14/09/2024
"Family & Seasons".. ili kutoka chini kupanda juu unahitaji watu wa kukushika mkono " Destiny helpers ".
Imagine wewe na rafiki yako nyote wawili mmekaa kwenye viti, ni ngumu sana mmoja wenu kumuinua mwingine lakini ukiwa umekaa ukashikwa mkono na Mtu aliyesimama ni rahisi sana kukuinua.
That's Why ili kufanikiwa hauhitaji kubadilika wewe tu ila unahitaji kuwa katika Circle ya watu ambao watachochea zaidi mafanikio yako na ukuaji wako.
Hao ni watu wa muhimu sana.
Kuna nyakati utapitia " Rock bottom " hii ni sehemu ambayo asilimia kubwa sana ya watu waliokuwa na ndoto kubwa na malengo wakifika hapa wanaona kila kitu walichodhani kinawezekana kutokea hakiwezekani tena kuwa kweli.
Hapa utapitia changamoto za kila aina, utajiona hufai, utapitia madeni, Biashara itasimama na utaona kabisa ndoto kubwa uliyokuwa nayo imeishia kuwa njozi.
Hawa watu ni wale ambao watakuwa na wewe hata pale ambapo wewe huwahitaji wawe Karibu yako lakini wao watachagua kusimama na wewe haijalishi nini unapitia wakati huo watakuonyesha uwezo mkubwa ulionao ndani yako hata k**a wewe ilikuwa hufahamu hilo.
Hawaishii tu kuwa Destiny helpers ila hao ni familia haijalishi umekutana nao kwenye mazingira gani.
K**a ambavyo unatamani sana kubadilisha hali yako ya sasa ndivyo ambavyo unatakiwa kutamani zaidi kuongeza aina hii ya watu wawe karibu yako.
" Your network is your networth ".
Unahitaji kuwa na watu sahihi wanaofanya jambo sahihi kwa wakati sahihi.
Wewe unao hao watu.?