24/07/2021
Najua baadhi yenu humu ni wataalamu wa masuala ya anga pia, sasa leo nataka tupeane fact za kutisha kuhusu sayansi ya anga za juu au fact nyingine yoyote lakini lazima iwe ya sayansi; mimi nitaanza na hii kuhusu eneo linalotisha zaidi kuwahi kugunduliwa na wanasayansi Ulimwenguni, hili eneo linaitwa Boötes void au kwa jina lingine linafahamika k**a Great Void ambalo lipo umbali wa miaka milioni 700 ya mwanga kutokea huku Duniani, hili eneo linatisha sana kutokana na weusi wake k**a inavyoonekana hapo kwenye picha yaani sehemu zingine zote kumezungukwa na nyota isipokuwa hapo katikati kwenye weusi ambapo mpaka leo hii wanasayansi wanashindwa kuelewa ni kwanini eneo hilo Ulimwenguni kuwe wazi hivyo. Hili eneo limetanuka kwa ukubwa wa miaka milioni 250 ya mwanga kutokea upande mmoja hadi mwingine, ukubwa ambao ni sawa na asilimia 0.27% ya kipenyo kizima cha Ulimwengu wetu wote ambao wenyewe umetanuka kwa miaka bilioni 93 ya mwanga kutokea upande mmoja hadi mwingine. Hili Boötes void kwa sasa ndilo eneo tupu kubwa zaidi kuwahi kugunduliwa na wanadamu na mpaka leo hii hakuna mtu anayefahamu ni kwanini eneo hili Ulimwenguni lipo tupu na nini ambacho kimesababisha eneo hili la Ulimwengu kuwa tupu bila hata chembe ya nyota, jambo la kutisha zaidi ambalo wanasayansi wanaamini kwa sasa ni kwamba hili Boötes void inaweza ikawa ndiyo mwisho wa Ulimwengu kwa maana hapo ndipo Ulimwengu wetu unapoishia na viumbe vyote Ulimwenguni huwa vinaangamiziwa hapo na pia Boötes void ndiyo inaweza ikawa sababu kwanini mpaka sasa hatujaona viumbe wengine (Aliens) kwa maana walikuwepo kwenye huu Ulimwengu wakaishi k**a sisi kisha wakaangamizwa na sisi pia tutapitia njia hiyo hiyo kuelekea kwenye hilo Boötes void na tukiangamizwa watakuja viumbe wengine yaani hivyo hivyo hii nadharia inafahamika k**a Kardashev III scale civilization, naomba niishie hapa. Tupe fact yako wewe ya kisayansi ya kutisha?