21/09/2025
UNAIKUMBUKA HII HADITH?
Nimei copy toka kilwa yetu
Wanyama wote wa pori walikumbwa na ukame,Hakuna maji mito yote ilikauka.
Wanyama wote wakaitisha kikao wachimbe kisima wapate maji ili kunusuru maisha yao.
Wanyama wote porin walifika ila sungura hakufika.wakajadili kisima kichwimbwe,Wakakubaliana asiechimba hatopata maji.Tembo akachaguliwa kuwa mwenyekit na msimamiz wa shughuli zote,Kazi ikaanza,kisima kikakamilika kikaanzakutumika.
Ila kilichowashangaza wanyama kila siku huwa wanakuta maji yamechafuka mno,wakabain kuwa sungura ambae hakushrikiana nao ndie huoga kisiman na kuchafua maji.
Wakamchagua kobe alinde kisima,sungura alipokuja aliingia na kuvura maji kobe mwenda pole hakuwa na mwendo wa kumfukuza sungura.Kobe akashindwa kazi.akachaguliwa fisi,Nae akadanganywa asali kisha sungura akazama kisiman na kuchota maji kisha kuchafua.
Akachaguliwa Simba mfalme wa msituni,Sungura alipokuja kisiman alimdanganya simba amsuke misuko.
kumbe sungura alimsuka misuko simba na kuifungia kweny mti mkubwa uliokuwa kando ya kisima,kisha sungura akazama kisiman na kuchezea maji,simba alipostuka ili amkamate akajikuta hawez kutoka alipo.