13/05/2023
Jambo ambalo mara zote huwa nasisitiza kwa watu wote ninaowafundisha mafunzo haya ya kibiashara ni kwamba,kuna utofauti kati ya "anayekutafuta tu kwa simu baada ya kuona umepost bidhaa au huduma yako na akaamua kuulizia tu bei ya bidhaa au huduma yako" na "MTEJA."( hawa ni watu wawili tofauti.
Mteja ni yule mtu anayekuulizia bidhaa au huduma yako na huku kweli anaihitaji bidhaa hiyo na huduma yako hiyo
Hivyo, mara zote kumbuka kuwa"sio kila anaye kutafuta na kuanza kuulizia kuhusu bidhaa au huduma yako ni mteja wako lakini wakati huohuo mteja wako anaweza kuwa yule aliyekuulizia bidhaa au huduma yako" ( bila shaka hili umelipata na kulielewa kisawasawa.)
Narudia kwa msisitizo,sio kila anayekutafuta kuulizia bei ya bidhaa au huduma yako ni mteja
Bali wengine huwa si wateja bali wasumbufu tu na wakatishaji tamaa wazuri tu na hivo ukishamtambua sio mteja wako unaachana naye ili nguvu na muda wako visiishie kwake bali nguvu hizo uzielekeze kwa wateja wako sahihi.
Na sio kila mtu lazima awe mteja wako na ukilitambua hili, ukikutana na rejection yoyote( kukataliwa kwa bidhaa au huduma yako) kutoka kwa aliye kutafuta kuulizia bidhaa au huduma yako na ukajitahidi sana kumhuhudumia na bado asinunue kwako, haitakufanya ujisikie vibaya bali moja kwa moja utaelewa huyo atakuja kuwa mteja wako wa siku zijazo na hivyo utaendelea kutengeneza ukaribu naye( akiwa na mtazamo chanya) na akiwa na mtazamo hasi, unaachana naye ili asikupotezee muda wako bure bali muda wako uelekeze ku deal na wateja wako sahihi.