03/04/2020
KUPANGA VIZURI NI NUSU YA KUTEKELEZA MRADI WAKO
------------------
Haijalishi ni biashara au ni taasisi au ni mradi, Vyote vinahitaji mipango ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. Wadau wengi wa maendeleo wanakwama sana kufikia malengo wanayojiwekea kwa sababu ya kutokupanga vizuri. Wengi wanajiuliza kupanga vizuri ni kupi? Na wengine wanafikiri kupanga ni kuweka malengo tu! La hasha! Ni Zaidi ya kuweka malengo. Tafuta Elimu ya Kupanga ujifunze namna nzuri ya kupanga.
JEHA Wills Consulting kuna wataalamu wanaoweza kufanikisha ndoto yako kwa kukusaidia kuelewa nini maana halisi ya kupanga, umuhimu wa kupanga, hatua za kupanga na kupanga malengo kimantiki.
---------------
Kupanga hapakuanza na sisi. Kulianza na mwenyezi Mungu. Ukisoma Luka 14:28-32, Mungu anasema;
“Kwa maana ni nani miongoni mwenu ambaye akitaka kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama zake ili ajue k**a ana kiasi cha kutosha cha kumalizia? La sivyo baada ya kuweka misingi na kushindwa kumaliza watu watamcheka wakisema, mtu huyu alianza kujenga lakini hakumalizia.”
Au
“Ni mfalme gani ambaye akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, hataketi kwanza na kufikiri k**a ataweza, kwa askari wake elfu kumi, kumkabili yule aliye na askari elfu ishirini? K**a anaona hataweza atawatuma wajumbe kutaka masharti ya amani wakati mfalme huyo mwingine angali mbali”
Hata Mungu alipoumba alikuwa na Mpango. Aliutekeleza kwa kuzingatia kipaumbele, mantiki, rasilimali na muda. Alifuatilia, Alitathmini, Alifurahia matokeo ya kazi yake, Alibadili mpango wake alipobaini dosari. (Soma Mw. 1: 1 – 29; 2: 1 - 3, 15; 3:22 -24)
Pia katika kitabu kitakatifu Qur’an, imeandikwa k**a ifuatatavyo:
“Wanapanga na Allah naye pia anapanga; lakini Allah ndiye mpangaji bora kabisa” (Qur’an 8:30)
Ikiwa inathibitisha kwamba, hata Mungu naye ana mipango, nasi binadamu tunatakiwa tupange mambo yetu pia.Ila kazi ya mwisho ya kutimiza mipango yetu tunatakiwa kumuachia Mungu kwa kuwa yeye anajua kupanga kuliko sisi wanaadamu.
K**a Mungu ni model wetu wa kwanza na tuige mfano wake, tupange kwa maendeleo Zaidi.
---------------
Ukitaka kupata Elimu zaidi, tutafute Jeha Wills Consulting tukuvushe daraja. Wasiliana nasi kupitia:-
PHONE: +255 766 534 261
E-MAIL: [email protected]
---------------