamaa kabisa mara baada ya kuhudumiwa katika hospital mbalimbali bila Mafanikio, wengine wameenda mpaka kwa waganga wapiga ramli na baadhi ya watoto wamelemaa na wengine kupoteza maisha ..
Hongera kwa kusoma makala hii natumaini umefahamu vizuri changamoto hii
Kwa kumalizia k**a una changamoto hii waweza wasiliana nasi tukupatie tiba mbadala ya virutubisho lishe ambayo itaenda kuweka sawa changamoto hii kwa dozi ya miezi mitatu mpaka sita.
Piga simu 0685 091 472

Kuhusu MYCHOCO MyChoco ni chocolate pekee inayozalishwa na yenye maana halisi ya Chocolate huku ikiwa imewekewa virutubi...
26/10/2021

Kuhusu MYCHOCO

MyChoco ni chocolate pekee inayozalishwa na yenye maana halisi ya Chocolate huku ikiwa imewekewa virutubisho vingi zaidi vyenye manufaa kwa Afya ya mwili.

MyChoco inaweza kuongezewa Maji ya moto au maji baridi na kubaki na radha yake ileile ya Chocolate huku ikiukinga mwili wako na mashambulizi ya magonjwa. My Choco ikichanganywa na maji baridi inaleta radha ya kusisimua itakayokufanya ufurahie kinywaji hicho huku ukipata tiba. . My Choco pia ikichangwa na maji moto inazalisha tabaka zuri la chokleti na maziwa linaloelea juu ya maji moto hivyo kumfanya mtumiaji kufurahia sana kinywaji chake.

My Choco imesagwa katika unga laini zaidi kumsaidia mtumiaji kuutumia kwa urahisi zaidi hata kwa kuramba. My Choco imetengenezwa na unga laini wa Cocoa na kuongezewa
virutubisho. Kwa Kifupi ukitumia My Choco hauwezi kuacha kutamani Kutumia.

Wazoefu wa kutumia My Choco wanakuambia, Ukianza kutumia My Choco hauwezi kuacha kamwe.

My Choco imetengenezwa na: Unga wa Cocoa wenye ubora, Maziwa, Sukari, Alive! Mega- Nutritionals na Ungaunga wa DHA.
FDA FR No. 7508 5

MANUFAA YA MYCHOCO

• Ina Ongeza hamu ya kula kwa watoto kwa asilimia 100
• Inasaidia mtoto katika ukuaji wa ubongo hivyo humfanya mtoto awe na akili na kutunza kumbukumbu
• Humfanya mtoto achangamke mda wote anapokua anacheza
• Huweka sawa Afya ya macho ya mtoto
• Huongeza Kinga ya mwili ya mtoto hivyo humlinda na magonjwa.
• Hufanya ngozi ya mtoto kunawili.

Umri huu watoto huwa watundu na huweza kutembelea sehemu kadhaa na kuingiza mdomoni vitu mbalimbali k**a udongo, maji ma...
26/10/2021

Umri huu watoto huwa watundu na huweza kutembelea sehemu kadhaa na kuingiza mdomoni vitu mbalimbali k**a udongo, maji machafu n.k
Unaweza kumlinda mwanao kwa kumuongezea kinga ya mwili (body immune) dhidi ya magonjwa madogo k**a minyoo, bakteria na fangasi wa mdomoni

Andaa
• Tangawizi iliyosagwa au kupondwa kijiko kimoja
• Maji ya limao kijiko kimoja
• Asali vijiko viwili mpaka vitatu.

Changanya vitu hivi kwa pamoja kisha acha ikae kwa dakika 10 au zaidi
Utakuwa ukimpa mwanao kijiko kimoja mara tatu kwa siku.
Haina dozi, ni wewe tu na mapenzi yako kwa mwanao...
Pia hata watu wazima mnaweza kutumia kuepuka magonjwa nyemelezi k**a mafua, kikohozi na matatizo ya choo kigumu....

Pia unaweza kumnunulia MYCHOCO Kirutubisho ambacho kitampa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa hatarishi na kumfanya awe na Furaha muda wote.
MYCHOCO inapatikana Ofisini kwetu waweza wasiliana nasi tukupatie
Piga simu 0685 091 472

Kuwa mzazi ni jambo jema, ila kulea mtoto si kitu rahisi, haswa akiwa ndio mtoto wa kwanza. Wengi wetu tunalea watoto ku...
26/10/2021

Kuwa mzazi ni jambo jema, ila kulea mtoto si kitu rahisi, haswa akiwa ndio mtoto wa kwanza. Wengi wetu tunalea watoto kutokana na maelekezo ya watu wenye uzoefu na malezi kwa muda mrefu. Tatizo linakuja pale ambapo mbinu wanazotumia zinapoleta madhara makubwa kuliko faida. Mie nasisitiza kuwa, kulea si rahisi, maana kila mtoto ana tabia zake na ni vizuri mzazi akiwa na muda wa kujua nini hasa atakacho mtoto kabla ya kufuata ushauri usio wa kitaalamu na kusababisha madhara makubwa.
Ni muhimu kuzingatia kuwa, katika mazingira yeyote yale usimlazimishe mtoto kula na ni hatari kubwa kumkaba ili ameze chakula. Kulazimisha mtoto kula ni kumjengea tabia ya kuchukia chakula. Mtoto akishajenga tabia hii hawezi kuacha sababu atakuwa anahusisha chakula na adhabu. Sababu hakuna mtu anayependa adhabu, atakuwa anachukia chakula cha aina yeyote. Matokeo yake ni kuwa mtoto atajenga tambia mbaya zaidi ya kukataa kula chakula cha aina zote. Pia, kumkaba mtoto kunaweza kuleta matatizo makubwa k**a vile kufanya chakula kuingia kwenye njia ya hewa, hii itakuletea kesi zisizo za lazima.
Zifuatazo ni njia 5 ambazo unaweza anza kuzitumia kumsaidia mwanao apende chakula na asisumbue.

1. KUBADILISHA VYOMBO VYA CHAKULA VYA MTOTO.
Mtoto huvutiwa zaidi na rangi, hasa kwenye vitu anavyotaka kula. Mtoto anaweza kuchoka kula chakula sababu anatumia chombo kimoja kila siku, hii haijalishi k**a chakula kinabadilika au la. Ni muhimu kumuandalia mtoto chakula kwenye vyombo vyenye rangi na maumbo tofauti. Jambo la kuzingatia usirudie chombo kwa wiki nzima, k**a inawezekana. Hii inamfanya mtoto kuona utofauti wakati wa kula, na kumfanya apate hamu ya kula.
Mfano, unaweza kutumia bakuli, vikombe, sahani, vijiko vyenye rangi tofauti ili kumfanya aone anakula katika mazingira tofauti na hii humfanya awe na hamu kula chakula zaidi.

2. WATOTO WALE PAMOJA NA FAMILIA.
Watoto hupenda kuiga wazazi. Mara nyingi sana watoto hupewa vyakula wale wakiwa wenyewe wakati watu wengine wanaendelea na shughuli za kawaida. Hii inaweza kumfanya mtoto kupendelea zaidi kucheza kuliko kula. Ni muhimu kumlisha mtoto wakati familia nzima imekaa mezani au jamvini tayari kwa kula. Katika muda huu mtoto atakula vizuri bila vikwazo, maana kila mmoja anakula.
Vilevile, watoto wengine (umri wa miezi 10 hadi miaka 2) hupendelea kula vyakula wanavyokula watu wazima, hata k**a haviwafai, na kugoma vyakula vya watoto. Ni bora kumuandalia chakula kinachofanana na unachokula wewe na kumpa ili apate kufurahia. Huwezi kubishana na mtoto, ingawa huwezi kumpa kila kitu anachotaka pia. Ila jaribu kutumia mbinu tofauti ili apate kula na kuridhika. Afya yake ni bora kuliko kitu kingine kwenye maisha yake kwa muda huu.

3. JARIBU KUMSOMA MTOTO ANAPENDA NINI
Kila mzazi ana jukumu la kumsoma mwanae anapendelea nini. Ili kuweza kumfanya mtoto ale vizuri, ni vyema kubadilisha vyakula kila wakati – siyo kila siku. Mara nyingi watoto huchukua muda kuzoea chakula, hivyo ni vizuri kumpa mtoto chakula kwa muda wa siku 2 hadi 3 na kumbadilishia na chakula kingine. Hii inasaidia mtoto kuonja ladha ya chakula. Anaweza kukipenda au kukichukia. K**a atakataa ladha ya chakula kipya, usikate tamaa, jaribu kumpa tena baada ya siku moja au mbili, unaweza kukuta akaipenda ladha na akala chakula bila tatizo.
Usikate tamaa kwenye kumpa mwanao upendo wako k**a mzazi. Jaribu kila njia unayoweza na usife moyo. Watoto ni wagumu kuwaelewa na inachukua muda, lakini pale unapofikia hatua ya kujua anachopenda utakuwa umepata jibu zuri jinsi ya kuendelea kumlea mwanao.

4. EPUKA KUMPA VITU VITAMU WAKATI WA MLO
Watoto wengi wanapenda kula vitu vidogo vidogo (p**i, biskuti, juisi, keki n.k.) kila mara. Hivi vitafunwa vinaweza kumfanya mtoto azibe njaa na kutokuwa na hamu ya kula chakula muda unapowadia. Ili kuzuia hii tabia, ni bora kuacha kumpa mtoto vitu vidogo vidogo kati ya milo ili kumfanya kuwa na hamu ya chakula muda unapowadia.
Mara nyingi inashauriwa kumlisha mtoto mara 4 hadi 5 kwa siku. Hii ni vizuri sababu mwili wa mtoto unakuwa unahitaji virutubisho vingi mara kwa mara kwa kusaidia kukua. Ni vizuri kumpa mtoto chakula bora kuliko kumjaza tumbo na vyakula vyenye sukari zisizo na kazi mwilini.

5. MSIKILIZE MTOTO ANACHOTAKA.
Mara nyingi mzazi au mlezi unaweza kudhani kuwa unajua zaidi kiwango cha chakula anachotakiwa kula mtoto kuliko hata mtoto mwenyewe. Hili linaweza kuwa tatizo kubwa litakalopelekea mzazi kumlazimisha mtoto kula chakula kingi kupita kiasi. Fahamu kuwa, watoto wanajua kiwango cha chakula kinachowatosha na wakati gani ni muafaka wa kula. Hivyo, itakuwa rahisi kwako k**a ukimsikiliza mtoto anataka nini, kuliko kulazimisha kile unachotaka wewe. Hakuna mtoto anayeweza kuvumilia kukaa na njaa. Watoto wote huhitaji chakula ili kucheza na kufurahi na wenzao. Hivyo basi, pale anakuwa na njaa atasema, au kulia, na ndio muda muafaka wa kumpa chakula unachotaka.
Swala muhimu la kuzingatia ni kuwa, katika mazingira yeyote, usimlazimishe mtoto kula. Usimkabe. Kulazimisha mtoto kula ni kumjengea tabia ya kuchukia chakula. Na akishajenga tabia hii hawezi kuacha sababu atakuwa anahusisha chakula na adhabu. Hakuna mtu anayependa adhabu. Hivyo, watu wengi wanaopenda kulazimisha mtoto kula kwa kumkaba huwa wanajenga tatizo kubwa zaidi ya lile la kula tu.

HABARI NJEMA.
Hongera kwa kusoma Makala hii natumaini inaenda kumsaidia mtoto wako kuwa na afya njema na kupenda kula, K**a changamoto hii ni kubwa kwa mwanao unahitaji msaada na ushauri wa haraka sana waweza wasiliana nasi kwani tunacho kirutubisho lishe maalumu kiitwacho MYCHOCO ambacho kitaenda kumsaidia mwanao kupenda kula kirahisi kabisa.
MAWASILIANO.
Piga simu namba 0685 091 472 Karibu sana.

1. Kwanza hii imani potofu inaeleza kwamba kubemenda mtoto ni pale wanandoa wanapojihusisha na tendo la ndoa baada ya mt...
25/10/2021

1. Kwanza hii imani potofu inaeleza kwamba kubemenda mtoto ni pale wanandoa wanapojihusisha na tendo la ndoa baada ya mtoto Kuzaliwa (pale mke anapokuwa tayari kiafya kwa tendo la ndoa baada ya kujifungua) kwa maana kwamba sperms(begu za kiume) huharibu maziwa ambayo mtoto ananyonya, si kweli, hakuna uhusiano wowote kati ya maziwa ya mama na sperms katika kuathiri afya ya mtoto.

2. Pili kubemenda mtoto ni kitendo cha wanandoa kujihusisha na tendo la ndoa na mke kushika mimba miezi mwili tu au mitatu tu baada ya kujifungua na kupelekea kuzaa mtoto mwingine baada ya mwaka na matokeo yake mtoto aliyetangulia Kuzaliwa huwa dhaifu kiafya (huchelewa kutembea) na huitwa ni mtoto ambaye amebemendwa, kitu ambacho ni imani potofu kwani kuna wanandoa wengi tu wamezaa watoto waliopishana mwaka na wote wana afya njema kabisa.

3. Tatu kubemenda ni kitendo cha mwanandoa mmoja kutoka nje ya ndoa (s*x) na akirudi ndani huendelea na tendo la ndoa na matokeo yake mtoto wa ndani ya ndoa huwa dhaifu, pia ni imani potofu hakuna kitu k**a hicho. Jambo la msingi ni kufuata ushauri wa kitaalamu ambao ni wiki 6hadi 12 baada ya kujifungua.

➡️ Je, kuna ukweli wowote kuhusiana na hii imani potofu iwe wanandoa kujihusisha na tendo la ndoa baada ya mtoto Kuzaliwa au kuzaa mwingine baada ya mwaka au hata kutoka nje hakuna uhusiano na mtoto aliyezaliwa k**a suala la usafi na lishe bora litazingatiwa kwa mtoto anayehusika.

➡️ Je, kulikoni mababu zetu wakaweka imani k**a hiyo kwa wanandoa?
K**a zilivyo imani zingine potofu k**a vile mwanamke mjamzito kutokula mayai mababu zetu walikuwa na somo ndani yake, inawezekana walitaka kuhakikisha wanandoa wanashiriki vizuri katika kulea mtoto kwa pamoja bila kueendekeza tabia za uchafu na kujirusha nje na ndani ya ndoa bila utaratibu. Pia labda mababu zetu walihofia kitendo cha mwanamke kutoa maziwa (chuluzika) wakati wa tendo la ndoa hasa anapofika kileleni (tangu ajifungue hadi miezi 8 hivi) na wakawa wanahofia kinaweza kuathiri kiwango cha chakula cha mtoto hivyo ili kuzuia ni kutunga imani (potofu) kwamba mtoto ataathirika kwa mke na mume kushiriki tendo la ndoa.

➡️ Je, ili mtoto asionekane amebemendwa wanandoa wanahitaji kufanya kitu gani?
Ni vizuri kufahamu kwamba hakuna uhusiano wa sperms kuharibu maziwa ya mama wakati wa kumnyonyesha mtoto hivyo wanandoa kushiriki tendo la ndoa halina uhusiano wowote na mtoto kuwa na afya mbaya kiasi cha kuchelewa kutembea.
Mtoto anahitaji watoto chakula bora chenye viini-lishe vyote vinavyohitajika ili kukua vizuri pia mama anahitaji kujiweka mazingira safi (kuwa msafi) wakati ananyonyesha, ahakikishe anasafisha chuchu zake na mikono yake au kuzingatia usafi kimwili kabla ya kumnyonyesha mtoto iwe baada ya s*x au muda wowote.

Hedhi yako imevurugika na unawaza ni kwa namna gani utaweza kuiweka sawa....!Unatumia dawa zipi kwa sasa kurekebisha hom...
24/10/2021

Hedhi yako imevurugika na unawaza ni kwa namna gani utaweza kuiweka sawa....!

Unatumia dawa zipi kwa sasa kurekebisha homoni au ndo umekataa tamaa kuhusiana na mambo ya uzazi....!

Today i have some tips for you..!
Wakati ukiendelea kutafuta ufumbuzi wa tatizo lako nakusisitiza kufanya mabadiliko katika vyako vya;
Haijalishi unaishi mazingira yapi au uchumi wako ukoje, jitahidi kuweka ulazima wa
👇🏼
• Kula parachichi zima 1 kila siku k**a huwezi walau kipande kimoja cha parachichi

• Tumia vyakula vya wanga kwa kiwango kidogo, vyakula k**a Mahindi, Ugali na Dona, Viazi, Mihogo, Ndizi, Tambi n.k, ila ongeza wingi wa mboga za majani na matunda k**a spinach, bamia, msusa, parachichi, ndizi mbivu n.k ni vizuri sana kwenye kuimarisha homoni zako

• Epuka kahawa, chai ya rangi, soda nyeusi na vinywaji vingine vyote vyenye kiwango kingi cha kafeina ndani yake

• Achana na msongo wa mawazo (stress) na upate usingizi wa kutosha kila siku, k**a hupati usingizi jitahidi kunywa glass ya maziwa fresh yaliyotiwa mdalasini na vijiko kadhaa vya asali mbichi, inaleta usingizi kuliko kumeza pilitoni

• Usitumie dawa za uzazi wa mpango k**a unahitaji kuweka homoni zako

• Kuna vyakula tunafosi kivitumia ila havina ulazima wowote wala havina faida mwili, vyakula k**a chipsi, chapati, vinywaji k**a soda.... Usishindane na utandawazi, kula kawaida uijenge Afya yako

• Kunywa chai yako yenye tangawizi, mdalasini, iliki na mchaichai
K**a utaweza kupata Unga Wa Mbegu Ya Parachichi utumie.
Weka kijiko kimoja cha unga wa mbegu ya parachichi kwenye kikombe cha chai, unasaidia kuondoa tindikali mwilini kwa ndugu zangu ambao mmetumia au mnatumia sana uzazi wa mpango, sindano, p2, vidonge n.k
Weka nia, chukua hatua ndani ya wiki 3 hadi 4 uje na mrejesho wako

👉🏻 Ni changamoto gani ya uzazi ambayo mpaka sasa inakuwazisha sana na unapenda nikusaidie..? [niandikie katika comment]
K**a unasumbuliwa na changamoto za ukavu ukeni, kukosa hisia za mapenzi, kukosa ute wa uzazi, kupata dalili za mimba ila ukipima haionekani, hedhi yako kukosa mpangilio mzuri, hedhi kutoka kidogo, yenye mabonge au utelezi n.k nina Kirutubisho kizuri cha asili kinachoweza kukusaidia kuondoa changamoto hizo, kusafisha fuko la uzazi na kurekebisha mzunguko hedhi.

Nipigie Simu /DM / WhatsApp namba 0685091472
Jifunze na Kuchukua Hatua bila Kukata Tamaa utazishinda nyakati ngumu.....

Kabla hujakata tamaa, nakuongezea mambo muhimu ya kuzingatia ili kuhakikisha mirija ya uzazi iko safi muda wote.Kwa kuku...
24/10/2021

Kabla hujakata tamaa, nakuongezea mambo muhimu ya kuzingatia ili kuhakikisha mirija ya uzazi iko safi muda wote.

Kwa kukumbusha ni kwamba mirija ya uzazi husaidia yai kusafiri kutoka kwenye ovari mpaka kwenye fuko la uzazi, hivyo mirija ya uzazi ikiziba yai la mwanamke huwa vigumu kusafiri kutoka kwenye ovari mpaka kwenye mji wa uzazi mimba inapotungwa...

Mirija inaweza kuziba iwapo k**a itashambuliwa na fangasi au bakteria na kupelekea kuziba kwa kujaa maji au kuvimba, au iwapo k**a kuna uvimbe wa fibroid kwenye mji wa uzazi.....

Pia k**a umewahi kuharibu mimba na kusafishwa kwa vyuma inaweza kupelekea vidonda au makovu ndani ya mirija ambayo huweza kusababisha mirija kuziba kwa sababu ya kuwepo kwa makovu
Wakati ukiendelea kutafuta dawa bora ya kukusaidia, jitahidi kuweka mazingatio ambayo yatakusaidia kukupa matokeo haraka kukuepusha na oparesheni

1. kwa sababu mirija inaweza kuziba kutokana na matatizo ya bakteria/fangasi, jitahidi kutibu magonjwa ya kaswende, U.T.I. sugu na matatizo ya P.I.D kwa kuzingatia usafi na matumizi ya vyakula vya kukusaidia kusafisha kizazi k**a tangawizi, tufaha (apple), kitunguu saumu, binzari ya manjano, maziwa mtindi, karafuu n.k
Weka mbali vyakula ambavyo si rafiki kwa afya yako k**a vyakula vya kukobolewa, soda, vyakula vya makopo na vile vya kutiwa mafuta mengi (natumaini unakumbuka)

2. Kwa sababu mirija inaweza kuziba kwa sababu ya uvimbe na makovu ni muhimu sana kupendelea kutumia vyakula vyenye kuondoa vivimbe ndani ya mwili na kubalansi homoni, vyakula hivi ni pamoja na Limao, Mdalasini, Machungwa, Mboga za Majani, Pilipili hoho, Kotimiri, Iliki n.k

3. Punguza stress, jitahidi kujiwekea mazingira ambayo yatakusaidia kuwa na furaha, msongo wa mawazo ni chanzo cha homoni kuvurugika, na mvurugiko wa homoni ni chanzo cha vivimbe kuongezeka ukubwa, usipothibiti stress unaweza kujikuta unazidi kuongeza tatizo badala ya kumaliza tatizo

4. Pendelea kufanya masaji ya maeneo ya nyonga na chini tumbo kwa kutumia mafuta ya mnyonyo...

5. Punguza uzito, hakikisha una uzito unaoendana na kimo chako

6. Fanya mazoezi ya Yoga... K**a ni mpenzi wa Mazoezi ya Kunyoosha Mwili wako basi fanya mazoezi ya yoga muda wowote utaoamua kufanya... Unaweza kuingia youtube kujifunza, zipo aina mbalimbali za kufanya yoga.... Unaweza kupitia intro kidogo ya video niliyoweka youtube
Bofya https://youtu.be/jd4W0DUKn5I

K**a una changamoto za uzazi k**a uvimbe, mirija kuziba, P.I.D, Hedhi Haieleweki na Unatamani Kuzitibu Changamoto hizi kwa pamoja nakushauri kuchukua huku ukiendelea kuzingatia kanuni zako bora za uzazi.

Wasiliana nami kwa simu au kwa kutuma ujumbe inbox 0685091472

Address

Makumbusho
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afya ya mzazi na mtoto posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share