Shule ya Biashara-SB

Shule ya Biashara-SB Tunafunisha yale tuliyo yakosa shuleni kuhusu dunia ya biashara na fursa

01/01/2022

Kheri ya mwaka mpya 2022.

Hata k**a ajira ngumu, zipo fursa za biashara za kufanya.

Kuna moja unanunua bidhaa kwa shilingi elf 19 unauza kwa shilingi elf 30, faida Tsh 11,000..... Ukiuza bidhaa 50 kwa mwezi unapata Tsh 550,000.

.

Usidhani hajasoma.. La hasha, kasoma, vyeti anavyo na huwenda ametumia miaka 16/17 au 20 kusoma, alipo kuwa shule aliand...
12/11/2021

Usidhani hajasoma.. La hasha, kasoma, vyeti anavyo na huwenda ametumia miaka 16/17 au 20 kusoma, alipo kuwa shule aliandaliwa kuajiriwa ofisi fulani lakini mara tu baada ya kuhitimu hakuna ile ajira aliyoisomea kwa miaka mingi.

Je nani alaumiwe?

08/11/2021

Faida ya kutangaza biashara online.

Leo nimetafutwa na watu 7 kutoka mikoa ya

Dar ×2, Mwanza, Morogoro, Songea, Mbeya, Arusha.

Katika hawa saba

Mmoja wa Morogoro amenunua leo.

Wa Songea ameahidi kulipa kesho.

Wengine wanajipanga(Hawa huwa siwa hesabu sana).. Wanaojipanga.

Somo
K**a ukiweza kuweka biashara online kila siku maana yake unawafikia watu mikoa yote kwa wakati mmoja wewe ukiwa eneo moja tena na simu yako.

Sio rahisi kukosa kuuza kila wiki.. Then kila mwezi.

Hatimae huwezi shindwa kujiwekea akiba na kupiga hatua japo ndogo

Hakuna alie zaliwa anajua, wote tunajifunza, kwa dunia ya leo ni vyema kujifunza habari ya Online k**a kweli mtu unataka kutanua soko

Tusiache kujifunza.

NB: Ninapo sema Online namaanisha Matangazo ya kulipia (Sponsored Ads) za Facebook na Instagram.

Organic reach za Insta na Facebook siku hizi haziuzi sana kwa sababu mara nyingi huwa na userious followers.

🖊️Kalam yangu.
Nawapenda 😊

Kiukweli inauma sana, tumesoma kwa miaka mingi, tumetumia gharama kubwa za ada, tuition, nauli, matumizi, peni, daftari ...
08/11/2021

Kiukweli inauma sana, tumesoma kwa miaka mingi, tumetumia gharama kubwa za ada, tuition, nauli, matumizi, peni, daftari mpaka kufika chuo kikuu lakini baada ya kumaliza ajira hakuna tumebakia kuhangaika. Kiukweli inauma, tuna ambiwa tujiajiri wakati hatukuandaliwa vizuri kwenye sekta hiyo, yani maisha ya sasa kusoma ni k**a kupoteza muda maana hakuna mwenye uhakika k**a elimu itamsaidia ama la. Inauma inauma inauma inauma sana.

Halafu na bodi ya mikopo wanasema tuwalipe pesa zao wakati hatuna ajira wala chanzo cha mapato, zikitangazwa nafasi za ajira wanataka uwe chini ya umri wa miaka 25 au uwe umepitia JKT sasa sisi tulio soma chuo tukiwa na umri mkubwa tukaombe wapi ajira? Je wale ambao hatukupangiwa kwenda jeshini tuombe wapi kazi. Inauma.

Me ndio maana niliamua kuanzisha hii shule ya biashara yani nimeanza upyaa huku nimeunganisha vijana waliopo chuo na walio maliza waje tujaribu kutafuta njia ya kutoboa kwenye maisha maana ajira sio jambo la kutegemea tena.

06/11/2021

Hakuna biashara ambayo utaianza leo na baada ya muda mfupi ikakupa mafaniko makubwa. Vijana tujifunze kuvumilia maana kufanikiwa ni safari ngumu.

05/11/2021

Sio lazima kile kinachokuingizia kipato kitokane na yale uliyo yasoma shuleni au chuoni, kuna wakati fursa zipo kwenye eneo ambalo sio professional yako, unachopaswa kufanya ni kuamua kujifunza upya, upate ujuzi wa eneo husika kisha anza taratibu, kadri muda unavyozidi kwenda utapata uzoefu.

Usituone tunauza mashuka WhatsApp Status na Instagram ukadhani tulifeli darasani.Sisi ndio wale tuliokuwa kwenye Top 10 ...
29/10/2021

Usituone tunauza mashuka WhatsApp Status na Instagram ukadhani tulifeli darasani.

Sisi ndio wale tuliokuwa kwenye Top 10 ya darasa enzi za shule ila mtaa umetuamrisha tupite huku.

Tumeamua kutafuta biashara halali za kufanya badala ya kumsubiria ajira ambae sasa hivi amekuwa sawa na binti mzuri anae panda dau la mahari ya kumuoa.

Siku hizi wanataka mpaka tuwe na mafunzo ya JKT ili kumuoa binti ajira na wanasema k**a tuna miaka 30 huyu binti hatumuoi. Tuacheni tuuze mashuka, viatu, simu, vipodozi. Ila sisi ndio wale Top 10 wa darasa.

28/10/2021

Ndugu zako walikuambia maneno gani ya kukatisha tamaa ulipoanza biashara yako ya kwanza?

27/10/2021

Ulipo hitimu chuo kikuu ilikuchukua miaka mingapi kupata ajira inayo endana na taaluma yako? Au uliamua kujitosa kwenye biashara?

26/10/2021

Siku ukistaafu kazini utafanya shughuri gani ambayo itaendelea kukupa kipato endelevu.

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Shule ya Biashara-SB posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share