Lissa Mona

Lissa Mona Mama Mtarajiwa
Mjasiriamali
Mbunifu
Mshauri
Rafiki Be You

Hapa kuwa huru kwa lolote lihusianalo na maisha, kazi,mahusiano, ajira, elimu, projects, ideas, biashara,Tutasikilizana na kushaurina kwa uwezo wake Mola atavyotujalia.

05/02/2026

Laa 'illaha 'illallahu wahdahu la shareeka lahu, lahul-mulku wa lahul-hamdu, wa Huwa 'alaa kulli shay'in Qadeer. Subhaanallahi, walhamdu lillaahi, wa laa 'ilaha 'illallahu, wallaahu 'akbar, wa laa hawla wa laa Quwwata 'illaa billaahil-'Aliyyil-'Adheem, Rabbighfir lee

05/02/2026

MKEO NI AMANA ISHI NAYE KWA WEMA.

05/02/2026

ALLAH NDIYE MWENYE KURUZUKU.

05/02/2026

USIWE MJINGA K**A WAO.

05/02/2026

UKIMALIZA KUNYWA MAZIWA SOMA DUA HII.

NA WANAWAKE wenye waume, isipo kuwa walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Ndiyo Sharia ya Mwenyezi Mungu juu yenu. Na ...
14/09/2024

NA WANAWAKE wenye waume, isipo kuwa walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Ndiyo Sharia ya Mwenyezi Mungu juu yenu. Na mmehalilishiwa wasio kuwa hao, mtafute kwa mali yenu kwa kuowa pasina kuzini. K**a mnavyo starehe nao, basi wapeni mahari yao kwa kuwa ni waajibu. Wala hapana lawama juu yenu kwa mtakacho kubaliana baada ya kutimiza waajibu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua na Mwenye hikima.

Na asiyeweza kati yenu kupata mali ya kuolea wanawake wa kiungwana Waumini, na aoe katika vijakazi Waumini iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa imani yenu. Nyinyi mmetokana wenyewe kwa wenyewe. Basi waoeni kwa idhini ya watu wao, na wapeni mahari yao k**a ada, wawe wanawake wema, si makahaba wala si mahawara. Na wanapo olewa kisha wakafanya uchafu basi adhabu yao itakuwa ni nusu ya adhabu waliyo wekewa waungwana. Hayo ni kwa yule miongoni mwenu anaye ogopa kuingia katika zina. Na mkisubiri ndio bora kwenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.{{Qur'an 4:24-25}}.

14/09/2024

Wanawake waovu ni wa wanaume waovu, na wanaume waovu ni wa wanawake waovu. Na wanawake wema ni wa wanaume wema, na wanaume wema ni wa wanawake wema. Hao wameepushwa na hayo wanayo yasema; wao watapata msamaha na riziki ya ukarimu.

Enyi mlio amini! Msiingie nyumba zisio nyumba zenu mpaka mwombe ruhusa, na mwatolee salamu wenyewe. Hayo ni bora kwenu mpate kukumbuka.

Na msip o mkuta mtu humo basi msiingie mpaka mruhusiwe. Na mkiambiwa: Rudini! Basi rudini. Hivi ni usafi zaidi kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua mnayo yatenda.{{Qur'an 24:26-28}}.

14/09/2024

Dua ya mzazi kwa mwanawe.

14/09/2024

Tusihau kutoa sadaka kila itwapo leo. Tujitahidi kutoa sadaka kwani Sadaka inamlinda mtu na mabalaa na pia kutoa sadaka ni kuzidishiwa riziki maradufu.

06/05/2023

Kwa mapokezi ya Umar (r.a) ambaye alisema;
Wakati tulipokaa siku moja na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ((s.a.w)) alitokea mbele yetu mtu aliyevaa nguo nyeupe sana na nywele nyeusi sana. Hakuna athari ya kusafiri iliyoonekana kwake, na hakuna hata mmoja wetu aliyemjua. Alikaa karibu na Mtume ((s.a.w)) akaweka magoti yake dhidi ya magoti ya Mtume ((s.a.w)) na akaweka mikono yake juu ya mapaja yake, akasema:

"Ewe Muhammad! Nijulishe juu ya Uislamu." Mjumbe wa Allaah ((s.a.w)) akajibu: "Uislamu ni kwamba unapaswa kushuhudia kwamba hakuna mungu anayestahili kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mjumbe wake ((s.a.w)), kwamba unapaswa kusimamisha salah (ibada ya swala), ulipe Zaka, ufunge mwezi wa Ramadhani, na fanya Hajj (Hija) kuiendea Nyumba ya Allah (Ka'bah huko Makka), ikiwa unaweza kupata njia ya hiyo (au pata njia ya kufanya safari yake). " Alisema: "Umesema kweli."

Tulishangazwa na hivyo kumuuliza maswali ((s.a.w)) na kisha kumwambia kwamba alikuwa sawa, lakini aliendelea kusema, "Nijulishe juu ya Iman (imani)." Yeye (Mtume) akajibu, "Ni kwamba kumwamini Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume wake na Siku ya Mwisho, na hatima (qadar), kwa uzuri na kwa ubaya." Alisema, "Umesema kweli."

Kisha (yule mtu) akasema, "Nijulishe kuhusu Ihsan." Yeye (Mtume) akajibu, "Ni kwamba unapaswa kumtumikia Mwenyezi Mungu kana kwamba unamuona, kwani ingawa huwezi kumwona bado anakuona." Akasema, Nijulishe juu ya Saa (kiyama). Yeye (Mtume) akasema, "Kwa kuwa yule aliyehojiwa hajui chochote zaidi ya anayeuliza."

Akasema:, niambie kuhusu ishara zake." Alisema, "Ni kwamba mtumwa wa k**e atazaa bibi yake na kwamba utawaona wasio na viatu,walio uchi, walio wanyonge, na wachungaji wa kondoo (wanaoshindana na kila mmoja) katika kujenga majengo ya juu." Kisha huyo mtu akaondoka.

Tukakaa muda kidogo, kisha yeye (Mtume) akasema, "Ewe Umar, unajua aliyehoji huyo alikuwa nani? " Nilimjibu, "Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake wanajua zaidi." Alisema, "Huyo alikuwa Jibril. Alikuja kukufundisheni dini yenu." [Muslim].

06/05/2023

Imesimuliwa kutoka kwa Amirul Mu'minin, Abu Hafs 'Umar bin al-Khattab (ra) ambaye alisema;

Nilimsikia Mjumbe wa Allaah (s.a.w) akisema: "Matendo yanahukumiwa kwa nia (niyyah), Na hakika ana kila mtu kile alichokusudia (anapofanya jambo).

Kwa hivyo, yule ambaye uhamiaji wake (hijrah) ulikuwa kwa Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake, uhamiaji wake ni Kwa Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake.Lakini yeye ambaye uhamiaji ni kwa ajili ya kupata vitu vya kidunia, au kwa ajili ya kupata mke ili amuoe, uhamiaji wake ni kwa yale ambayo alihamia".[Bukhari & Muslim].

Usijaribu kumbadilisha mtu yeyote, tafuta Nafsi(Roho) inayofanana na wewe tangu mwanzo.
05/05/2023

Usijaribu kumbadilisha mtu yeyote, tafuta Nafsi(Roho) inayofanana na wewe tangu mwanzo.

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Lissa Mona posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share