17/02/2026
“Chini ya mwamvuli wa Institution of Engineers Tanzania (IET), wahandisi wetu wakitoa ufafanuzi wa kina juu ya umuhimu wa uhandisi katika kuharakisha maendeleo ya taifa, kukuza ubunifu wa kiteknolojia na kutoa suluhisho endelevu kwa jamii. Kikao Kikuu cha AGM kilichofanyika tarehe 06 Februari, Kingjada – Morocco (DSM) kimeendelea kuimarisha mshikamano, taaluma na maono ya wahandisi wa Tanzania katika kujenga kesho bora.”