Kwaheri umasikini, mali ipo kitabuni

Kwaheri umasikini, mali ipo kitabuni Therefore the goals of this page is to help people from zero to hero economically.

The name" Kwaheri umasikini, mali ipo kitabuni " generalised all Tips in business activities which can help people to know the best ways on how to become a millionaire.

UFAFANUZI KUHUSU MAANA YA UREMBO NA VIPODOZIBiashara ya urembo na vipodozi ni kitu kimoja kwani lengo la mtu kutumia vip...
06/05/2021

UFAFANUZI KUHUSU MAANA YA UREMBO NA VIPODOZI

Biashara ya urembo na vipodozi ni kitu kimoja kwani lengo la mtu kutumia vipodozi ni ili apendeze au kuwa mrembo. Hivyo basi unaposema biashara ya bidhaa za urembo unakuwa unamaanisha vipodozi na vitu vyote vinavyo husiana na watu kupendeza au kuwa katika hali ya usafi na unadhifu.

Hata hivyo kuna baadhi ya watu huweka biashara ya urembo katika kundi lake na biashara ya vipodozi katika kundi lengine kulingana na wanavyoona. Mara nyingi watu hawa huwa wanahusisha urembo na vitu vya kuvaa k**a vile hereni, pete, bangiri, mikufu, nywele za bandia, kucha na kope za bandia. Huku wakihusisha vipodozi na bidhaa zote za ngozi, nywele na manukato k**a vile Cream, losheni, dawa za meno, Pafyumu, sabuni, shampuu na poda.

Lakini kitalamu vipodozi ni kitu chochote kile kinacho weza kutumiwa katika kufanya muonekano wa mtu uwe wa kuvutia zaidi au kuwa na harufu nzuri. Kwa hapa kwetu Tanzania na duniani kote vipodozi hujumuishwa ndani ya kundi kubwa la bidhaa za afya( Health care products ). Biashara ya vipodozi ni moja kati ya biashara zinazodhibitiwa kisheria ( regulated business ) na usimamizi wa biashara ya bidhaa hizi kwa Tanzania bara unafanywa na Mamlaka ya chakula na dawa ( TFDA ).

K**a ulikuwa hujui basi biashara ya urembo na vipodozi ni moja kati ya biashara kubwa duniani ambayo inaingizia watu mamilioni ya pesa kila kukicha. Kwasasa mahitaji ya bidhaa za vipodozi yapo juu sana tofauti na vipindi vya nyuma. Nadhani ukiondoa biashara ya chakula basi biashara ya urembo na vipodozi inashika namba mbili duniani kwa kupanda kwa kasi. Sidhani k**a kuna binadamu leo hii duniani anaweza akajitokeza mbele za watu na kudai hatumii kipodozi cha aina yoyote na k**a yupo basi hana tofauti na wanyama wanaoishi porini.

Narudia tena biashara hii ya urembo na vipodozi ni moja kati ya biashara zinazoenea kwa kasi ya ajabu hapa nchini, karibu kila mtaa huku mjini huwezi kupita hatua chache bila kukutana na duka la vipodozi. Kwa taharifa yako tu biashara ya vipodozi ni biashara ambayo soko lake ni kubwa sana na linaendelea kukua siku hadi siku sasa wewe endelea kuzubaa na kushangaa shangaa mataa tu.

Nakuibieni siri tu k**a mlikuwa hamjui basi biashara hii ya urembo na vipodozi unaweza kuanzisha na mtaji wowote ule haijarishi unamtaji mdogo au mkubwa unachotakiwa ni kuwa mjuzi na mbunifu katika kuindesha na kuisimamia biashara yako. Kwa bahati nzuri biashara hii inaitaji ujuzi kidogo tu katika usimamizi na uendeshaji wake.

Ni ujuzi gani huo ambao unahitajika ili niweze kusimamia na kuendesha vyema biashara yangu ya urembo na vipodozi? Kuwa na mimi katika kipindi kijacho ili uweze kufahamu zaidi.

HITIMISHO

Mwisho wa kipindi hiki ndio mwanzo wa kipindi kingine. Tukutane hapo kesho ili tuweze kuliendeleza gurudumu la maendeleo yetu mbele. Nawaombeni kila mtu baada ya kusoma makala hii hapo alipo kwanafasi yake ainue mikono yake juu kisha amwambie Mungu maneno haya" Asante Mungu kwa kwenda kubadilisha maisha yangu kupitia biashara hii ya urembo na vipodozi🙏🙏🙏".

ZINGATIA

Usisahau kufollow ukurasa huu iliuweze kuwa karibu kabisa na Uncle Rama kwa kuendelea kupata masomo mengi zaidi yanayo husu biashara. Pia usisahau kushare elimu hii, k**a si wewe basi inaweza kumsaidia ndugu, rafiki au jamaa yako.

Mimi ndugu yenu kipenzi RAMA WA KITABUNI

@ Uncle rama

BIASHARA YA UREMBO NA VIPODOZIKuna mambo mengi sana ambayo tunakwenda kujifunza kuhusu biashara ya urembo na vipodozi ku...
05/05/2021

BIASHARA YA UREMBO NA VIPODOZI

Kuna mambo mengi sana ambayo tunakwenda kujifunza kuhusu biashara ya urembo na vipodozi kuanzia A-Z ili tutakapomailza darasa letu basi tupate watu wakwenda kuthubutu na hatimae kusonga mbele katika nyaja hii. Mambo ambayo tunakwenda kujifunza ni haya yafuatayo:

A. UFAFANUZI NA MCHANGANUO KUHUSU MAANA YA UREMBO NA VIPODOZI.

B. AINA MBALI MBALI ZA UREMBO NA VIPODOZI

C. AINA ZA UREMBO NA VIPODOZI AMBAVYO VINANUNULIWA SANA, VINAFAIDA KUBWA SANA SOKONI NA VINAPENDWA SANA NA WATUMIAJI

D. AINA ZA UREMBO NA VIPODOZI AMBAVYO UNATAKIWA KUANZA NAVYO K**A UNAMTAJI MDOGO.

E. SABABU MBALIMBALI ZINAZOPELEKEA ONGEZEKO KUBWA LA WATU KUTUMIA VIPODOZI( KWANINI WATU WANAPENDA KUTUMIA VIPODOZI AU KUJIREMBA)

F. SECTA YA BIASHARA YA UREMBO NA VIPODOZI TANZANIA.(UNDANI WA BIASHARA YA UREMBO NA VIPODOZI)

G. NAMNA UNAVYO WEZA KUNUFAIKA NA FURSA KUBWA ILIYOKUWEPO KATIKA SEKTA HII YA UREMBO NA VIPODOZI.

H. NAMNA YA KUANZISHA , KUSIMAMIA NA KUENDELEZA BIASHARA YA UREMBO NA VIPODOZI KWA MTAJI MDOGO

I. UTARATIBU AU MUONGOZO AMBAO UNAPASWA KUUFATA KABLA YA KUANZA BIASHARA YA VIPODOZI ( NAMNA YA KURASIMISHA BIASHARA YA VIPODOZI)

J. ENEO AU SEHEMU SAHIHI AMBAYO UNATAKIWA KUFUNGUA BIASHARA YAKO YA UREMBO NA VIPODOZI

K. SEHEMU AMBAYO UNAWEZA KUCHUKUA NA KUFUNGASHA MZIGO WAKO WA UREMBO NA VIPODOZI KWA BEI RAHISI SANA HAPA KWETU TANZANIA.

L. SEHEMU AMBAYO UNAWEZA KUCHUKUA NA KUFUNGASHA MZIGO WAKO KWA BEI RAHISI SANA KWA WALE WANAOSAFIRI NJE YA TANZANIA

M. CHANGAMOTO NA HASARA AMBAZO UNAWEZA KUZIPATA KATIKA BIASHARA YAKO YA UREMBO NA VIPODOZI NA NAMNA YA KUKABILIANA NAZO

N. KIASI CHA MTAJI AMBACHO UNATAKIWA KUANZA NACHO ILI UWEZE KUANZISHA BIASHARA YA UREMBO NA VIPODOZI

O. VITU VYA MSINGI AMBAVYO UNATAKIWA KUWA NAVYO ILI UWEZE KUANZISHA BIASHARA YA UREMBO NA VIPODOZI

P. MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA UNAPOKWENDA KUNUNUA AU KUUZA BIDHAA ZA VIPODOZI

Q. MBINU ZITAKAZO KUSAIDIA KUPATA NA KUONGEZA WATEJA WENGI ZAIDI WA UREMBO NA VIPODOZI KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII NA ENEO UNALOFANYIA BIASHARA YAKO

R. NAMNA YA KUFANYA UTAFITI YAKINIFU ILI KUJUA AINA YA VIPODOZI VINAVYO HUZIKA HARAKA KULINGANA NA WAKATI ULIOPO

S. ORODHA YA VIPODOZI VINAVYO TAMBULIWA NA MAMLAKAYA CHAKULA NA DAWA TANZANIA TFDA

T. ORODHA YA VIPODOZI VYENYE SUMU NA VILIVYO PIGWA MARUFUKU NA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA TFDA

U. MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI WA KUFUNGUA BIASHARA YAKO YA UREMBO NA VIPODOZI

ZINGATIA

Kamwambie ndugu, rafiki na jamaa yako kwamba somo la BIASHARA YA UREMBO NA VIPODOZI ndio kwanza limeanza bado jipya kabisa. Hivyo basi asisahau KUFOLLOW ukurasa huu wa kwaheri umasikini mali ipo kitabuni ili aweze kupata elimu mbalimbali kuhusu biashara.

Nawapenda sana na ndio maana nimeamua kuwapa elimu hii bure kabisa bila malipo yoyote, Mungu ndio atakaye nilipa. Wewe cha kufanya ni kufollow ukurasa huu na share ili kila mtu apate elimu hii.

Kuna baadhi ya watu wanadhani kuwa biashara ya urembo na vipodozi ni biashara ambayo inatakiwa kufanywa na wanawake tu peke yao. Kuanzia leo nendeni mkawaambie kuwa wanatakiwa kufollow ukurasa huu ili tuwasaidie kuondoa dhana potofu juu ya kufanya biashara ya urembo na vipodozi.

Mimi ndugu yenu kipenzi RAMA WA KITABUNI

@ Uncle Rama

Kutokana na maombi ya watu wengi kuomba nifundishe darasa la BIASHARA YA UREMBO NA VIPODOZI nimekubariana na wengi walio...
04/05/2021

Kutokana na maombi ya watu wengi kuomba nifundishe darasa la BIASHARA YA UREMBO NA VIPODOZI nimekubariana na wengi waliopendekeza. Sasa nendeni mkawaambie ndugu jamaa na marafiki zenu kwamba darasa letu linaanza soon hapa hapa kwenye page yetu pendwa ya kwaheri umasikini, mali ipo kitabuni. Unachotakiwa kufanya ni kushare na kulike kwa wingi ili kila mtu aweze kupata elimu hii.

ZINGATIA

Mafunzo haya ya biashara ya urembo na vipodozi ni bure kabisa hakuna ada yoyote itakayo tozwa kwa mfanyabiashara anaye taka kujifunza. Watu wote mnakaribishwa.

@ Uncle Rama

BARUA YA UCHUNGU SEHEMU YA KWANZAKwako kaka yangu mpendwa Chapombe, hujambo? Mimi huku ni mzima wa afya tele kwa hilo ni...
06/04/2021

BARUA YA UCHUNGU

SEHEMU YA KWANZA

Kwako kaka yangu mpendwa Chapombe,
hujambo? Mimi huku ni mzima wa afya tele kwa hilo ninamshukuru Mungu. Lengo la kukuandikia barua hii ni kukujulisha ya kwamba maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe mwenyewe.

Je wajua k**a ukinywa bia moja ni sawa na umekunywa tofari mbili za kujengea nyumba, ambapo kwa bei ya kawaida kabisa ya bia moja maeneo mengi hapa nchini kwetu ni inauzwa Tsh 2,500/=. Na bei ya tofari la nchi sita kwa maeneo mengi hapa nchini hususa ni mijini ni Tsh 1,300/=.

Hivi unajua endapo kila siku moja ukiwa unakunywa bia tano, maana yake ni kwamba kwa mwaka mzima wenye jumla ya siku 366 itakuwa umekunywa jumla ya bia 1,830 ambazo bia hizo ni sawa na pesa za Kitanzania 4,575,000/=.

Hivi unaelewa k**a ungekuwa umenunua tofari za kujengea nyumba yako ungepata jumla ya tofari 3,660 ambazo zinatosha kabisa kujengea nyumba ya vyumba vitatu, Seating room moja, Dining room moja, Jiko moja, Vyoo viwili( master na public ) pamoja na store.

Kaka yangu mpendwa Chapombe hesabu hiyo niliyoifanya hapo juu siyo hesabu yako, hapo nimefanya tu makadirio ya hesabu ya mtu anayekunywa angalau bia tano tu kwasiku. Sasa piga hesabu za bia ulizo kuwa unakunywa tangu mwaka hule wa 2007 nilipoanza kukujua kuwa unakunywa pombe kupindukia.

Kaka yangu mpendwa hapo sijataka kujua hesabu ya zile bia za offer ulizokuwa unawanunulia rafiki zako akina Jeni, Anna, Jonson na Eliza pale Corner bar, Sinza Africa sana. Sitaki kujua hesabu ya zile bia ulizokuwa unawanunulia wapambe wako akina Juma , Neema, Amina na Wine kule La chaaz bar.

Kaka yangu tangu mwaka 2007 hadi leo mwaka 2021 unakunywa bia tu huku unalala kibarazani, hivi unajua umesha kunywa nyumba ngapi? Si utakuwa umekunywa nyumba zaidi ya kumi kaka.

Kaka siku zote bahati ya mtu iko mikononi mwa mtu mwenyewe. Kumbuka unaingamiza bahati yako kwa mikono yako mwenyewe. Angalia usije ukamtafuta mchawi aliye kuroga maisha yako uzeeni panapo majaliwa. Mchawi wa maisha yako nenda ukamtazame kwenye kioo cha kujiangalia.

Nimekuandikia barua hii kwa makusudi huku nikiwa najua hata usiposoma wewe basi atasoma baba, mama na Dada zangu wenye akili k**a zako. Tafakari kisha chukua hatua, nakutakia maisha malefu na nakupenda sana kaka yangu kwasababu udugu ni adhina yetu.

Mimi mdogo wako mpendwa RAMA WA KITABUNI,

AKIBA NI NINI ?UTANGULIZINaanza kwa kutanguliza shukurani zangu za dhati zikuendee wewe Mungu mkuu na muokozi wa maisha ...
05/08/2020

AKIBA NI NINI ?

UTANGULIZI

Naanza kwa kutanguliza shukurani zangu za dhati zikuendee wewe Mungu mkuu na muokozi wa maisha yangu kwa kunipa usikuvu, akili na maarifa ya kuwatumikia watu wako bila kujali itikadi ya dini, chama wala makabila yao. Leo tutajifunza Akiba na faida ya kuweka akiba kwa malengo ya baadaye. Hapa tutaangalia kwa ufupi sana maana ya akiba alafu tutakwenda kwenye dhamila yetu halisi;

Tunapozungumza kuhusu AKIBA tunatakiwa kujua kuwa hii ni sehemu ya fedha unayohifadhi kutoka kwenye chanzo cha mapato yako. Chanzo cha mapato kinaweza kuwa biashara au kazi. Hii ndio maana halisi ya akiba.

FAIDA KUU ( 8 ) ZA KUWEKA AKIBA KWA MALENGO YA BAADAYE

Watu wengi wamekuwa wakifikilia kwamba ili kuweka akiba unatakiwa uwe na pesa nyinginza ziada, kitu ambacho si kweli. Lakini ukweli ni kwamba kuweka akiba ni maamuzi na mipango stahiki ya mtu. Hivi unakumbuka mara ngapi ulijaribu kuweka fedha katika njia unazozijua wewe na ukashindwa au ukazitumia kabla ya kutimiza malengo yako uliyo jipangia. Pengine haya yote huwenda yamekutokea kwasababu ya kutokujua umuhimu wa kuweka akiba. Sasa basi leo ninakwenda kukuelezea faida kuu 8 za kuifadhi fedha. Faida hizo ni k**a zifuatazo;

1. KUJIKINGA NA DHARURA
Dharura ni jambo ambalo hutokea bila ya taarifa. Kipindi cha dharura watu wengi hulazimika kuingia kwenye madeni wasiyo yatarajia kutokana na kutokuwa na akiba yoyote ya kujikimu kutokana na changamoto ya dharura iliyowafikia. Dharura inaweza ikiwa magonjwa, ajari , msiba na mengineyo. Hivyo kujiwekea akiba kutakuepusha na madeni wakati wa dharura.

2. HUONDOA HOFU NA KUKUPA UTULIVU WA AKILI
Unapokuwa huna akiba yoyote huwezi kuwa na utulivu wa akili. Kila wakati unakuwa na hofu na wasiwasi juu ya maisha yako, yani unakuwa mtu wa kujiuliza maswali tu, likitokea tatizo itakuwaje? au likitokea hitaji muhimu nitafanyaje?. Lakini unapokuwa na fungu lako la akiba huna haja ya kuwa na wasiwasi kwani unajua hata ukikosa pesa akiba yako ipo na itakusaidia.

3. INAKUPA UHURU WA KIFEDHA
Uhuru wa kifedha ni zaidi ya kuwa na pesa. Itakuwa akuna umaana wowote k**a utakuwa unamiliki mahela mengiiii alafu ukakosa uhuru wa kifedha. Uhuru wa kifedha ni kitendo cha mtu kuweza kufanya au kupata kile anachohitaji maishani bila kuvunja sheria au mipaka. Hata hivyo pesa ni muhimu sana kwenye swala la uhuru wa kifedha k**a tu pesa hizo zitaambatana na fikira sahihi. Kwa njia hii ya kujiwekea akiba utaweza kujiwekea msingi mzuri wa kifedha ambao ukiambatanishwa na fikra sahihi utakuletea uhuru wa kifedha.

4. INALETA NIDHAMU YA FEDHA
K**a nilivyo eleza huko mwanzo kuwa kuweka akiba sio lazima uwe na pesa nyingi bali haya ni maamuzi na mipango stahiki ya mtu mwenyewe. Hivyo basi kwa mantiki hiyo kuweka akiba kutakufaidisha sana kwa kukuwezesha kutumia pesa vizuri na katika mpangilio maalumu. Ikiwa unapata Tsh 5000 kwa siku, itakubidi utumie vizuri ili uweze kutenga fedha ya akiba. K**a huweki akiba utawezaje kutumia pesa vyema wakati hakuna hata sehemu ya akiba inayotakiwa kutengwa.

5. KUKUWEZESHA KUWAHI FURSA
Ni mara ngapi umekuwa ukisema au hata kusikia kwa watu wakisema kauli k**a vile, Ningekuwa na pesa ningenunua hiki, Ningekuwa na hela ningefanya biashara hii, Ningekuwa na pesa ningenunua kiwanja kile. Hii inadhihirisha kuwa watu wanakosa fursa mbalimbali kutokana na kukosa akiba ya fedha. Unapokuwa na akiba ya fedha ni rahisi kuwahi fursa mbalimbali zinazojitokeza kwenye jamii yako. Hivi unajua ukiwa na akiba ya fedha hata wazo la kuanzisha biashara linakuja lenyewe.

6. KUWEZA KUMUDU WANAOKUTEGEMEA
Akiba inamsaada mkubwa sana kwa watu wanaokutegemea. Ikiwa kuna watu wanaokutegemea k**a vile wazazi, watoto, ndugu, jamaa na marafiki ni vyema kuweka akiba ili uweze kuwa na fedha ya kukidhi mahitaji yao mara wapatapo na uhitaji. Kutokuweka akiba kutakufanya uhangaike huku na kule kutafuta fedha hata kwa mkopo ili kukidhi mahitaji ya wategemezi wako, k**a vile chakula, matibabu au hata ada za shule.

7. HUKUWEZESHA KUANDAA MALENGO YAKO VYEMA
Maandalizi sahihi ya kesho yako yanafanywa leo. Kuweka akiba kunasaidia kijiandaa kwa mahitaji ya kifedha ya baadaye. Mtu asieweka akiba mara nyingi hafikirii kuhusu kesho wala hana malengo kwa ajiri ya baadaye yake. Ili kujenga baadaye au kesho njema ni muhimu pia kuimarisha msingi wako wa kiuchumi kwa njia ya kuweka akiba.

8.HUKUWEZESHA KUFANYA MANUNUZI AU MIRADI YA GHARAMA KUBWA
Kuna baadhi ya manunuzi au miradi huwa inahitaji pesa nyingi sana ili kutekeleza. Maswala k**a ujenzi wa nyumba au ununuzi wa kiwanja ni baadhi ya mambo yanayohitaji fedha nyingi ili ukamilishe. Hivyo basi ukiwa na akiba utaweza kutekeleza mambo haya kwa urahisi zaidi kuliko ungefanya bila akiba.

HITIMISHO
Fedha ni jambo linahitaji nidhamu na busara ya hali ya juu sana. Vivyo hivo kuweka akiba ni swala linalohitaji kufanya maamuzi sahihi na upembuzi yakinifu ili uweze kutekeleza. Baada ya kusoma makala hii nimatumaini yangu hutopuuza tena swala la kuweka akiba. Hakikisha hutumii akiba yako hovyo pasipo kuwa na sababu ya msingi ili iweze kukusaidia sana mbeleni wakati wa uhitaji.

Mungu akazitunze na kuzilinda akiba zenu mlizojiwekea kwa malengo yenu ya baadaye k**a kitunzo na kilindo alicholindia maneno yake matakatifu,,, Ameeeen 🙏🙏🙏🙏

MASWALI
Tafadhari tuandikie maoni yako hapo chini kisha washilikishe wengine makala hii ili nawao wajifunze mengi kupitia ukurasa huu. Usisahau KU LIKE na KU SHARE ili kufahamu mengi zaidi kisha M TAG rafiki yako mpenzi mwambie anapitwa na mengi sana huku katika darasa letu la biashara, Ujasiriamali, Uchumi na fedha .

Nawapenda sana ,,,,,, I love you ,,,,,, Mmwaaaaaaa

@ Uncle Rama

TABIA NA SIFA ZA MJASIRIAMALI SEHEMU YA PILIUTANGULIZI Tutaendelea kuziangalia sifa na tabia za Mjasiriamali sehemu ya p...
04/08/2020

TABIA NA SIFA ZA MJASIRIAMALI

SEHEMU YA PILI

UTANGULIZI

Tutaendelea kuziangalia sifa na tabia za Mjasiriamali sehemu ya pili ili tuweze kujifunza zaidi. Katika makala iliyopita ya sifa za Mjasiriamali tulijaribu kuangalia sifa 5 muhimu na hapa tunakwenda kuangalia sifa nyingine 5 muhimu za Mjasiriamali. Ili uwe Mjasiriamali ni lazima uwe na sifa zipi? hili ni swali ambalo tunapaswa kujiuliza pindi tunapotaka kuwa wajasiriamali. Kuanzia leo mpaka unakufa unatakiwa kufahamu ili uwe Mjasiriamali bora ni lazima uwe na sifa zifuatazo:

1. KUFANYA KAZI KWA BIDII
Bidii ni msingi imara wa kufanikiwa kwenye jambo au shughuli yoyote. Mjasiriamali ni lazima awe na bidii na maarifa ya kile anachokifanya ili aweze kufikia malengo yake. Ikumbukwe kuwa Mjasiriamali yeyote mwajiri wake ni yeye mwenyewe, Hivyo basi ni muhimu kujituma na kufanya kazi na kufanya kazi kwa bidii bila kusukumwa na mtu yeyote ili kufikia malengo.

2. UWEZO WA KUONA FURSA
Mjasiriamali ni lazima uwe na jicho au uwezo wa kuona fursa katika jamii yako inayo kuzunguka. Mjasiriamali anatabia ya kutizama changamoto zinazojitokeza kwenye jamii yake na kuzitumia changamoto hizo k**a fursa kwake. Kwamfano sehemu unayokaa kuna changamoto ya upatikanaji wa huduma za kifedha kwa njia ya kielektroniki, k**a vile huduma za kibenki, Malipo ya umeme, malipo ya maji (dawasco) na utumaji fedha kwanjia ya simu( Tigo pesa , M pesa , Airtelmoney , halo pesa nk ). Hapa Mjasiriamali unatakiwa kuona changamoto hizo ni k**a fursa kwako kwa kuanzisha vibanda vya kutolea huduma hizo za kifedha na kujipatia kipato.

3. UWEZO WA KUTUNZA SIRI YA BIASHARA
Mjasiriamali ni lazima pia awe na uwezo mkubwa wa kutunza siri za biashara yake hasa kwa washindani wake. Hapa katika kutunza siri ya biashara Mjasiriamali anapaswa kuwa makini sana katika kuchagua wafanyakazi atakao saidiana nao kwenye biashara yake. Hakikisha unachagua wasaidizi ambao utakuwa una uhakika kuwa ni watunzaji wazuri wa siri za ndani ya biashara yako. Kwamfano k**a umefungua mgahawa wa chakula na mtu mwengine amekuja kufungua mgahawa wa chakula katika eneo hilo hilo ulilopo kumbuka huyo ndio mshindani wako. Basi hakikisha unatunza siri za ubunifu wako katika mapishi mbalimbali ambazo zinapelekea watu wengi kuja kula kwako. "Ficheni siri zenu kwani kuficha siri ndio mafanikio yenyewe" ( Sheikh Nurdin Kishki , Tanzania).

4. UWEZO WA KUONGOZA
Mjasiriamali ni lazima awe na uwezo wa kuongoza na kutoa maamuzi. Katika Ujasiriamali uongozi ni jambo muhimu sana ambalo kila Mjasiriamali anapaswa kuwa nalo. Mjasiriamali ni lazima aweze kusimamia na kuongoza biashara yake vizuri tena katika mpangilio maalumu wa uongozi bora. Pia ni lazima awe na uwezo mkubwa wa kuwaongoza na kuwasimamia wafanyakazi wake kwa kutumia mbinu bora za uongozi ili apate matunda kwa kile ambacho anakifanya.

5. UAMINIFU, UKWELI NA UWAZI
Uaminifu, ukweli na uwazi hii ndio sifa nguzo mama na sifa kuu kabisa ya Mjasiriamali yeyote ulimwenguni. K**a umewahi kuwasikia wajasiriamali wowote waliofanikiwa k**a akina Aliko Dangote wa Nigeria, basi mpaka wanakufa hawawezi kuicha sifa hii. Hii ndio sifa na tabia bora miongoni mwa tabia bora za Mjasiriamali. K**a Mjasiriamali ni lazima ufanye kazi yako katika mazingira ya Uaminifu, ukweli na uwazi ili upate wateja wengi. Ni lazima uwe mkweli na muwazi katika ubora wa bidhaa zako, Lazima uwe mkweli na muwazi katika upangaji wa bei ya bidhaa zako. Lakini pia ni lazima uwe mkweli na muwazi katika eneo maalumu ampapo wewe na bidhaa zako mnapatikana. Uongo ni sumu kali sana yenye kuua kwa haraka zaidi biashara yako, iepuke sumu hiyo.

HITIMISHO
Ni muhimu sana kufuatilia makala zangu na vitabu mbalimbali vinavyo husu biashara, Uchumi na Ujasiriamali. Hii itakujengea msingi imara katika biashara zako lakini pia utaweza kujua mabadiliko makubwa yanayotokea mara kwa mara kwenye biashara zako.

MASWALI
K**a umejifunza kitu kwenye makala hii basi usisite kutuandikia maoni , ushauri au maswali hapo chini. K**a kuna mtu anashida binafsi njoo inbox utasaidiwa. Nakupendeni sana, I love youuuuuuuu, Mmwaaaaaa

LIKE na SHARE page hii katika vikundi mbalimbali ili kila mtu apate elimu hii. M - TAG rafiki mwambie darasa la biashara, Uchumi na Ujasiriamali chini ya usimamizi wa Uncle Rama lina endelea.

@ Uncle Rama

HATUA 10 ZA KUZINGATIA WAKATI UNAFANYA UTAFITI KABLA YA KUANZISHA BIASHARA UTANGULIZI Kabla ya kuanza biashara ni vyema ...
02/08/2020

HATUA 10 ZA KUZINGATIA WAKATI UNAFANYA UTAFITI KABLA YA KUANZISHA BIASHARA

UTANGULIZI

Kabla ya kuanza biashara ni vyema kufanya utafiti kwanza. Je ni hatua gani za kuzingatia wakati unafanya utafiti kabla ya kuanza biashara? Hili ni swali ambalo unapaswa kujiuliza mwanzoni kabisa kabla hata ujaingia kwenye ulimwengu wa biashara. Leo naomba tuangalie hatua 10 muhimu za kufuata na kuzingatia wakati unafanya utafiti kabla ya kuanza biashara. Hatua hizo ni hizi zifuatazo:

1. WAZO LA BIASHARA
Katika kila wazo zuri la biashara ulilonalo jua kuna mamia ya watu wana wazo hilo hilo. Hapa unatakiwa ujiulize, Je ni aina gani ya biashara unataka kufungua, Je katika hiyo biashara kuna watu wangapi tayari wanafanya. Kuwa na wazo la biashara itakusaidia kujua mapema k**a utapata wazo jingine la biashara au utafanya biashara hiyo hiyo kwa kuitofautisha na watangulizi wako.

2. ENEO LA BIASHARA
Hapa unatakiwa kufanya utafiti wa kina ili kujua ni biashara gani inayofaa kwenye eneo hilo. Ni muhimu sana kufanya utafiti yakinifu ili kujua k**a wazo lako la biashara linaweza kufanikiwa katika eneo hilo. Hapa unatakiwa kujua, Je eneo hilo lina vyanzo vizuri vya uzalishaji, Je kuna rasilimali watu yani wafanyakazi na wateja, Je kuna taasisi za kifedha zilizo karibu nawe. Unatakiwa kujua kiwango cha kodi kwenye eneo hilo. Pia sio vibaya ukachunguza k**a miundo mbinu na teknolojia ni rafiki kwa aina ya biashara unayotaka kufungua.

3. UPATIKANAJI WA SOKO
Hapa ni muhimu kuangalia uhitaji wa soko kabla ya kuchagua wazo la biashara. Unapo angalia uhitaji wa soko hii itakusaidia kujua ni wazo gani la biashara ambalo litauzika. Usichague wazo kwasababu ni wazo lililokujia akilini au umeona wengine wanafanya, hapana bali unatakiwa kuhakikisha wazo lako linahitajika sokoni tena katika wakati husika.

4. WASOME WASHINDANI WAKO
Hakuna biashara ambayo unaweza kuianzisha ikawa haina washindani kwa asilimia 100%. Kila biashara huwa inawashindani wake. Na wewe unahitaji kuwa fahamu washindani wako ni akina nani? Wapo wapi? Wana nini ambacho wewe huna? Na wewe una nini ambacho wao hawana?. Kwahiyo kabla ya kuanza biashara hakikisha unazunguka maeneo yote ya karibu na wewe ili uweze kuwa soma washindani wako. Angalia mapungufu ambayo wanayo ili uweze kuyatumia mapungufu yao k**a ngazi ya wewe kuelekea kwenye mafanikio ya biashara yako.

5. FAIDA YA BIASHARA
Hakuna biashara ambayo inafanywa bila kuzingatia upatikanaji wa faida. Faida ndio kiini na sababu ya watu kufanya biashara. Wafanyabiashara wengi wanapoanza biashara hutegemea faida, lakini sio biashara zote zina toa faida kwa wakati. Hapa unatakiwa kuangalia ni biashara zipi unatakiwa kufanya ambazo zinaleta faida kwa wakati kulingana na eneo ulililopo. Kutambua faida ya biashara mapema kutakusaidia kujua aina ya bidhaa na bei ya bidhaa ambayo utatakiwa kuuza katika eneo ulilopo ili upate faida kwa wakati.

6. UPEKEE WA BIASHARA
Hapa mfanyabiashara unatakiwa kufanya utafiti wa kina juu ya kuangalia namna ya kuifanya biashara yako iwe ya kipekee zaidi katika eneo ulilopo. Hapa utachunguza ili kujua k**a biashara unayotaka kuanzisha inafanana na washindani wako. Hii itakusaidia kujua mapema namna ya Kuipa thamani biashara yako kwa kuiwekea ubunifu wa kibiashara. Ubunifu ambao utakufanya uwe na ushindani kwenye biashara yako, utakao kutofautisha wewe na washindani wako ili uweze kufika kwenye
kilele cha mafanikio yako.

7. MSIMU WA BIASHARA
Hapa mfanyabiashara unatakiwa kufanya utafiti ili kujua ni aina gani ya biashara ambayo inaendana na msimu uliopo. Kuna biashara nyingine huwa hazi athiriwi na msimu lakini unatakiwa kujua kuwa kuna biashara nyingine huwa zinaathiriwa na msimu. Kwamfano wakati wa kiangazi tena jua kali alafu upo kwenye mkoa k**a Dar es salaam yani joto lake huko ni halivumiliki, wewe unaenda kufungua duka la kuuza makoti ya kuzuia baridi hayo ni matumizi mabaya ya fedha. K**a mfanyabiashara unatakiwa kujua ni biashara gani ufungue kwenye msimu wa joto na biashara gani unatakiwa kufungua kwenye msimu wa baridi.

8. UZOEFU WA BIASHARA
Ni muhimu sana kufanya utafiti wa kuwajua watu mwenye uzoefu wa biashara ya aina yako ambao wamewahi kuifanya biashara k**a yako na wakafanikiwa. Kufanya hivyo kutakusaidia kupata uzoefu wa biashara unayotaka kuifanya na namna ya kuindesha pia kutakusaidia kuzijua changamoto zitakazo ikumba biashara yako na namna ya kukabiliana nazo.Hapa unatakiwa kuhakikisha unachagua watu sahihi watakao kuwa tayari kukupa siri za mafanikio yao bila kukuficha, watu watakao kuwa tayari kukupa elimu kila siku hasa katika kipindi cha miaka miwili ya mwanzo juu ya biashara yako, watu watakao kuwa tayari kukushika mkono kwa dhati pale utakapokuwa umejikwaa mpaka ufikie malengo yako, watu watakao kuwa tayari kukupa taarifa sahihi juu ya kukuonyesha njia ya wapi pa kukanyaga na wapi pa kukwepa ili ufikie mafanikio yako. Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu k**a itatokea umewapata watu k**a hao basi washikilie na uwakumbatie usije ukawapoteza, maana wengi wao walishakufaga kwenye vita vya pili vya dunia waliobaki ni wachache sana.

9. MUDA WA BIASHARA
Hapa mfanyabiashara ni lazima ufanye utafiti wa kujua muda sahihi wa kufungua biashara katika eneo ulilopo. Imezoeleka kuona biashara nyingi zinafunguliwa asabuhi na kufungwa jioni, lakini hutakiwi kukalili hivyo. Siku hizi biashara zimebadilika sana kuna maeneo mengine biashara zao zinafunguliwa jioni na kufungwa asabuhi pia kuna maeneo mengine biashara zinafanyika masaa 24 hii inatoka na wateja walivyo zoeshwa na wafanyabiashara. Hivyo unapaswa kuangalia eneo ulilopo wateja wao wengi wapo muda gani, kinyume na hapo kila siku wewe utakuwa ni mtu wa kupishana na wateja wako. Wakati wewe unaingia wenzio wanatoka wakati wewe unatoka wenzio wanaingia. Kwahiyo kuchunguza muda wa biashara kwa makini kutakusaidia kujua ni wakati gani wateja wanakuwa wengi na wakati gani wanapungua, pia itakusaidia kutengeneza mpangilio mzuri wa muda wa kuingia kazini na kutoka ili uweze kutengeneza faida kwa wakati.

10. ELIMU YA BIASHARA
Hapa mfanyabiashara unatakiwa kujichunguza na kujitathimini wewe mwenyewe juu ya elimu na uelewa wako kuhusu biashara unayotaka kuifungua. Kitu cha kwanza tunacho kuwa tunasikiaga kutoka kwa wafanyabiashara wanapokuwa wameanguka kiuchumi ni msemo wa ningelijua. Hii inaonesha wazi kuwa huyu mtu hakufatilia kwa makini biashara yake kabla ya kuianza. Ni muhimu sana kabla ya kuanzisha biashara kufuatilia biashara yako kwa kusoma makala na vitabu mbalimbali vinavyo husu biashara hiyo. Hii itakujengea msingi imara katika biashara yako lakini pia utaweza kujua mabadiliko makubwa yanayo tokea kwenye biashara yako usiku na mchana. Hivyo basi nasisitiza tena endelea kusoma makala zangu kila siku ili ujue ni mabadiliko gani yanayotokea kwenye biashara yako.

HITIMISHO
Fanya utafiti lakini jali muda. Sio unafanya utafiti miaka nenda rudi .Wenzako wameshaanza biashara zao tangu mwaka 1992 wewe mpaka leo mwaka 2020 bado unafanya utafiti tu, sasa sijui utakuwa unafanya utafiti wa kuanza biashara au utafiti wa kuumba dunia mpya. Muda haukusubiri, kuna biashara nyingine zinaenda na muda, ukizichelewa kuzifanya katika kipindi fulani cha muda itakuja kukugharimu sana baadaye.

Kwamfano k**a ulikuwa unafanya utafiti wa kufungua biashara ya huduma ya kibanda cha simu ili watu wawe wanapata huduma ya kupiga simu tangu mwaka 2002 mpaka leo hii mwaka 2020 wewe bado umeng'ang'ana na utafiti wako tu. Alafu unategemea mwaka huu ndio uanze biashara yako ya huduma ya kibanda cha simu. Kaka acha, hayo ni matumizi mabaya ya fikira, muda na pesa. Hivi ushangai dunia yote hii ilivyo kubwa lakini watu siku hizi wameamua wanatembea nayo kiganjani lakini wewe bado tu unataka uje na huduma yako ya mwaka 1960 huko. Watu watakushangaa sana. Badilika maisha hayakusubiri, fanya utafiti lakini jari muda

MASWALI
Je umejifunza nini kwenye makala hii , Tafadhari tuandikie maoni yako hapo chini , ushauli na maswali k**a yapo nitakuwa nasoma na kujibu papo hapo. K**a unashida binafsi nitafute tuzungumze. Nakupendeni sana I love youuuuuuuu , Mmwaaaaaaaaaa

LIKE na SHARE page hii k**a umependa masomo yangu kisha M - TAG rafiki mwambie hajachelewa darasa la biashara, uchumi na Ujasiriamali linaendelea huku .

@ Uncle Rama

TABIA NA SIFA ZA MJASIRIAMALI SEHEMU YA KWANZA UTANGULIZI Naomba hapa tujifunze tabia na sifa za mtu anayefaa kuwa Mjasi...
27/07/2020

TABIA NA SIFA ZA MJASIRIAMALI

SEHEMU YA KWANZA

UTANGULIZI

Naomba hapa tujifunze tabia na sifa za mtu anayefaa kuwa Mjasiriamali au anayetaka kuwa Mjasiriamali. Katika karne hii tuliyokuwa nayo Ujasiriamali ni chaguo muhimu sana ili kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kujipatia kipato. Leo hii katika jamii zetu wapo Wajasiriamali wengi waliofanikiwa na pia wapo wengine hawajafanikiwa.

Ili uwe Mjasiriamali bora ni lazima uzifahamu na kuziishi kwa kina sifa na tabia za Mjasiriamali. Ni vigimu sana kuwa Mjasiriamali bora wakati hauna sifa za kuwa Mjasiriamali. Ukimuona Mjasiriamali yeyote kwenye jamii yako amefanikiwa basi kwa hakika ujue anazifahamu na kuziishi sifa za Mjasiriamali bora.

Zipo sifa na tabia nyingi sana za Mjasiriamali, nikisema nizi orodheshe zote kwa pamoja tutakesha. Lakini leo naomba tuangalie chache miongoni mwa hizo. Sifa na tabia za Mjasiriamali ni k**a zifuatazo:

1. MWENYE MALENGO

Malengo ni muongozo wa kukuwezesha kufanikisha jambo lolote katika shughuli yako. Mjasiriamali ni lazima awe na malengo yaliyo nyooka na yanayoeleweka. Kuwa na malengo ni sifa muhimu ambayo kila Mjasiriamali anapaswa kuwa nayo. Bila malengo utafanya mambo bila muongozo wowote na nivigumu sana kufanikiwa. Ukiwa na malengo ndio utajua ni bidhaa gani au huduma gani unatakiwa kuzalisha, wapi , lini na kwa ajili ya nini? pia ni njia zipi utapitia kuzalisha bidhaa au huduma yako.

2. NIDHAMU

Nidhamu ni sifa muhimu kwa Mjasiriamali kwani inamtenga na mambo mengi yasiyo kuwa na umuhimu. Mjasiriamali ni lazima awe na nidhamu ya maswala k**a vile matumizi ya muda pamoja na pesa. Kila Mjasiriamali anapaswa kujinyima na kukataa vitu vyote ambavyo hivimuwezeshi kufikia malengo yake. Mjasiriamali ni lazima atambue matumizi ya hiari na matumizi yasiyo ya hiari ili kuokoa upotevu wa pesa.

3. UJASIRI NA UTHUBUTU

Mjasiriamali ni lazima awe na ujasiri na uthubutu. Ujasiri na uthubutu ni sifa muhimu sana kwa Mjasiriamali ili aweze kutekeleza malengo yake. Ujasiriamali ni swala linalo hitaji sana ujasiri na uthubutu wa kufanya jambo na kuchukua maamuzi magumu hata k**a kuna changamoto au hatari mbalimbali zinazo ikabili shughuli yake au jambo lake.

Amini amini nawaambia, Huwezi kuwekeza pesa zako kwenye mradi au biashara yoyote k**a hutokuwa na ujasiri na uthubutu. Ujasiri na uthubutu hauta ruhusu hofu na mashaka ya kushindwa, kukata tamaa au kupata hasara vikutawale. Na siku zote hofu ni adui wa maendeleo tuna takiwa tumpige vita na tumshinde.

4. UBUNIFU

Mjasiriamali ni lazima awe ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kiakili, tena wenye ubunifu ndani yake, na pia autumie uwezo huu katika kuchambua matatizo mbalimbali yaliyo izunguka jamii ili kuyatafutia ufumbuzi. Ubunifu humtofautisha kati ya Mjasiriamali mmoja na mwingine. Mjasiriamali anahitaji ubunifu ili abuni wazo la pekee ambalo litampa matokeo mazuri katika shughuri zake. Wajasiriamali wengi hawana ubunifu ndiyo maana wanakwama.

Kwamfano, Mjasiriamali mmoja akianzisha biashara ya kuuza maandazi basi wengine 30 wataiga tena eneo hilo hilo moja. Mjasiriamali ni lazima uwe na ubunifu utakao kuwezesha kufanya mambo yenye tija.

5. UVUMILIVU

Kila jambo lina changamoto zake. Ujasiriamali unachangamoto nyingi sana ambazo zinahita subira na uvumilivu wa hali ya juu ili kuzimudu. Hivyo basi sifa ya kuwa na uvumilivu ni muhimu sana kwa kila Mjasiriamali anayetaka kufanikiwa. Haijalishi umepata hasara kiasi gani au umekutana na changamoto nyingi kiasi gani cha muhimu ni kuvumilia tu.

HITIMISHO

Nimatumaini yangu kuwa mpaka sasa utakuwa umezijua na kuzitambua sifa na tabia za Mjasiriamali. Naamini ukiwachunguza vyema wajasiriamali waliofanikiwa utabaini kuwa wanasifa na tabia hizi zilizo elezwa hapa. K**a wewe ni Mjasiriamali ni muhimu kuhakikisha unajitahidi kuwa na sifa na tabia zilizoelezwa hapo juu ili ufikie malengo yako.

ANGALIZO

Hichi ninacho fundisha sio kwamba ni kipya au kigeni hapana, hichi ninacho fundisha ndio kile kile ambacho walimu wengine wa maswala ya uchumi, biashara na Ujasiriamali wanafundisha katika madarasa yao. Mimi sio muelevu sana kuliko wengine hapana nakataa , bali hizi ni neema za Mungu kwangu katika kuwatumikia.

MAZINGATIO

Sifa na tabia za Mjasiriamali zipo nyingi sana hivyo tutaendelea kuangalia sifa nyingine zinazoendelea katika madarasa mengine ili tupate kujifunza mengi zaidi. Kitu pekee cha kuzingatia ni kusoma sana kwa bidii haya ninayokufundisha na kuyaishi ili uweze kufikia malengo yako.

MASWALI

Je umejifunza nini kwenye mada hii? Tafadhari tuandikie maoni yako hapo chini tutayasoma na kukujibu.

LIKE na SHARE page hii kisha M - TAG rafiki mwabie darasa linaendelea huku

@ Uncle Rama

Address

KIJITONYAMA
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kwaheri umasikini, mali ipo kitabuni posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Kwaheri umasikini, mali ipo kitabuni:

Share