Usalama wa Raia Saccos

Usalama wa Raia Saccos Huduma ya akiba na mikopo Ndani ya wizara ya mambo ndani ya nchi

Salaam za Mei Mosi   tanzania
01/05/2026

Salaam za Mei Mosi



tanzania

Tunawatakia maadhimisho mema ya siku ya Muungano.
26/04/2026

Tunawatakia maadhimisho mema ya siku ya Muungano.

Salaam za Pasaka
05/04/2026

Salaam za Pasaka

Salaam za Eid. tanzania
21/03/2026

Salaam za Eid.
tanzania

 ELIMU YA URA SACCOS LTD YAWAFIKIA WANACHAMA WA MABWEPANDE WILAYA YA KINONDONI Katika kuwajengea uelewa wa kifedha na uw...
19/03/2026



ELIMU YA URA SACCOS LTD YAWAFIKIA WANACHAMA WA MABWEPANDE WILAYA YA KINONDONI

Katika kuwajengea uelewa wa kifedha na uwekezaji ndani ya ushirika, timu ya URA SACCOS LTD ikiongozwa na Meneja wa URA SACCOS Tawi la Dar es Salaam Mrakibu wa Polisi Edwine Mkole imewapatia wanachama wa Mabwepande elimu ya fedha, maandalizi ya kabla na baada ya kustaafu, sheria na kanuni mbalimbali zinazoongoza ushirika nchini, huduma za kijamii zitolewazo na URA SACCOS pamoja na mrejesho wa Maazimio ya Mkutano Mkuu wa 16.

 URA SACCOS LTD IMETOA ELIMU YA USHIRIKA KWA WANACHAMA WA WILAYA YA KIGAMBONITimu ya URA SACCOS LTD ikiongozwa na Mrakib...
19/03/2026



URA SACCOS LTD IMETOA ELIMU YA USHIRIKA KWA WANACHAMA WA WILAYA YA KIGAMBONI

Timu ya URA SACCOS LTD ikiongozwa na Mrakibu Msaidizi wa Polisi Salimu Mwakasa ambaye ni Afisa Uhusiano Tawi la Dar es Salaam Leo tarehe Machi 19, 2026 wameendelea kutoa elimu ya ushirika ikiwa na lengo la kuwajengea uelewa wanachama juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na URA SACCOS.

Sambamba na hilo msisitizo kwa wanachama ulitolewa katika kuitumia URA SACCOS katika kujiwekea malengo yao ya muda mrefu na wa kati kiuchumi kwa kuweka Akiba, Amana na Hisa kwani kwa sasa ni rahisi zaidi kupitia mfumo wa kidijitali wa chama wa URA Mobile sehemu yoyote na muda wowote mwanachama anaweza kujihudumia kupitia simu yake ya kiganjani.

 ZINGATIENI UWEKEZAJI WA KUDUMU KATIKA KUIMARISHA KIPATO CHENU.Mwakilishi wa URA Saccos Ltd Mkoa wa Arusha Koplo wa Poli...
19/03/2026



ZINGATIENI UWEKEZAJI WA KUDUMU KATIKA KUIMARISHA KIPATO CHENU.

Mwakilishi wa URA Saccos Ltd Mkoa wa Arusha Koplo wa Polisi Chiunda David ametoa wito kwa askari wa kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo Nchini (STPU) Mkoani Arusha, kuzingatia uwekezaji wa kudumu ikiwa ni pamoja na kununua hisa katika katika kujiimarisha kiuchumi na kuongeza ustawi wa Mfuko.

CPL Chiunda ametoa wito huo Machi 17, 2026 wakati akitoa elimu maalumu ya fedha katika kikao kazi cha kikosi hicho ambapo amesema kuwa ni vyema mwanachama kuwa na utamaduni wa kukuza kipato chako kwa kufanya uwekezaji wa kudumu kwa kununua hisa ndani za URA SACCOS Ltd pamoja kuweza katika fursa zilizopo Jijini Arusha ikiwemo fursa ya ardhi.

Aidha wanachama hao wamekumbushwa kuongeza akiba kwenye saccos yao pamoja na kujipatia elimu ya fedha na uwekezaji.

Hata hivyo washiriki wa elimu hiyo walipata fursa ya kutoa maoni yao kuhusu namna ya bora ya kuboresha ustawi wa mfuko na ustawi wao binafsi.

 URA SACCOS LTD IMEENDELEA KUTOA ELIMU KWA WANACHAMA WAKE WA MKOA WA TANGAKatika kuutekeleza msingi wa tano wa ushirika,...
19/03/2026



URA SACCOS LTD IMEENDELEA KUTOA ELIMU KWA WANACHAMA WAKE WA MKOA WA TANGA

Katika kuutekeleza msingi wa tano wa ushirika, URA SACCOS Ltd imewafikia wanachama wake mkoa wa Tanga leo tarehe 19/03/2026 na kuwapatia elimu juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na chama na umuhimu wake katika kujikwamua kiuchumi na namna ya kuwekeza ndani ya chama.

Aidha wanachama hao walisisitiziwa juu ya elimu ya maarifa ya fedha katika maandalizi ya kustaafu pamoja na umuhimu wa matumizi ya mfumo wa kidijitali wa URA Mobile ambao unawasaidia kupata huduma za chama kirahisi kupitia simu zao za viganjani na kuweza kujihudumia popote walipo na muda wowote.

 Msingi wa tano wa ushirika umeendelea kutekelezwa kwa vitendo kwa wanachama wa URA SACCOS wilaya ya Igunga kupewa elimu...
19/03/2026



Msingi wa tano wa ushirika umeendelea kutekelezwa kwa vitendo kwa wanachama wa URA SACCOS wilaya ya Igunga kupewa elimu ya ushirika.

 URA SACCOS IMEENDELEA KUUTEKELEZA MSINGI WA TANO WA USHIRIKA KWA VITENDO KWA KUTOA ELIMU YA USHIRIKA KWA WANACHAMA GEIT...
19/03/2026



URA SACCOS IMEENDELEA KUUTEKELEZA MSINGI WA TANO WA USHIRIKA KWA VITENDO KWA KUTOA ELIMU YA USHIRIKA KWA WANACHAMA GEITA

Machi 19, 2026 katika ukumbi wa Bwalo la Polisi mkoani Geita, Watendaji kutoka URA SACCOS Kanda ya Ziwa, Mkaguzi wa Polisi (INSP) Godfrey Pallangyo ambaye ni Afisa Mikopo, na Heri Mtemaluge, Afisa Tehama, wametoa elimu na mrejesho kwa wanachama wa URA SACCOS wa wilaya ya Geita juu ya maazimio ya Mkutano Mkuu wa 16 uliofanyika Novemba 2025 mkoani Arusha na masuala mbalimbali yanayotarajiwa kutekelezwa kwa mwaka 2026.

INSP Pallangyo amefafanua masuala ya kifedha na maboresho ya huduma za mikopo, huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia taratibu na kuongeza nidhamu ya fedha ili wanachama wanufaike zaidi na huduma za chama.

Kwa upande wake, INSP Mtemaluge amesisitiza matumizi ya mifumo ya kidijitali na kuwahimiza wanachama kuendana na teknolojia ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na kuongeza uwazi katika shughuli za ushirika.

Aidha, wanachama wamepatiwa elimu ya ushirika ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uelewa wao kuhusu haki na wajibu ndani ya chama.

Tunawatakia wanawake wote maadhimisho mema ya siku ya mwanamke duniani.
08/03/2026

Tunawatakia wanawake wote maadhimisho mema ya siku ya mwanamke duniani.

Address

Kilwa Road
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00

Telephone

+255677026301

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Usalama wa Raia Saccos posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share