Mbunda Amosi Global Ltd.

Mbunda Amosi Global Ltd. Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Mbunda Amosi Global Ltd., Consulting Agency, Dar es Salaam.

13/06/2017

"Unless you change how you are, you will always have what you've got." —

15/03/2017

JE WAJUA????

Ili uweze kukipata/kuyapata hayo unayoyahitaji lazima upunguze kulala (masaa yasizidi 8)

Ni lazima ufanye kazi kwa muda usiozidi masaa 8.

Ni lazima uyatumie vizuri masaa 8 yaliyobakia katika mambo mazuri ya kukuzalishia yaani yakuingizie chochote mfukoni sio kinyume chake.

Ni lazima ukubali kuachana na marafiki ambao uko nao mpaka sasa ambao kiuhalisia ndio waliokufikisha hapo ulipo.

Ni lazima ufikirie nje ya box yaani mawazo yako yasiishie tu ndani ya box au ni lazima utoke katika comfort zone.

Ni lazima urefresh/uscan ubongo wako ili uweze kuingiza vitu sahihi na hivyo ambavyo havikujengi vikose nafasi kabisa.

Ni lazima ukubali kufundishika na kuambatana na watu sahihi wanaokupa changamoto za kimaendeleo za kukutoa hapo ulipo kwenda hatua nyingine sio Wa kukurudisha nyuma.

Ni lazima uwe na watu ambao kweli ukifanikiwa kutokana na juhudi zako wanakupongeza sio watu ambao kila kukicha ni kukusema Mara free mason Mara mchawi nk

Ni lazima ukubali kuumia ndipo ufanikiwe usipoumia hadi machozi yakutoke kufanikiwa itabaki kuwa stori tuu.(No pain No Gain).

Ni lazima ukubali kutoa ili upate maana usipotoa hupati chochote....kumbuka mkono unaotoa ndio unaorudishiwa....

Ni lazima ufanye kitu ambacho kinakupa matokeo ya 100% endapo utatoa juhudi za 100%.

Ni lazima ukubali kufanya maamuzi sahihi ingawa hapa kila mtu maamuzi anayoyafanya kwa upande wake ni sahihi nadhani kuna wachache wameelewa na wengi hawajaelewa namaanisha nini.

Amua kuamua sasa....hatima ya maisha yako ipo mikononi mwako na maamuzi utakayoyafanya leo ndio yataamua maisha yako kesho yaweje....

14/03/2017

Ukipewa siku mpya ni jambo la kumshukuru Mungu, fanya kitu fulani usikubali ipite tu bure, k**a jana iligoma Leo jaribu tena.

Unaweza ukawa unafungua mlango pengine kitasa na ufunguo ni tofauti, kaa tafakari namna ya kufanya kitu kiwezekane. Hebu jaribu Leo tena na ufunguo mwingine,

Usikubali ujikatishe au wakukatishe tamaa watu, amini inawezekana maadamu tumepata neema ya uzima na afya, inawezekana kufanyika

Anza siku yako ukiwa na shauku ya kuitumia vizuri kila dakika kutimiza majukumu yako, inawezekana kabisa, jaribu Leo

Inawezekana unafanya vizuri sana lakini hupati matokeo mapya mambo yanakuwa yale yale kwasababu unafanya kwa mazoea."Hat...
01/03/2017

Inawezekana unafanya vizuri sana lakini hupati matokeo mapya mambo yanakuwa yale yale kwasababu unafanya kwa mazoea."Hatufanyi vitu vya tofauti, tunafanya vitu vilevile lakini kwa tofauti"

K**a unachokifanya kuna mtu mwingine anaweza kukifanya kabisa yaani sawa sawa na wewe ujiangalie vizuri sana.
Inawezekana biashara moja wakaifanya watu wengi na baadhi yao wakapata matokeo bora yaani mafanikio na wenginewasione mabadiliko yeyote hii inasababishwa na ufanyaji.

K**a hupati matokeo angalia namna unavyofanya, wenzako waliofanikiwa wanafanyaje?
Kuna kitu gani ambacho kinakutofautisha na wengine?

Utofauti wako ndio unaleta maana ya kile unachokifanya. K**a hakuna tofauti unachokifanya kinakuwa cha kawaida tu.Usikubali kufanya vitu kwa mazoea kabisa. K**a unataka mafanikio anza kubadilika. Huu ni mwezi wa pili wa mwaka huu namara nyingi kadiri tunavyosongambele kuingia katikati ya mwaka ndipo watu huanza kuacha yale waliyosema watafanya.

Inawezekana na wewe umeshaanza kurudia hali yako yamazoea. Hata kusoma hutaki tena. Kununua kitabu unaona ngumu sana. Yaani unataka vitu virahisi tu uletewe hapo mdomoni ule.Mafanikio yanahitaji watu walioamua kufanya vitu vya tofauti.

Aliegundua simu janja (smartphone) sio mwanzilishi halisi wa simu bali ni mojawapo ya watu waliofikiria kwa tofauti na wakaleta mapinduzi haya tunayoyaona. Sasa ni kazi kwako pia kuangalia hapo ulipo na kile unachokifanya ni kwa njia gani unaweza kufanya kwa tofauti naukaleta mapinduzi?

Mazoea yameharibu mahusiano na ndoa nyingi sana pale mtu anapoona sasa tayari nimeshampata hawezi kuniacha tena na kisha akaanza kusahau yale ambayo alikua anayafanya yakasababisha akaoa au akaolewa. Inawezekana mtu alikubali kuwa na wewe kwasababu ulikua una vitu Fulani unafanya anafurahi sasa baada ya kuwa pamoja umejisahau hufanyi tena yale uliyoyafanya mwanzoni.

Mazoea yameua biashara nyingi sana, mtu anakaa dukani anasubiria mteja aje anunue. Dunia ya sasa inabadilikka umejipangaje kumfata mteja kule alipo? Kuna wageni wangapi wanaingia kwenye mji wako kila siku? Hawa wateja ungeweza kuwajulisha kabla hawajaja kwamba una duka la kitu Fulani hapo ulipo. Wakija wanakuja kununua.

Endelea kushangaa tu sasa hivi dunia inabadilika acha mazoea. Haijalishi biashara ni ndogo kiasi gani k**a una lengo la kufikia mafanikio makubwa acha kufanya kwa mazoea badilika.

MAISHA YA MAZOEA NI MABAYA SANA NA YANAWAFANYA WATU WAWE WAKAWAIDA ACHANA NAYO HARAKA SANA.

Consulting agency

Failure is not a FINAL result. It’s simply practice - its an opportunity for you to learn and GROW. If you don’t fail, y...
27/02/2017

Failure is not a FINAL result. It’s simply practice - its an opportunity for you to learn and GROW. If you don’t fail, you have no chance at ever succeeding. So, remember, when you fall, when you fail, dust yourself off and get back in the game.

Consulting agency

24/02/2017
23/02/2017

Consulting agency

THE FUTURE BELONGS TO THOSE WHO PREPARE FOR IT TODAY.Fanya kazi kwa bidii sana sasa, usisubilie kesho. Najua umeisha ham...
23/02/2017

THE FUTURE BELONGS TO THOSE WHO PREPARE FOR IT TODAY.

Fanya kazi kwa bidii sana sasa, usisubilie kesho. Najua umeisha hamasika vya kutosha, anza kuzielekea ndoto zako. Tatizo la watu wengi tunaishia kusoma makala za hamasa kisha tunatamani tuendee kusoma kila mala bila kuchoka. Najua umejaza vitabu na majrida ya kutosha ndani. Pia utakuwa umesikiliza na kutazama video za hamasa za kutosha kiasi kwamba hutamani ziishe.

Swali la kujiuliza , je izo hamasa zimekusaidiaje kutimiza kile unachotamani kufanya au kuwa?

Wakati huu wa HAPA KAZI TU, ni kufunika makala za hamasa na kuzima video za hamasa kisha kuanza kufanya kwa vitendo.

Ukikaa kusoma na kusikiliza au kutazama hamasa utabaki apoapo. maana utaishia kutamani kufanikiwa ukiwa umekaa chini na kusoma makala na video za hamasa.

Nyanyuka sasa na anza kufanyia kazi hamasa zako kwa vitendo.

Consulting agency

Umaskini wa mawazo ni mbaya sana, namainisha mtu anakosa yale mawazo sahihi ya kujenga. Hapo ndipo utagundua tofauti kat...
23/02/2017

Umaskini wa mawazo ni mbaya sana, namainisha mtu anakosa yale mawazo sahihi ya kujenga. Hapo ndipo utagundua tofauti kati ya anayetumia maarifa na ujuzi alionayo na yule ambaye alipata maarifa na ujuzi na hataki kutumia kwa sababu hajaoni kuwa hayo maarifa na ujuzi alionayo ni wa thamani sana.

Pia umaskini huu wa mawazo unamfanya mtu hata asione fursa sahihi ambayo inaweza kumsaidia akatimiza ndoto na malengo yake au fursa sahihi ambayo inaweza ikabadilisha maisha yake.

Mtu anayeuishi umaskini wa mawazo uwa anaukomo wa kupanga malengo yake na kufiria, hawezi kufanya maamuzi sahihi siku zote, na pia hawezi hata kuona mbali ( not having vision) juu ya ndoto zake.

Naomba utambue mtu ambaye hajui atokako hata anakoenda hawezi kukujua.

Je umewahi kujiuliza muda mwingine hauoni fursa kwa sababu mawazo yako ni ya kimaskini?

Anza leo kubadilika na maisha yako yatabadilika

By Amosi Mbunda

Consulting agency

20/02/2017

KWA NN WAAJIRIWA WENGI HUWA NI MASIKINI ? jibu hilihapa

Umaskini ndani ya kundi la wasomi unazidi kuingia kwa kasi ya ajabu kadili siku zinavyozidi kwenda. Kundi la watu ambao wako kwenye hatari kubwa zaidi ni hasa wale walioko kwenye “ajira”. Ukweli ni kwamba watu wengi walioko kwenye ajira, kitu pekee wanachouza ili kupata kipato ni “nguvukazi” tena ambayo bado ni “ghafi”.

Uzoefu unaotokana na tafiti zilizofanywa, unathibitisha kuwa zipo sababu nyingi zinazosababisha waajiriwa na hasa wasomi wengi kuwa maskini. Lakini kubwa zaidi ni utamaduni wa wasomi kuendelea kuuza nguvukazi ikiwa bado ni “ghafi” (nguvukazi ambayo haijachakatwa).

Katika ulimwengu wa “uwekezaji” nguvu kazi ghafi ni mtaji muhimu sana, ambao ukichanganywa na mitaji mingine k**a vile mashine, una uwezo wa kuzalisha bidhaa na huduma zenye thamani kubwa kwa watu wengine.

Ukiuza nguvukazi ghafi unakuwa umeuza “mtaji” wako: Waajiriwa wengi wanaendelea kukumbwa na adha kubwa ya umasikini kutokana na kushindwa kutambua ukweli kwamba mara nyingi kwenye maisha ya ajira wamekuwa wakifanya zaidi biashara ya kuuza mtaji walionao (nguvukazi) kwa matajiri wenye hitaji la mitaji.

Ikumbukwe kuwa, ili uweze kuzalisha bidhaa na huduma unahitaji mitaji ya aina mbalimbali ikiwemo nguvu kazi ghafi. Ndiyo maana matajiri wengi wanapendelea zaidi kununua mitaji kwa ajili ya kuzalisha bidhaa na huduma, ambazo huwapatia faida kubwa sana.

Katika biashara yoyote duniani, kuuza mtaji ni kufirisika jumla. Kwahiyo, umasikini tulionao umetokana na kuuza mtaji wetu kila siku tunapotumikia ajira zetu. Kwa maana nyingine waajiriwa wengi wanafirisika kila siku ya pale wanapokwenda kazini.

Watu wanaouza zaidi nguvu kazi ghafi wanabaki kuwa maskini kutokana na ukweli kwamba thamani ya nguvu kazi ghafi huwa ni ndogo sana, kwasababu inapatikana kwa wingi na haina usumbufu kuipata.

Kwa mfano: ukijifanya kutoza bei kubwa nguvu kazi yako; waajiri wengi watakukimbia na chapuchapu watapata watu wengine wenye kuuza nguvu kazi ile ile kwa bei nafuu sana.

Hivi ndivyo unavyouza nguvu kazi ghafi: Unauza nguvu kazi ghafi pale unapotumia nguvu yako kufanyakazi ya kuzalisha bidhaa na huduma ambazo siyo mali yako bali ni mali ya mtu aliyekuajiri (mwajiri).

Unahitaji kufahamu kuwa, mwajiri amekuajiri ili umpatie (umuuzie) nguvu kazi ambayo ni mtaji wa kuzalisha bidhaa na huduma ambazo ni mali yake binafsi.

Kwakuwa bidhaa zinazozalishwa ni za thamani kwa watu wengine, basi ni wazi kwamba watu hao watampatia pesa mwajiri wako ili kupata bidhaa; LAKINI hawatakupatia pesa wewe, kwasababu wewe unayo nguvu kazi peke yake, ambayo siyo hitaji muhimu kwa wateja wenye pesa zao.

Ukiuza nguvukazi ghafi unauza “muda” wako: Kwakuwa umeajiriwa kwa madhumuni ya kutoa nguvu kazi kwa mwajiri wako, basi thamani yako inapimwa kwa kuangalia muda unaoutumia kufanya kazi.

Ili uweze kulipwa ni lazima kila siku ufike kazini na kusajiri muda wako. Usipoonekana kazini hakuna malipo yoyote, kwasababu muda wako utakuwa hujauwekeza kwa mwajiri.

Kwahiyo, unapouza nguvu kazi ghafi basi ujue umeuza “muda” na binadamu wa kawaida hawezi kufanya kazi zaidi ya masaa nane kwa siku. Masaa yote haya unafanya kazi bila kupumzika na kuzalisha vitu vyenye thamani kubwa kuliko mshahara unaolipwa na mwajiri wako.

Haijalishi, thamani ya vitu vilivyozalishwa ni kubwa kiasi gani, mshahara wako unaolipwa unaendelea kubaki pale pale kila mwezi. Hali hii ndiyo inakufanya wewe mwajiriwa kukosa muda wa kufanya vitu vyenye kukuletea faida kubwa na mafanikio maishani, na hivyo kuzidi kuwa maskini kadiri umri wako unavyoongezeka.

Ukiuza nguvukazi ghafi huna cha kurithisha familia yako: K**a unauza nguvukazi ghafi siyo rahisi kuirithisha kwa watu wako wa karibu, kwasababu nguvukazi k**a ilivyo haihamishiki kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. K**a kitu hakihamishiki ni vigumu pia kukibadilisha kwa urahisi kuwa pesa.

Hali hii inazidi kutukumba wasomi na waajiriwa waliowengi kutokana na ukweli kwamba unakuta umeajiriwa kwenye kampuni kubwa na una cheo kikubwa lakini ukifukuzwa au kufariki, haitokei mke au mtoto wako akapewa nafasi k**a uliyokuwa nayo na wala familia haiwezi kutumia vyeti vyako vya elimu kuomba kazi.

Lakini k**a ungekuwa kwa mfano umeandika vitabu, hata ukifa hakimiliki ya kuendelea kuvichapisha na kuviuza inahamishiwa kwa warithi wako na wanaendelea kufaidi sawa na wewe ulivyokuwa ukifaidi.

Ukiuza nguvukazi ghafi unapata hasara: Hasara kubwa unayoipata kutokana na kuuza nguvu kazi ni pale unapoishia kuuza kitu kimoja tu! Nacho ni nguvu kazi.

Hali hii inakubana kiasi kwamba unajikuta unalazimika kumtegemea mteja mmoja ambaye ni “mwajiri” na inakuwa siyo rahisi kubadilisha mteja kadiri unavyotaka.

Endapo ukiamua kuchakata nguvukazi yako na hatimaye kuzalisha bidhaa na huduma za thamani ni rahisi kupata wateja wengi, ambao ndio huleta mapato makubwa.

Hasara nyingine unayopata pindi unapouza nguvu kazi ghafi ni kuendelea kubaki kwenye kundi la watu maskini ambao wanapata kipato hai (active income), yaani unapata pesa unapofanya kazi tu, ukiacha pesa hakuna. Endapo, ikitokea unaumwa au umesafiri basi ujue hakuna pesa itakayoingia.

Ndiyo maana unakuta mtu ni tajiri leo kwasababu anafanya kazi ya kibarua, lakini baada ya muda mfupi unakuta ni maskini na kwa waajiriwa ni hivyo hivyo wanakuwa na pesa wakiwa bado kazini LAKINI wanapostaafu ajira wanarudia kwenye hali ya umaskini jambo ambalo huwafanya watu wengi kufa miaka michache baada ya kustaafu.

Washindi dhidi ya umaskini ni wale walioamua kuchakata nguvu kazi yao: Ukweli ni kwamba kila mchakato wowote lazima utoe matokeo. Matokeo ya kuchakata nguvu kazi ghafi ni “bidhaa au huduma” zenye thamani kubwa kwa watu wengine.

Kitendo cha kuchakata nguvu kazi kinatokana na matumizi ya nguvu ya akiri pamoja na nguvu ya mwili kwenye rasilimali k**a ardhi, maliasili, ujuzi, pesa n.k, kwa lengo la kupata mali au bidhaa kwaajili ya watu wengine.

Ukishapata bidhaa zenye thamani (manufaa) kwa watu wengine, basi mara moja watakuletea pesa ili kujipatia bidhaa na huduma muhimu kutoka kwako. Kadiri utakavyotengeneza bidhaa nyingi na zenye thamani kubwa ndivyo utakavyopata pesa nyingi ambayo haina kikomo.

Ni wakati sasa tuamke na tujibidishe sana kwa kuandaa mazingira yatakayotuwezesha hasa sisi wataka mafanikio kuuza “matokeo” ya nguvu kazi badala ya utamaduni wa sasa wa kuuza nguvu kazi ghafi.

Ukweli ni kwamba, unapokuwa mtu wa kuuza matokeo ya nguvu kazi ambayo ni bidhaa na huduma mbalimbali, tayari unakuwa umemaliza kazi, kinachofuatia ni kuendelea kuuza bidhaa hizo na wakati huo huo unakwenda kuwekeza muda wako huo kwenye kuzalisha vitu vingine, huku akiendelea kufaidi matunda ya kazi aliyoifanya mwanzo.

Kwa watu wote na hasa waajiriwa tunaotaka mafanikio makubwa, ni lazima kila mmoja wetu ajiwekee tarehe ya mwisho ya kuacha kuuza nguvu kazi ghafi.

Kila mmoja akifikia tarehe yake ya mwisho kuuza nguvu kazi ghafi, mara moja aanze kujikita katika kubadili nguvu ya akiri na hisia kuwa bidhaa na huduma zenye kuwa suruhisho la kudumu kwa matatizo na changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wengine.

Kwakuwa utazalisha bidhaa na huduma zenye kuwa na manufaa makubwa kwa watu wengine, basi na wao watakupatia zawadi ambayo ni pesa, ili kujipatia kila kilicho bora kutoka kwako. Tukiweza kufanikisha azima hii, basi tutatajirika kutokana na ukweli kwamba watu wengi kwasasa wanataka bidhaa na huduma ambazo ni suruhisho ya changamoto zao.

Wateja ni wengi ambao wako tayari kununua kila kitu kitakachozalishwa ilimradi kina thamani kwao, kwa hiyo soko ni kubwa. Nchi yetu inapokaribia kuingia uchumi wa kati, mahitaji ya bidhaa na huduma zitokanazo na nguvu ya akiri/fikra zitazidi kuongezeka.

Bidhaa zenyewe ni k**a vile muziki, sanaa, vitabu, program za mafunzo ya ujasiriamali/biashara/afya/kilimo/majengo pamoja na machapisho juu miongozo mbalimbali ya uwekezaji katika mambo ya utalii, uwindaji, gasi, mafuta, madini, kilimo n.k.

Uchumi wa watanzania ukizidi kuongezeka na idadi ya wasomi ambao ndio wahitaji wakubwa itazidi kuongezeka huko tuendako ~ Kwa hiyo ewe mtanzania mwenzangu, anza kuchukua hatua leo, wakati ni sasa.

Nitafute kupitia hii namba 0763232431 kujifunza zaidi ujasiriamali na biashara

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mbunda Amosi Global Ltd. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share