Mesiah Consult Limited

Mesiah Consult Limited Broader land Co Ltd - is company that offers the following services:- Real estate, Town Planning

JE UNAFAHAMU MAANA YA URASIMISHAJI?Urasimishaji Makazi - Ni kitendo cha kutambua na kuboresha miliki za wananchi kwenye ...
23/12/2019

JE UNAFAHAMU MAANA YA URASIMISHAJI?

Urasimishaji Makazi - Ni kitendo cha kutambua na kuboresha miliki za wananchi kwenye maeneo yaliyoendelezwa bila kupangwa na kupimwa kisheria.

Urasimishaji ni zoezi shirikishi kwa sababu linatoa nafasi kwa kila mwananchi kukubaliana mipaka ya viwanja vyao ,kufungua njia na kutoa maeneo ya huduma za kijamii K**a vile shule, zahanati, maeneo ya wazi ,vituo vya polisi.

Yafahamu Malengo ya urasimishaji Makazi ni K**a ifuatayo:-

1. Kutambua ,kupanga, kupima na kumilikisha kila kipande ili kuongeza usalama wa miliki.

2. Kuongeza huduma za jamii na miundombinu ya msingi K**a vile barabara ,mifereji ya maji, maji ya mvua na masoko.

3. Kuongeza thamani ya ardhi na nyumba ya kuwawezesha wamiliki kutumia miliki hizo K**a rehani ili kupata mitaji kutoka taasisi za fedha.

4.Kupunguza migogoro ya ardhi hususani migogoro ya mipaka.

5. Kupunguza athari zinazotokana na majanga ya asili na magojwa ya mlipuko.

6.Kuongeza wigo wa mapato ya serikali yatokanayo na rasilimali ardhi.

Kwa ushauri wowote juu ya maswala ya ardhi na urasimishaji usisite kuwasiliana nasi kwa namba 0717311995 / 0769881795

Ardhi ni dhahabu

MAMBO MATATU MUHIMU YA KUZINGATIA   UNAPONUNUA ENEO AU KIWANJA1. Uhakiki wa Matumizi ya ardhi√ Matumizi ya ardhi yamegaw...
19/12/2019

MAMBO MATATU MUHIMU YA KUZINGATIA UNAPONUNUA ENEO AU KIWANJA

1. Uhakiki wa Matumizi ya ardhi

√ Matumizi ya ardhi yamegawanyika katika namna ya mbalimbali K**a vile matumizi ya viwanda, kilimo,taasisi, biashara, ibada na huduma za kijamii. Wakati wa kununua eneo lako jitahidi unahakiki matumizi ya eneo hilo kwa ufasaha.

JE NI ATHARI IPI UTAIPATA USIPOHAKIKi MATUMIZI YA ENEO UNALOTAKA KUNUNUA? l

√ Athari kubwa kabisa ni kwamba, unaweza ukajikuta eneo ulilonunua haliendani na matumizi unayohitaji kuyafanya wewe, mfano inawezekana umenunua eneo kwa ajili ya kujenga nyumba kwa ajili ya matumizi makazi lakini kwa bahati mbaya kumbe hilo eneo ni eneo la wazi( open space) au ni eneo la viwanda, maana yake ni kuwa unaweza kuendelea na ujenzi wako wako wa nyumba mpaka kukamilika na kuhamia kabisa kwa ajili ya makazi yako, ila siku itakapofahamika kuwa eneo hilo ni eneo la wazi (open space) au eneo ni eneo lisiloendana na matumizi uliyoweka, nyumba yako itabomolewa bila fidia yeyote, kwa maana hiyo utakuwa umepata hasara mbili yaani hasara ya kununua eneo pamoja na hasara ya ujenzi.

2. Kuhakiki sehemu ya kiwanja

√ Hapa napenda kuzungumzia location ya kiwanja, unaponunua eneo la kiwanja jaribu kukagua kikamilifu K**a eneo hilo liko nje ya mfumo wa miundombinu K**a vile bomba la gesi, maji au mafuta, pia angalia K**a eneo lipo nje ya njia kuu ya umeme, mwisho angalia K**a sehemu hiyo ipo nje ya mkondo wa maji ya mvua. K**a eneo lipo nje ya mkondo wa maji ya mvua Wala halijaguswa na mfumo wa miundombinu wowote, basi unaweza nunua hilo bila shaka yoyote.

3. Uhakiki wa Umiliki wa kiwanja

Kabla ya kununua eneo kwanza kumbuka hakuna kipande Cha ardhi hapa Tanzania ambacho hakina mtu anayekimiliki.
Kila kipande Cha ardhi kina mmiliki wake, kwa hiyo kabla ya kutoa pesa yako kununua eneo hilo, jiridhishe kwanza kuwa huyo anayekuuzia ndie mmiliki halali wa eneo hilo.

√ Pia K**a eneo lina hati miliki unaweza kwenda kwa msajili wa hati( registrar of title) ili kunijiridhisha juu ya mmiliki halali wa eneo hilo, ama K**a eneo hilo Lina kizuizi chochote, hiyo itakusaidia kuepuka migogoro ya Umiliki unaweza kujitokeza mbele.

✓ Mwisho, Zingatia Mambo matatu hapo juu, ili kujenga dhamana ya kudumu ya eneo unalopanga kununua na pamoja na kuepuka harasa, migogoro ya ardhi.

HIVYO BASI KWA USHAURI WOWOTE JUU YA UNUNUZI WA ENEO; WASILIANA NASI KWA NAMBARI YA SIMU TAJWA HAPO CHINI. USHAURI NI BURE.
0717311995/ 0769881795

ni dhahabu #

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255785906510

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mesiah Consult Limited posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Mesiah Consult Limited:

Share